Deinstein 01
JF-Expert Member
- May 12, 2024
- 2,090
- 3,928
Habari wakuu!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, Ulaya ya karne ya 19 kurudi nyuma sio kama Ulaya ya karne hii ya 21 yaani ni kama vile wameridhika na maendeleo yao.
Hata katika upande wa sayansi na teknolojia bara hilo lipo nyuma katika gunduzi za sayansi na teknolojia. Ukizingatia ya kuwa Ulaya imetoa magenius wengi wenye mchango mkubwa katika sayansi. Mfano Newton, Mendeleev, Carl Benz, Galileo, Gregory Mendel na wengine wengi.
Lakini leo Ulaya imeachwa nyuma katika suala zima la sayansi na teknolojia. Imagine nchi kama Uingereza ndo ilikuwa ya kwanza kufanya mapinduzi ya viwanda lakini leo China ina viwanda vingi kuliko Uingereza. Nchi kama Ujerumani ndo ilikuwa ya kwanza kutengeneza magari ila leo wanapitwa na nchi kama ya Brazil katika kutengeneza EV.
Leo bara la Ulaya linasikika tu kwenye maswala ya mpira, movie na labda uchaguzi na maswala mengine ya kisiasa. Ila kwenye maendeleo Ulaya ipo nyuma. Juzi BBC walitoa ripoti ya kuwa uchumi wa Uingereza umeshuka kwa 0.1% mpaka kufikia mwaka 2025.
Shida ni nini katika bara la Ulaya? Ama ndo kutangulia sio kufika.
Yangu ni hayo tu. Karibuni kwa maoni.