KERO Bar ya Camp Edward (Tabora) wanapiga muziki mkubwa sana na IPO katikati ya makazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Prince05

Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
43
Reaction score
84
Bar ya CAMP EDWARD iliyoko kwenye makazi ya watu MKOANI TABORA, wanapiga mziki mkubwa sana na mbaya zaidi ni kila siku hawana jumatatu wala weekend, mbaya kuliko zote wanapiga mziki hadi saa mbili asubuhi kwa sauti kubwa.

Mamlaka zituambie ni kibali cha aina gani wanapewa kupiga mziki hadi asubuhi au kupiga mziki sauti juu kila siku na wanajua wako kwenye MAKAZI YA WATU?
 
Gentleman,
ni vizuri kero hii ikawasilishwa kwa mamlaka husika in details, ili hatimae hatua muafaka kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kumlazimisha mwenye bar ya CAMP EDWARD kuweka mazingira ya soundproof, ikiwa atashindwa kuacha kusitisha shughuli zenye muziki wenye kelele unaoleta usumbufu kwa wakazi walio jirani na bar hiyo, nadhani itapendeza zaidi
 
Wanapiga mpaka saa ngapi. Kama ni mpaka saa sita usiku basi kuweni tu wapole. Vipi, kuna wahudumu wazuri?
 
Pia sheria ina decibel level ya kupiga mziki watalazimishwa kuifata hiyo level
 
Moja ya taasisi za hovyo nchini ni NEMC
 
Poleni kwa Bata.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…