Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

US Dollar ni sarafu bora kuwa nayo kwa sasa hivi na kushindana nayo inabidi uwe na uchumi imara.
Africa tungeanza na kuwa na uchumi imara kwanza.
 
Mnaota!!mambo madogo madogo tu yamewashinda sembuse hilo?!!
 
Kuanzisha Sarafu yetu ni kwa ajili ya Biashara zetu za Ndani ya Afrika... Suala la Deni la Taifa hiyo ni kesi ya nchi binafsi, tunachotaka ni kuwa Tanzania ikifanya biashara na South Africa basi tutumie fedha yetu na si kutumia Dollar ambayo ikiyumba na Sisi tunayumba... Sarafu yetu itakuwa kwa ajili ya matumizi ya bara la Afrika kama ilivyo Euro kwa bara la Ulaya
 
Ule mpango wa Putin uliishia wapi?
 
Hata Uingereza inatumia Euro?
Uingereza inatumia Pound... Lakini usitake kuleta mambo ya uingereza hapa... Hapa sisi tunazungumzia Uchumi wa Afrika na biashara za ndani ya bara la Afrika bila kutumia Dollar ambayo ikiyumba vitu vinapanda bei
 
Kweli kabisa... Yani inashangaza hata humu jamii forum kuna watu wanakuja na kusema eti ni jambo lisilowezekana... Akili zetu wa Afrika ni za kufikiri kushindwa tu ndio maana Bara linabaki nyuma kila siku
 
Swali fikirishi je ni kwa kiasi gani nchi za kiafrika zinafanya biashara baina yao?
Hazifanyi baina yao ambapo pia moja wapo ya sababu ni uaba wa Dollar... Kenya ikiuza TV haitataka kuiuzia Tanzania kwa sababu Shilling yetu haina nguvu, watataka kutuuzia kwenye Dollar, na kwenye Dollar napo Tanzania ina uaba hivyo Kenya atalazimika kupeleka bidhaa zake kwenye nchi zenye Dollar nyingi ili alete Dollar Nchini kwake... Sasa wewe unauza kitu hili upate Dollar, alafu ukamuuzie tena mwenzako ambae naye hana Dollar kama wewe? Ndio maana nchi nyingi za Afrika zinafanya biashara na nchi za nje ya bara la Afrika sababu kuu ni kwenda kuitafuta Dollar... Sasa tukiwa na sarafu yetu basi biashara zetu hazitahitaji tena kutumia Dollar bali sarafu yetu wenyewe tunakuwa tunafanya nayo biashara
 
Mpango wa kuipatia dola jina lingine ila thamani yake itabakia pale pale....jamani Waafrika tufanye kazi.
Lengo kuu la Sarafu ya Afrika ni kwa ajili ya kufanya biashara ndani ya bara la Afrika. Hivi leo ili ununue Nigeria kiatu inatakiwa uwe na Dollar, hivyo mnaijeria huyo kuliko kukuuzia kwa Dollar hiyo anaona bora akamuuzie mmarekani mwenyewe hili apate Dollar original kuliko kuunga unga biashara na wewe mtanzania mwenye Dollar ya kubangaiza... Sasa lengo la sarafu ya Afrika ni kuvunja huu mlango wa Dollar... Hata kama thamani ya Dollar itabaki pale pale hiyo sisi haituhusu, kinachotuhusu ni kuweza kufanya biashara zetu ndani ya Afrika bila kushawishiwa na Dollar
 
Kweli aisee! Hili lipo tricky sana
Mbona Euro wameweza na wanauziana na kufanya biashara kwa pesa yao... Hakuna cha tricky hapo, au unamuogopa mmarekani kiasi hicho... Dollar yake ibaki pale pale, ila huku kwetu ndani ya Afrika tufanye biashara kwa pesa yetu
 
Kweli kabisa... Yani inashangaza hata humu jamii forum kuna watu wanakuja na kusema eti ni jambo lisilowezekana... Akili zetu wa Afrika ni za kufikiri kushindwa tu ndio maana Bara linabaki nyuma kila siku
Confidence hakuna kwa mswahili yaani kila kitu anaona hawezi
Mbona kuiba wwnaweza? Kwanini wasiibe maarifa?
Kweli continent lote linategemea misaada tu kila kukicha
 
Hili sio swala la viongozi ni swala la sisi wenyewe wananchi, kiongozi mwenyewe anatoka kwa wananchi... Kiongozi atakuwa na nguvu endapo tu wananchi wasipokuwa na kauli mmoja... Hakuna nchi ambayo kiongozi wake anaweza kuwapelekesha wananchi endapo wakiwa na sauti moja... Utofauti wetu ndio unapekelekea inakuwa rahisi kupelekeshwa, kwa sababu wengine wanakuwa wana support ndio na wengine wanasapoti hapana sasa hapo ndipo Kiongozi wananchi anatumia mwanya kuwaangamiza wale wasioendana naye, ila kama wote mna kauli mmoja, kiongozi anakuwa mchache sana
 
This thing will not work.
 
Siyo wazo jipya hilo.

"Kwani Ghaddafi alipoleta wazo hilo alisema iitwe vipi?

Unafikiri kilichomuuwa Ghaddafi ni nini?
 
US Dollar ni sarafu bora kuwa nayo kwa sasa hivi na kushindana nayo inabidi uwe na uchumi imara.
Africa tungeanza na kuwa na uchumi imara kwanza.
Kuwa na sarafu yetu moja haimaanishi tunataka kupigana na Dollar... Kuwa na sarafu yetu inamaanisha kufanya biashara sisi kwa sisi... Chukua mfano wewe unavyochukua pesa yako ya Shillings unaenda kununua Sukari bila kutumia Dollar hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa sarafu ya Afrika unapoenda kufanya biashara na Msudani au Muafrika kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…