Arnold Kalikawe
Senior Member
- Sep 28, 2016
- 152
- 374
- Thread starter
- #101
Sasa utafanya uwekezaji gani kwenye nchi za Afrika mashariki kama hauna Dollar? Wakenya wenyewe wanatushinda uchumi kwa sababu wanaingiza Dollar nyingi kutushinda... Na usichanganye mambo kwamba eti kisa Uganda na Kenya na Tanzania tunatumia Shillings basi ndio tunatumia sarafu mmoja.... Ugandan shillings, Kenyan shillings na Tanzanian Shillings ni sarafu tatu tofauti kabisa japo zinafanana neno shillings.Mfano mdogo.
1. Sisi hapa East Africa tunafanya biashara baina yetu zenye masilahi ya kuinua uchumi?
2. Tanzania tunaweza kufanya uwekezaji kwenye nchi za Afrika na uwekezaji gani?
Utawekeza nchi gani Afrika bila kuwa na Dollars? Nani atakayeyakubali mashilingi yako yasiyoweza kuuzwa popote duniani... Dollar inauzika popote duniani ndio maana lazima uwe na Dollar... Sasa tukiwa na sarafu ya Afrika lazima itakuwa juu kwa sababu nchi yoyote ya nje ya Afrika ikitaka kufanya biashara na nchi yoyote ya Afrika basi ni lazima inunue kwanza sarafu ya Afrika ili iwe rahisi kufanya manunuzi barani Afrika