Bar zinavyochipuka ukanda wa Mbezi Beach

Bar zinavyochipuka ukanda wa Mbezi Beach

Mbezi Beach ilishakongoroka kitambo tu mbona.

Kwa sisi ambao tumeiona Mbezi Beach tangu inajengeka, tumejenga huko tangu enzi za Nyerere, tumeliona hilo Tangi Bovu tangu lilipokuwepo zima, tumepewa mashamba ya kukatiwa na CCM bure huko siku hizo, Mbezi Beach ilishakongoroka miaka 10 iliyopita.
Mjuaji wa jamii forum... Hakuna kitu usichojua.
 
Bar Ni moja tu... KB Bar kisima Cha burudani iko pale Tegeta pale karibu na Brazil Bar.
 
Mjuaji wa jamii forum... Hakuna kitu usichojua.
Unaona hivyo kwa sababu vitu nisivyovijua sichangii.

Kuna uzi wa vitongoji vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa kachangia sana Mshana Jr. anayeijua mitaa hiyo, mimi sijachangia kwa sababu si mitaa yangu hiyo.

Sasa unataka nisichangie uzi unaojadili habari za mtaa wangu?
 
Sijui Kwa nini JF ukielezea vitu kadha wa kadha unaishia kupewa majina [emoji848]

Negativity all over the forum
 
Sijui Kwa nini JF ukielezea vitu kadha wa kadha unaishia kupewa majina [emoji848]

Negativity all over the forum
Nilikuwa napinga sana ku simplify vitu kwa minajili ya "ni wivu tu".

Lakini sehemu nyingine hamna jinsi. Inaonekana "Ni wivu tu" ina apply.

Mtu anaona uchungu mimi kuijua Mbezi Beach tangu enzi za Nyerere.

Kwani yeye kakatazwa kuandika kwenye uzi wa kijiji chao?
 
Huyo jamaa ni kiboko, hakuna asichojua [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Anakera saana yaani hakuna hata siku moja kikasemwa kitu Asilete ujuaji wake labda kiwe hakimpi maujiko Kama kile Cha mitaa ya mwananyamala kakaushia akamwacha mshana Jr aangaike na uswazi.
Ulipokuja mjadala wa kishua anasema amejenga mbezi kipindi Cha Nyerere. [emoji1787][emoji1787]
Kweli JF hakuna mtu choka mbaya kila mtu Ni wa kishua.
 
Wewe ile Bar duuh, Brazil imekufa hatari Whats Up imeifunika Brazil kwa mapochopocho yale
KB Bar haifi... Ilikuja China Bar imekufa, ikaja WhatsApp naona inachechemea. Pale Club 71 ya kibo ishajifia.
Lakini KB Bar inarindima daily na vibe Lile lile daily.
 
Nilikuwa napinga sana ku simplify vitu kwa minajili ya "ni wivu tu".

Lakini sehemu nyingine hamna jinsi. Inaonekana "Ni wivu tu" ina apply.

Mtu anaona uchungu mimi kuijua Mbezi Beach tangu enzi za Nyerere.

Kwani yeye kakatazwa kuandika kwenye uzi wa kijiji chao?
Endelea kujinadi maana JF kila mtu ana gari na kila mtu kasoma abroad, Mimi tu ndo natokea Ludewa isipokuwa wakina kiranga na wenzie machino.
 
Huyo jamaa ni kiboko, hakuna asichojua [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwanza Hii Avatar Ni ya jamaa naemheshimu na kumkubali saana bw Humble African? Ni wewe au? Ilikuwaje na wewe ukaweka hiyo Avatar? What's the story behind?
I'm curious?
 
Endelea kujinadi maana JF kila mtu ana gari na kila mtu kasoma abroad, Mimi tu ndo natokea Ludewa isipokuwa wakina kiranga na wenzie machino.
Unahisi hayo maneno yatabadili uhalisia?. Endelea kupambana mkuu.
 
Endelea kujinadi maana JF kila mtu ana gari na kila mtu kasoma abroad, Mimi tu ndo natokea Ludewa isipokuwa wakina kiranga na wenzie machino.
Wewe umeona kuwa na gari na kusoma abroad ndiyo kuyapatia maisha?

Unanitafuta nifunguke halafu useme zaidi Kiranga anajitapa siyo?

Wewe kama una roho ndogo mimi nikieleza maisha yangu ya kawaida tu lazima utaona najitapa.

Hayo maisha ya magari na kusoma abroad kwetu nimeyakuta kabla sijazaliwa.

Acha kijiba cha roho.
 
Kwanza naunga mkono kauli ya RC mstaafu wa Mwanza kuwa "watu wanywe bia maana bia ni uchumi" Lakini pamoja na hilo siku za karibuni kumeibuka mfululizo wa bar ukanda wa mbezi beach ya chini hali inayopelekea mtaa kukosa utulivu hii imepelekea hata baadhi ya wasanii kuhama mjini sinza na kufata viwanja Mbezi beach.

Ongezeko la bar linaweza kuleta vitendo vya uhalifu, mapaka, madawa ya kulevya na kuharibu sifa ya mtaa. Bar zenyewe zinajaa watoto wa shule za kata wanyoa viduku na vidangaji vya kutoka uswahilini Kawe. Ukiondoa Oysterbay na Masaki mtaa unaofuatia kwa ustaarabu na makazi yenye utulivu ni Mbezi beach ila tunapoelekea sasa utakuwa mtaa wa fujo. Mwanzoni zilianza kumbi za sherehe, sasa hivi bar nani anajua kitakachofuatia?

Mipango miji tupeni jicho pande hizi kuna mitaa itunzwe na kuheshimiwa kama makazi mfano Mbezi beach, Mikocheni, Mbweni na Ununio na mitaa mingine ibaki ya starehe kama Sinza, kinondoni, Tabata n.k.

Baadhi ya bar hizo ni:
Rainbow
Juliana
Kidimbwi
Na nyingine nyingi siwezi taja zote wino utaisha.
Kumbe
 
Usiwe na wasiwasi sana Baa ambazo zitabaki muda mrefu ni hizo Juliana, Nyambizi, Amsterdam,Kidimbwi . Hilo eneo la mbezi ya chini maarufu kwa zena kawawa sasa hivi ndio eneo hot kwa starehe za usiku. Wale dada popobawa wasiolala wanatoka tabata kuja kujiuza huko juliana, kidimbwi na hata mawela.

Juzi kulitokea ujambazi hapo Juliana akuwawa Jimson Kibiki na hao wezi walimpora maeneo ya juliana.

Baa hizi pia zinaleta mkusanyiko wa watu wasio wema, madalali wa sinza wote wamehamia juliana wanashinda hapo na vijana wa sinza wanajulikana wao ni pesa mbele deal yoyote watapiga. Baa hizi zinakwenda kuharibu ule utulivu uliokuwepo.

Shopping malls zinazoibuka pande hizo ni hatari pia.
Apo Juliana kuna watoto wazuri sana
 
Sio njaa yenu ndio imewafanya kila nyumba muweke fremu zinazogeuka bar? Hata Masaki nyumba za waswahili hasa waliokopeshwa na serikali ndio zimejaa fremu na kuleta vurugu. Mimi nakaa uswahili ila nimegoma kabisa kuweka hizo fremu kwasababu sitaki vurugu nje kwangu.
Watu wa mbezi beach,oysterbay wasingeendekeza njaa na kufungua vifremu kusingekuwa na vurugu huko, wakazi wa uswazi wanaokuja kunywa bia huko mnawaonea tu.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Wewe umeona kuwa na gari na kusoma abroad ndiyo kuyapatia maisha?

Unanitafuta nifunguke halafu useme zaidi Kiranga anajitapa siyo?

Wewe kama una roho ndogo mimi nikieleza maisha yangu ya kawaida tu lazima utaona najitapa.

Hayo maisha ya magari na kusoma abroad kwetu nimeyakuta kabla sijazaliwa.

Acha kijiba cha roho.
Una maisha gani kiranga? Kutwa unashinda JF. Unafanya kazi muda gani kwanza? [emoji1787][emoji1787]
 
Una maisha gani kiranga? Kutwa unashinda JF. Unafanya kazi muda gani kwanza? [emoji1787][emoji1787]
Wewe unataka nikuambie kwamba upeo wa mawazo yako ni kwamba kila mtu anafanya kazi.

Hujui wengine inawezekana hatufanyi kazi, tumewekeza hela inatufanyia kazi.

Wengine ni "Trust Fund Babies".

Do you even know what is a Trust Fund?[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom