Bar zinavyochipuka ukanda wa Mbezi Beach

Bar zinavyochipuka ukanda wa Mbezi Beach

Niliagiza bucket Juliana...nilikuwa nimekaa karibu na vijana kadhaa karibu ,Ile naangalia pembeni si wakachomoa vinywaji......kweli vijana wa uswahili wanaharibu Sana image ya hizi bar siku hizi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kuna siku bucket 6 zilienda kimasihara tu mbezi huko huko.
Nashuhudia
 
Kulikuwa na kiwanja fulani masaki mwisho jeshini pale kulikuwa na mishikaki sana

Kiwanja kilikuwa kimetulia sana walikuwa wanaenda watu fulani wanao jielewa
Kuna mazingira fulani ukiyaweka automatically watoto wenyewe wanapakimbia eneo

Ova
Karibu kaites tbt
 
Pale Junction kutokea tangi bovu kama unaelekea kwa mboma katikati pale nakumbka
Mke wa e.mmry alikuwa na eneo kubwa ilikuwa shamba ,majirani pembeni walikuwa wakina mataka...
Watu walipoanza kuhamia huko nakumbka kulikuwa na uvamizi sana majumbani watu walingiliwa sana

Ova
Kama unaelekea shule ya msingi Mwalimu Nyerere. Siku hizi kuna “kiwanja” fulani kinatazamana na hiyo shule huwa kinachanganya sana mwisho wa wiki.

Kuna nyumba ya waziri wa kilimo miaka ya Nyerere panafugwa ng’ombe ndani ya hiyo nyumba.
 
Kujazana kwa watu kwenye hizo bar ulizozitaja kunachangiwa na bei ya vinywaji kuwa chini, bei ikiwa chini uwavutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali, hali hii ikitokea amani au ustaarabu kwenye maeneo hayo utoweka. Mbona Mbezi kuna bar nzuri tu tena zenye watu waliostaarabika, mfano Pit Stop na kwa Tegeta jengo la Kibo Complex kuna Castle Lounge huko vibinti vyenye viduku hautovikuta wala kuibiwa bia, naamini bei siku zote ndio umfanya mtu achague wapi kwa kwenda.
Japo nimetundika daruga kwenye kupiga masanga, ila naamini siku zote ili akili ifanye kazi inahitaji utulivu na kukutana na watu wenye mawazo chanya, bar kama Juliana, Kidimbwi ,Kitambaa Cheupe, Brazil tegeta, Whatsapp, Great park- Tabata, Forty Forty-Tabata Bima,Micasa Lounge na nyinginezo kama hizo ni nadra sana kukutana na watu wenye mawazo chanya, huko usitegemee kupata dili la maana ila tegemea kuibiwa au kujeruhiwa, bar za namna hizo zimejaa wahuni na malaya waliokubuhu ukitaka kwenda huko jiandae kwa lolote litakalokutokea.​
 
Kuna bar za malegend bado zipo dar ukienda bado unakalia viti vile vya chuma za longtime
Hakuna mambo ya bucket na mambo mengine
Mwendo wa vyombo tu

Ova

Kisuma bar, riverside bar, maryland bar, etc
 
Kwanza naunga mkono kauli ya RC mstaafu wa Mwanza kuwa "watu wanywe bia maana bia ni uchumi" Lakini pamoja na hilo siku za karibuni kumeibuka mfululizo wa bar ukanda wa mbezi beach ya chini hali inayopelekea mtaa kukosa utulivu hii imepelekea hata baadhi ya wasanii kuhama mjini sinza na kufata viwanja Mbezi beach.

Ongezeko la bar linaweza kuleta vitendo vya uhalifu, mapaka, madawa ya kulevya na kuharibu sifa ya mtaa. Bar zenyewe zinajaa watoto wa shule za kata wanyoa viduku na vidangaji vya kutoka uswahilini Kawe. Ukiondoa Oysterbay na Masaki mtaa unaofuatia kwa ustaarabu na makazi yenye utulivu ni Mbezi beach ila tunapoelekea sasa utakuwa mtaa wa fujo. Mwanzoni zilianza kumbi za sherehe, sasa hivi bar nani anajua kitakachofuatia?

Mipango miji tupeni jicho pande hizi kuna mitaa itunzwe na kuheshimiwa kama makazi mfano Mbezi beach, Mikocheni, Mbweni na Ununio na mitaa mingine ibaki ya starehe kama Sinza, kinondoni, Tabata n.k.

Baadhi ya bar hizo ni:
Rainbow
Juliana
Kidimbwi
Na nyingine nyingi siwezi taja zote wino utaisha.
Shida ni Nini?,Hawalipi kodi?.
 
Acha watu wachape starehe bana, kama we mlokole wenzio wana njia zingine.
Umetaja mambo yote mazuri yanayopatikana kwenye hizo bar,, bado unataka zidhibitiwe!

Samahani lakini,, tupige ulabu na hizo totoz.
 
Kwani segerea iko wapi?!
Kimanga, bima, kinyerezi, segerea zote zipo ndani ya tabata
Nilikuwa natafuta tu uhakika kama ndio hiyo kwa sababu siijui wala sijawahi kufika ila najua inakaribia kufungiwa muda si mrefu
 
Mrangi wewe ni mkazi wa pale nyuma ya BOT flats karibu na yule mzee mwenye nafasi kubwa ndani ya Chama tawala?.
Nyie wazee wa upanga si ndy mlipawahi mbezi beach naona mlitaka iwe kama upanga 😂😂
Wale wa sinza walihamia tabata

Ova
 
Back
Top Bottom