Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

US Dollar ni sarafu bora kuwa nayo kwa sasa hivi na kushindana nayo inabidi uwe na uchumi imara.
Africa tungeanza na kuwa na uchumi imara kwanza.
 
Ndio tunatakiwa tuchague au kupendekeza jina moja.... Mfano Euro, inatumiwa Ulaya, kila nchi inatumia Euro barani ulaya...

Afrika napo tunataka Sarafu yetu ili kuepuka misukosuko ya Dollar kupanda na kushuka... Wewe unapendekeza jina gani, na namna ipi tufanye hii sarafu kuwa Hai
Mnaota!!mambo madogo madogo tu yamewashinda sembuse hilo?!!
 
Mkishaanzisha hiyo sarafu bado mnatakiwa kulipa madeni yenu ambayo ni trilioni za dola kwa US$ na wala sio kwa hiyo sarafu mtakayoanzisha.

Na bado kuna kukopa na misaada mingine ambazo nazo bado zitatolewa kwa dola ya Marekani, hivyo hayo ni mambo ya kwenye vijiwe vya tangawizi tu.
Kuanzisha Sarafu yetu ni kwa ajili ya Biashara zetu za Ndani ya Afrika... Suala la Deni la Taifa hiyo ni kesi ya nchi binafsi, tunachotaka ni kuwa Tanzania ikifanya biashara na South Africa basi tutumie fedha yetu na si kutumia Dollar ambayo ikiyumba na Sisi tunayumba... Sarafu yetu itakuwa kwa ajili ya matumizi ya bara la Afrika kama ilivyo Euro kwa bara la Ulaya
 
Hivi karibuni kumekuwa na uhaba wa sarafu ya Dollar Duniani, kitu ambacho kimepeleka pia sarafu za nchi nyingi barani Afrika kuyumba, na vitu kupanda bei bila mpangilio.

Kwa sababu mimi pia ni Admin wa page moja ya facebook inayoitwa Icon Africa ambapo humo tupo ma-Admin wengi kutoka nchi za Afrika na kila mmoja anapost mambo ya nchi yake ususani utalii. Basi nikaamua kwenda kwenye page kuuliza ni namna gani tuwaweza kuwa na pesa yetu ya bara la Afrika ili kuepuka madhara ya Dollar.

Na kama mnavyojua nchi zetu nyingi za kiafrika bado zinatumia sarafu ya Dollar kufanya manunuzi sehemu mbali ndani na nje ya bara la Afrika. Hivyo ukosefu wa sarafu ya Dollar imepelekea pia nchi nyingi kutikisika kiuchumi. lakini endapo tungekuwa na sarafu yetu ya bara la Afrika kama jinsi ilivyo sarafu ya Ulaya (Euro [emoji387] €), basi tutakuwa imara kiuchumi, hata kama dollar ikitikisika, sisi bado tutakuwa salama. Na pia tutaweza kufanya manunuzi ndani ya bara letu bila kutatizwa na kupanda na kushuka kwa sarafu ya Dollar.

Nimeanza kuona muitikio mkubwa wa watu mbalimbali kwenye comment za hiyo post wakipendekeza Sarafu iitwe Afro au Afric. Na muitikio ni mkubwa na kila mwafrika anatamani tuwe na sarafu yetu. Haya maoni ni namna gani yanawezwa kufikishwa Africa Union na yakafanyiwa kazi kwa haraka. Maana sidhani kama kuna nchi ya kiafrika inataka kuendelea kuikumbatia dollar
Ule mpango wa Putin uliishia wapi?
 
Hata Uingereza inatumia Euro?
Uingereza inatumia Pound... Lakini usitake kuleta mambo ya uingereza hapa... Hapa sisi tunazungumzia Uchumi wa Afrika na biashara za ndani ya bara la Afrika bila kutumia Dollar ambayo ikiyumba vitu vinapanda bei
 
Kweli tutamkumbuka sana mwamba Gadaffi na wengine waliokuwa na mawazo haya
Hongera zako mkuu ila kwa Africa ni waoga sana mpaka mito yao ya maji hawana uhuru nao
Kila kitu tunaogopa kufanya

Leo kama tuna akili tungekuwa na matajiri wakubwa duniani kwa kuwa na maduka ya almasi na dhahabu kuanzia London, Paris na NY hata Dubai
Ila hizi ni ndoto zangu tu
Kweli kabisa... Yani inashangaza hata humu jamii forum kuna watu wanakuja na kusema eti ni jambo lisilowezekana... Akili zetu wa Afrika ni za kufikiri kushindwa tu ndio maana Bara linabaki nyuma kila siku
 
Swali fikirishi je ni kwa kiasi gani nchi za kiafrika zinafanya biashara baina yao?
Hazifanyi baina yao ambapo pia moja wapo ya sababu ni uaba wa Dollar... Kenya ikiuza TV haitataka kuiuzia Tanzania kwa sababu Shilling yetu haina nguvu, watataka kutuuzia kwenye Dollar, na kwenye Dollar napo Tanzania ina uaba hivyo Kenya atalazimika kupeleka bidhaa zake kwenye nchi zenye Dollar nyingi ili alete Dollar Nchini kwake... Sasa wewe unauza kitu hili upate Dollar, alafu ukamuuzie tena mwenzako ambae naye hana Dollar kama wewe? Ndio maana nchi nyingi za Afrika zinafanya biashara na nchi za nje ya bara la Afrika sababu kuu ni kwenda kuitafuta Dollar... Sasa tukiwa na sarafu yetu basi biashara zetu hazitahitaji tena kutumia Dollar bali sarafu yetu wenyewe tunakuwa tunafanya nayo biashara
 
Mpango wa kuipatia dola jina lingine ila thamani yake itabakia pale pale....jamani Waafrika tufanye kazi.
Lengo kuu la Sarafu ya Afrika ni kwa ajili ya kufanya biashara ndani ya bara la Afrika. Hivi leo ili ununue Nigeria kiatu inatakiwa uwe na Dollar, hivyo mnaijeria huyo kuliko kukuuzia kwa Dollar hiyo anaona bora akamuuzie mmarekani mwenyewe hili apate Dollar original kuliko kuunga unga biashara na wewe mtanzania mwenye Dollar ya kubangaiza... Sasa lengo la sarafu ya Afrika ni kuvunja huu mlango wa Dollar... Hata kama thamani ya Dollar itabaki pale pale hiyo sisi haituhusu, kinachotuhusu ni kuweza kufanya biashara zetu ndani ya Afrika bila kushawishiwa na Dollar
 
Kweli aisee! Hili lipo tricky sana
Mbona Euro wameweza na wanauziana na kufanya biashara kwa pesa yao... Hakuna cha tricky hapo, au unamuogopa mmarekani kiasi hicho... Dollar yake ibaki pale pale, ila huku kwetu ndani ya Afrika tufanye biashara kwa pesa yetu
 
Kweli kabisa... Yani inashangaza hata humu jamii forum kuna watu wanakuja na kusema eti ni jambo lisilowezekana... Akili zetu wa Afrika ni za kufikiri kushindwa tu ndio maana Bara linabaki nyuma kila siku
Confidence hakuna kwa mswahili yaani kila kitu anaona hawezi
Mbona kuiba wwnaweza? Kwanini wasiibe maarifa?
Kweli continent lote linategemea misaada tu kila kukicha
 
Ndicho nilichosema mkuu viongozi wote wa africa waungane na waweke misimamo sisi wananchi tukiona hivyo nasi tutaunga mkono tu wala hatuwezi kuwa na shida, ila kama viongozi wao wenyewe tu wanageukana na wengine ni mamluki sisi wananchi wa kawaida hatuwezi kuwa na nguvu yoyote ya kupitisha hilo hata hizo nchi za magharibi kuungana ni kwa sababu viongozi waliamua hilo, maana wananchi walianza kupiga kelele muda mrefu ila viongozi walipoamua tu kwamba kweli sasa ni muda wa kumkataa mfaransa ndio habari ikaishia hapo
Hili sio swala la viongozi ni swala la sisi wenyewe wananchi, kiongozi mwenyewe anatoka kwa wananchi... Kiongozi atakuwa na nguvu endapo tu wananchi wasipokuwa na kauli mmoja... Hakuna nchi ambayo kiongozi wake anaweza kuwapelekesha wananchi endapo wakiwa na sauti moja... Utofauti wetu ndio unapekelekea inakuwa rahisi kupelekeshwa, kwa sababu wengine wanakuwa wana support ndio na wengine wanasapoti hapana sasa hapo ndipo Kiongozi wananchi anatumia mwanya kuwaangamiza wale wasioendana naye, ila kama wote mna kauli mmoja, kiongozi anakuwa mchache sana
 
Hivi karibuni kumekuwa na uhaba wa sarafu ya Dollar Duniani, kitu ambacho kimepeleka pia sarafu za nchi nyingi barani Afrika kuyumba, na vitu kupanda bei bila mpangilio.

Kwa sababu mimi pia ni Admin wa page moja ya facebook inayoitwa Icon Africa ambapo humo tupo ma-Admin wengi kutoka nchi za Afrika na kila mmoja anapost mambo ya nchi yake ususani utalii. Basi nikaamua kwenda kwenye page kuuliza ni namna gani tuwaweza kuwa na pesa yetu ya bara la Afrika ili kuepuka madhara ya Dollar.

Na kama mnavyojua nchi zetu nyingi za kiafrika bado zinatumia sarafu ya Dollar kufanya manunuzi sehemu mbali ndani na nje ya bara la Afrika. Hivyo ukosefu wa sarafu ya Dollar imepelekea pia nchi nyingi kutikisika kiuchumi. lakini endapo tungekuwa na sarafu yetu ya bara la Afrika kama jinsi ilivyo sarafu ya Ulaya (Euro [emoji387] €), basi tutakuwa imara kiuchumi, hata kama dollar ikitikisika, sisi bado tutakuwa salama. Na pia tutaweza kufanya manunuzi ndani ya bara letu bila kutatizwa na kupanda na kushuka kwa sarafu ya Dollar.

Nimeanza kuona muitikio mkubwa wa watu mbalimbali kwenye comment za hiyo post wakipendekeza Sarafu iitwe Afro au Afric. Na muitikio ni mkubwa na kila mwafrika anatamani tuwe na sarafu yetu. Haya maoni ni namna gani yanawezwa kufikishwa Africa Union na yakafanyiwa kazi kwa haraka. Maana sidhani kama kuna nchi ya kiafrika inataka kuendelea kuikumbatia dollar
This thing will not work.
 
Siyo wazo jipya hilo.

"Kwani Ghaddafi alipoleta wazo hilo alisema iitwe vipi?

Unafikiri kilichomuuwa Ghaddafi ni nini?
 
US Dollar ni sarafu bora kuwa nayo kwa sasa hivi na kushindana nayo inabidi uwe na uchumi imara.
Africa tungeanza na kuwa na uchumi imara kwanza.
Kuwa na sarafu yetu moja haimaanishi tunataka kupigana na Dollar... Kuwa na sarafu yetu inamaanisha kufanya biashara sisi kwa sisi... Chukua mfano wewe unavyochukua pesa yako ya Shillings unaenda kununua Sukari bila kutumia Dollar hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa sarafu ya Afrika unapoenda kufanya biashara na Msudani au Muafrika kusini
 
Back
Top Bottom