Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

Akili yako ina minyororo mingi sana.

Ndio maana nimekuita dogo unafikiri minyororo ni kufungwa miguuni na mikononi.
Dogo umekaririshwa na wanafalsafa wa mitaani... Uhuru unaanza na fikra, mimi tayari niko huru na siamini kwenye kutumia Dollar miongoni mwa nchi zetu za Afrika... Wewe uliyefungwa minyororo ya fikra baki kwenye kuitukuza dollar...

Keep exposing your stupidity
 
Dogo umekaririshwa na wanafalsafa wa mitaani... Uhuru unaanza na fikra, mimi tayari niko huru na siamini kwenye kutumia Dollar miongoni mwa nchi zetu za Afrika... Wewe uliyefungwa minyororo ya fikra baki kwenye kuitukuza dollar...

Keep exposing your stupidity
Imenibidi nicheke😆 dogo unasema upo huru 😆 daaah!

Dogo wewe UVCCM nini ? maana hamna akili nyie.
 
Kuwa na sarafu yetu moja haimaanishi tunataka kupigana na Dollar... Kuwa na sarafu yetu inamaanisha kufanya biashara sisi kwa sisi... Chukua mfano wewe unavyochukua pesa yako ya Shillings unaenda kununua Sukari bila kutumia Dollar hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa sarafu ya Afrika unapoenda kufanya biashara na Msudani au Muafrika kusini
Thamani ya hela yako kwa msudani (exchange rate) itakuwa based on what ili tuwe na sarafu moja?
 
Hivi karibuni kumekuwa na uhaba wa sarafu ya Dollar Duniani, kitu ambacho kimepeleka pia sarafu za nchi nyingi barani Afrika kuyumba, na vitu kupanda bei bila mpangilio.

Kwa sababu mimi pia ni Admin wa page moja ya facebook inayoitwa Icon Africa ambapo humo tupo ma-Admin wengi kutoka nchi za Afrika na kila mmoja anapost mambo ya nchi yake ususani utalii. Basi nikaamua kwenda kwenye page kuuliza ni namna gani tuwaweza kuwa na pesa yetu ya bara la Afrika ili kuepuka madhara ya Dollar.

Na kama mnavyojua nchi zetu nyingi za kiafrika bado zinatumia sarafu ya Dollar kufanya manunuzi sehemu mbali ndani na nje ya bara la Afrika. Hivyo ukosefu wa sarafu ya Dollar imepelekea pia nchi nyingi kutikisika kiuchumi. lakini endapo tungekuwa na sarafu yetu ya bara la Afrika kama jinsi ilivyo sarafu ya Ulaya (Euro [emoji387] €), basi tutakuwa imara kiuchumi, hata kama dollar ikitikisika, sisi bado tutakuwa salama. Na pia tutaweza kufanya manunuzi ndani ya bara letu bila kutatizwa na kupanda na kushuka kwa sarafu ya Dollar.

Nimeanza kuona muitikio mkubwa wa watu mbalimbali kwenye comment za hiyo post wakipendekeza Sarafu iitwe Afro au Afric. Na muitikio ni mkubwa na kila mwafrika anatamani tuwe na sarafu yetu. Haya maoni ni namna gani yanawezwa kufikishwa Africa Union na yakafanyiwa kazi kwa haraka. Maana sidhani kama kuna nchi ya kiafrika inataka kuendelea kuikumbatia dollar
Zingatia ;
Kitu Cha muhimu ni uimara (stability) wa hiyo sarafu, utahitaji bidhaa nyingi na zenye ubora kuweza kuistabilize hiyo sarafu...usisahau political positions na stability za wahusika....

Ushauri Wangu hili jambo ni zuri Ila liwe la kiuchumi zaidi ya kuwa la kisiasa
 
Swali fikirishi je ni kwa kiasi gani nchi za kiafrika zinafanya biashara baina yao?
Watu wanafikiri ni kwasababu ya dollar kumbe kwasababu ya umasikini wa nchi.
Utatengeneza sarafu halafu kinachofuata? Nchi za afrika ni masikini, uzalishaji mdogo, teknolojia ndogo, sera mbaya ya uchumi na uongozi mbaya. Nchi za afrika zenyewe hazifanyi biashara baina yaom
Utakuwa na sarafu lakin bado upo pale pale kwenye umasikini.
Mtu aliyeoko Congo brazaville kukutumia 2000 ya kibongo haiwezekani ila mtu aliyeoko DRC, Kenya, burundi, rwanda na malawi unaweza kumtumia hela. Je, tunafanya biashara baina yetu?
 
Hata mwanzoni gaddafi alikuwa kama hao wanaobeba sifa za kiwaki ss hv, muda ukifika watawakana tu hao magenerali wao.
Gadaffi hakusapotiwa na baadhi ya wananchi wake... Alafu hii sarafu moja ya Afrika sio ishu ya kisiasa bali kiuchumi... Gadaffi alitoa kauli kama mtu binafsi, lakini agenda ya sarafu tunaitoa kama waafrika wote na si kutegemea rais ndio atoe... Wazungu hawawezi kuua waafrika wote eti kisa wamedai sarafu mmoja, lakini watamuua mtu mmoja endapo yeye peke yake ndio atasimama peke yake kudai...
 
Kuwa na sarafu yetu moja haimaanishi tunataka kupigana na Dollar... Kuwa na sarafu yetu inamaanisha kufanya biashara sisi kwa sisi... Chukua mfano wewe unavyochukua pesa yako ya Shillings unaenda kununua Sukari bila kutumia Dollar hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa sarafu ya Afrika unapoenda kufanya biashara na Msudani au Muafrika kusini
Mfano mdogo.
1. Sisi hapa East Africa tunafanya biashara baina yetu zenye masilahi ya kuinua uchumi?
2. Tanzania tunaweza kufanya uwekezaji kwenye nchi za Afrika na uwekezaji gani?
 
Comment za Facebook[emoji1782][emoji38] kweli wewe bado dogo kabisa.

Afrika imejaa wapumbavu wengi sana wasiojua lolote mradi siku imeenda usifurahie kuungwa mkono na wajinga wenzako
Nimeshakwambia kula nyama nyamaza... Hao unaowaita wapumbavu wengine wanakuzidi Elimu na Exposure, wakati wewe ukisafiri sana ni umeenda Tandahimba, Passport huna, unabaki kuwa Keyboard warrior wa jamii forum... sasa facebook na jamii forum zina utofauti gani, tena at least Facebook kuna Raia wa nchi kibao wanaleta Exposure kwenye comment section wakati wewe umekalia U-CCM na U-Chadema humu

Uwezi kujua umuhimu wa Sarafu mmoja kama ufanyi biashara za kimataifa au utembei nchi za kiafrika... Tafuta Passport dogo utembee na upunguze kelele
 
Imenibidi nicheke[emoji38] dogo unasema upo huru [emoji38] daaah!

Dogo wewe UVCCM nini ? maana hamna akili nyie.
Mi niko huru Dogo, wewe endelea kubaki kwenye hiyo minyororo ya wazungu na vyama vya siasa ndio Topic zenu... Kujua kuliongelea CCM ndio unadhani ni exposure [emoji23]. Dogo bado unasafiri ndefu sana ya kujua uhuru ni nini, baki kwenye minyororo ya fikra
 
Thamani ya hela yako kwa msudani (exchange rate) itakuwa based on what ili tuwe na sarafu moja?
Kwani thamani ya Euro kati ya Waespania na Wajerumani inakuwaga based on what?

Kwani wewe na Mangi hapo dukani ukienda kununua Sukari si mnatumia sarafu mmoja ya shilingi, je thamani ya hela baina yenu wawili (Exchange rate) inakuwa based on what?

Tangu lini sarafu mmoja ikawa na Exchange rate tena? Hapo hakuna Exchange rate, ukienda Sudan unaenda na pesa hiyo hiyo uliyotoka nayo Tanzania bila kubadilishwa kwenda kwenye Dollar... Utofauti labda iwe bei ya bidhaa tu kama sukari Tanzania inauzwa Afro 800 kwa kilo lakini ukienda sudani labda itakuwa inauzwa Afro 1000 kutokana na uchumi wa nchi usika, kama jinsi unavyonunua kuku dar es salaam anauza elfu 30,000 lakini kwa hiyo hiyo hela ukienda Kigoma anauzwa 15,000 na wote mnauza kwa shilling...
 
Mnajidanganya bure.
Hivi nyie mnaijua Afrika na asili yake au mmevimbiwa?
Afrika ni mtumwa wa kila mtu mweupe.
Issue ni kumkataa huyo mtumwa then tuanze upya.
Mkoloni gani atakubali tuwe na sarafu yetu?.
Kwa akili hizi za Kiafrika za Royal Tour?
 
Wapo baadhi ya viongozi wameweza kufanya vyema... Pia Usitumie reference ya viongozi wachache kujumuisha viongozi wote, uongozi unaanza na mimi na wewe... Sasa kama tu wewe mwenyewe unaamini kwenye kushindwa inamaanisha pia hiyo spirit ya kushindwa utaenda kuwaaminisha na wengine hatuwezi mwisho wa siku wote tunakuwa na fikra ya kushindwa... Wewe ukiamini kwenye kuweza hata watoto wako na watu wako utawaamnisha Tunaweza na mwisho wa siku tunafanya mageuzi... Sasa kama tu wewe unaamini kwenye kushindwa si tukikupa uongozi utakuwa kama hao hao walioshindwa... Ukitizama vizuri hata hayo mawazo kwamba waafrika hatuwezi ni kuwa umerithishwa na mwingine.. tukiendelea kurithishana mwishowe kushindwa kunatimia kwa sababu kila mtu anaamini kushindwa
Kwani hii ndiyo mara ya kwanza kuongelewa? Kwenye ukanda tu hakuna hivi kungekuwa na matumaini East Africa tungekuwa tayari, sahizi watu wanapinduana .

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Zingatia ;
Kitu Cha muhimu ni uimara (stability) wa hiyo sarafu, utahitaji bidhaa nyingi na zenye ubora kuweza kuistabilize hiyo sarafu...usisahau political positions na stability za wahusika....

Ushauri Wangu hili jambo ni zuri Ila liwe la kiuchumi zaidi ya kuwa la kisiasa
Yeah sura kabisa... Kiuhalisia Afrika ni nchi tajiri sana, hivyo hata tukiwa na sarafu yetu, kutokana na rasilimali tulizonazo basi sarafu lazima iwe na nguvu Duniani... Kwa sababu hili mataifa mengine hafanye biashara na nchi yoyote ya bara la Afrika yatalazimika kuwa au kununua sarafu ya bara la Afrika, ili iwe rahisi kufanya miamala... Stability itakuja tu maana resources nyingi za duniani zinatoka Africa, watanunua kwa pesa yetu... Lakini tukibaki kila mmoja kivyake basi itatubidi tuendelee kutumia Dollar na kuendelea kuifanya iwe na nguvu zaidi
 
Bomba la mafuta kutoka Tanga kwenda Uganda linapigiwa kelele et litaharibu mazingira, ukiachilia mbali wao mabomba ya mafuta kutoka RUssia na kwingineko.

Hoja yangu : hao jamaa ni bora dunia isambaratike ila sio kuona Africa inakua huru kiuchumi na kisiasa.
 
Watu wanafikiri ni kwasababu ya dollar kumbe kwasababu ya umasikini wa nchi.
Utatengeneza sarafu halafu kinachofuata? Nchi za afrika ni masikini, uzalishaji mdogo, teknolojia ndogo, sera mbaya ya uchumi na uongozi mbaya. Nchi za afrika zenyewe hazifanyi biashara baina yaom
Utakuwa na sarafu lakin bado upo pale pale kwenye umasikini.
Mtu aliyeoko Congo brazaville kukutumia 2000 ya kibongo haiwezekani ila mtu aliyeoko DRC, Kenya, burundi, rwanda na malawi unaweza kumtumia hela. Je, tunafanya biashara baina yetu?
Unajua kwa nini nchi za Afrika hatufanyi biashara baina yetu, kikwazo kikuu hapo ni Dollar... Sukari utakayoenda kumuuzia Mzambia atakupa dollar chache kwa sababu yenye mwenyewe hana Dollar za kutosha, lakini hiyo hiyo sukari ukienda kuiuza Marekani utapewa Dollar nyingi... Sasa mtu hapo si lazima akatae kufanya biashara na Muafrika mwenzake kwa sababu hana Dollar, mwisho wa siku ataenda kumuuzia mzungu hili apate Dollar nyingi... Ndio maana nikasema hili biashara tuweze kufanya baina yetu nchi za Afrika inatakiwa tuwe na sarafu mmoja ili kusiwe na kizingiti cha Sarafu ya Dollar.. kwa sababu sasa hivi hili wewe uende kula Bata south Africa inapaswa uwe na Dollar, tayari hapo ni kikwazo. Na Dollar ukiyumba basi ndio hivyo tena
 
Hazifanyi baina yao ambapo pia moja wapo ya sababu ni uaba wa Dollar... Kenya ikiuza TV haitataka kuiuzia Tanzania kwa sababu Shilling yetu haina nguvu, watataka kutuuzia kwenye Dollar, na kwenye Dollar napo Tanzania ina uaba hivyo Kenya atalazimika kupeleka bidhaa zake kwenye nchi zenye Dollar nyingi ili alete Dollar Nchini kwake... Sasa wewe unauza kitu hili upate Dollar, alafu ukamuuzie tena mwenzako ambae naye hana Dollar kama wewe? Ndio maana nchi nyingi za Afrika zinafanya biashara na nchi za nje ya bara la Afrika sababu kuu ni kwenda kuitafuta Dollar... Sasa tukiwa na sarafu yetu basi biashara zetu hazitahitaji tena kutumia Dollar bali sarafu yetu wenyewe tunakuwa tunafanya nayo biashara
Ushawahi kununua bidhaa kenya, wakakataa wanataka dollar?
Wakenya wengi wapo pale Mang'ola wananunua vitunguu kwa pesa za kibongo.
Shida kubwa siyo Sarafu, shida
1. Afrika hatuna bidhaa za kuuziana kwasababu ya uzalishaji. Hii tv unayosema zinatoka China, Marekani na mataifa yaliyoendelea
2. Hatuna mifumo ya kutuma pesa na kupokea. Ni rahisi sana mtu aliyeoko Marekani kukutumia hela na ikaingia kwenye simu ila ni ngumu sana mtu aliyeoko Ghana akutumie hela iingie kwenye simu.
3. Teknolojia yetu ni ndogo sana. Mpk sasa tunalima kwa jembe la mkono, tunahangaika na matundu ya choo, umeme na maji bado ni changamoto. Chakula tunacholima Tanzania hakitutoshi tutaweza kuzalisha ili kuwauzia wengine?
4. Nchi za Afrika zimebinafsisha kwa kila rasilimali tena miaka na miaka. Utamuuzia nini mwenzako?
5. Umasikini wa nchi. Nchi yenyewe inanuka shida, viongozi wanafanya ufisadi na rushwa. Mnafanyaje biashara?
Tutaweza kutengeneza sarafu lkn je, itakuwa mkombozi wa kiuchumi?
 
Back
Top Bottom