Mabadiliko uanza na mimi... Kama kila mwafrika mmoja akiweka nia ya kuwa na sarafu mmoja, hili jambo linawezekana... Muammar Gaddafi aliibuka wakati mbaya, Siasa za kibeberu usijitoe wewe kama wewe kupingana nao, wewe sema wananchi ndio wamesema... Huoni Burkina Faso na Mali walivyomuweza Mfaransa, sio mtu mmoja ambaye alitoka kupigania nchi, bali raia wote... Lakini kule Libya kilichomua Gaddafi ni baadhi ya wananchi wake kuanza kumuita Dictator, wananchi wengine hawakumuunga mkono, na Marekani akishaona tu wengine hawakuungi mkono, ndio anawatimua hao hao kukuangamiza... Sasa sisi kama Afrika na mwafrika mmoja mmoja sote kwa pamoja tukisimama hawawezi kufanya kitu... Niger, Mali na Burkina Faso wananchi wote hawakutengana, waliungana na kua taifa kama taifa