Bara la ulaya ni kama vile linasinzia kama sio kulala

Deinstein 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
2,090
Reaction score
3,928
Habari wakuu!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, Ulaya ya karne ya 19 kurudi nyuma sio kama Ulaya ya karne hii ya 21 yaani ni kama vile wameridhika na maendeleo yao.

Hata katika upande wa sayansi na teknolojia bara hilo lipo nyuma katika gunduzi za sayansi na teknolojia. Ukizingatia ya kuwa Ulaya imetoa magenius wengi wenye mchango mkubwa katika sayansi. Mfano Newton, Mendeleev, Carl Benz, Galileo, Gregory Mendel na wengine wengi.

Lakini leo Ulaya imeachwa nyuma katika suala zima la sayansi na teknolojia. Imagine nchi kama Uingereza ndo ilikuwa ya kwanza kufanya mapinduzi ya viwanda lakini leo China ina viwanda vingi kuliko Uingereza. Nchi kama Ujerumani ndo ilikuwa ya kwanza kutengeneza magari ila leo wanapitwa na nchi kama ya Brazil katika kutengeneza EV.

Leo bara la Ulaya linasikika tu kwenye maswala ya mpira, movie na labda uchaguzi na maswala mengine ya kisiasa. Ila kwenye maendeleo Ulaya ipo nyuma. Juzi BBC walitoa ripoti ya kuwa uchumi wa Uingereza umeshuka kwa 0.1% mpaka kufikia mwaka 2025.

Shida ni nini katika bara la Ulaya? Ama ndo kutangulia sio kufika.

Yangu ni hayo tu. Karibuni kwa maoni.
 
Maendeleo zaidi yanahitaji pia Ardhi....Ulaya eneo la Ardhi n dogo ni kama lishaisha.
Lazima tu wasimame kwenye issue izo za kimaendeleo esp viwanda.
 
Wazungu washamaliza maendeleo yao sasa hivi wanaishi tu hawana wanachotafuta
Hizo takataka wamewaachia wamarekani na wa asia
Kwanza wahasibu karibia wote nchini uingereza ni wahindi
Wazungu pure hawataki stress hata kuzaliana hawataki
Juzi niliangalia takwimu za kuzaliana bara la ulaya lilikuwa na -0.2 yani sasa hivi wanaokufa ni wengi kuliko wanaozaliwa
Ni suala la muda tu hii race itafutika
 
Habari yako imekosa data.

Takwimu pekee uliyoweka ni ya uchumi wa Uingereza kushuka kwa 0.1% ambayo haituambii kitu zaidi ya kutuambia uchumi wa Uingereza kushuka kwa 0.1. Na hata hapo hujatuambia unaongelea GDP au nini? Unaongelea GDP au economic growth?

Hata kwenye takwimu uliyotupa, maneno yako yako vague hueleweki.

Uchumi wa Mo Dewji mwenye net dola bilioni moja ukishuka kwa 0.1%, na wewe mwenye uchumi wa $ 1,000 uchumi wako ukipanda kwa 100% utasema kuwa Mo Dewji kaanguka kiuchumi na wewe umefanya vizuri kuliko yeye?

Weka data za unachotaka kupima, za dunia nzima, kwa nuktadha.

Mara nyingine masikini anaweza kuoandisha uchuni wake kwa kasi sana zaidi ya tajiri, kwa sababu tajiri kashamaliza stage ya kujua jwa kasi ana uchumi wa juu sana ambao hauwezi tena kujua kwa kasi.

Sasa hapo utasema masikini kamshinda tajiri kwa sababu uchumi wake wa kimasikini unakua kwa kasi sana?

Pia, soma kitabu cha Fareed Zakaria kinaitwa "The Post Amwrican World". Kinaelezea kwa upande wa Marekani ni jinsi gani the rest if tge wirld is catchibg up with America. Kwamba hata kama dunia ikiyoendelea hairudi nyuma, ukweli kwamba nchi kama za BRICS (Brazil, Russia, India, China na South Africa) zinapiga hatua kubwa, unafanya ionekane kuwa Marekani haiendelei.

The same thing could be happenning in Europe.

Europe yenyewe ipo very divwrae, so kuongelea Eurooe kama kitu kimoja ni misleading.

Weka data za research and innovation za dunia nzima hapa tuangakie Europe ilikuwa wapi na ipo wapi leo.
 
Mimi pia nafikiri hii ni moja ya sababu. Wazungu wanapenda sana kurelax ukienda nchi kama Switzerland wengi wao wanakula bata tu hawafanyi kazi yaani kule kama hauna ajira serikali inakulipa. Wachina wao wanapiga kazi ni nadra sana kumuona mchina kwenye mbuga za wanyama ila angalia wazungu visit mbuga zetu ni wengi kuliko hata wazawa.
 
Nakubali sikuhizi kwenye maendeleo bara la asia wanakimbiza uenda wakapngoza uchumi wa dunia
 
Mkuu kuna vitu vingine havihitaji data ni suala la common sense tu leo hii India anakaribia kuipita Uingereza kiuchumi. Hata kwenye vyombo vya habari Ulaya imepoa inasikika kwenye mambo ya UEFA na EPL na ligi zingine ila kwenye mambo serious wapo off.
 
Kila kitu kinahitaji data.

Hata hilo la India inakaribia kuipita Uingerwza kiuchumi liweke hapa kwa data.

Kusema "India inakaribia kuipita Uingerwza kiuchumi" is so vague, mtu anayejua uchumi hatakiwi kusema hivyo.

Tuangalie unaposema India inakaribia kuipita Uingereza kiuchumi una maana gani?

Unachopima na kulinganisha hapo ni kitu gani?

Weka GDP per capita ya India na Uingereza tuangalie hapa.
 
Maendeleo zaidi yanahitaji pia Ardhi....Ulaya eneo la Ardhi n dogo ni kama lishaisha.
Lazima tu wasimame kwenye issue izo za kimaendeleo esp viwanda.

Ulaya ina tatizo hili la Ukosefu wa Ardhi ya kutosha. Tatizo hili kwa upande mwingine pia limesababisha suala zima la kukwana kwa Kuongezeka kwa idadi ya Watu kwenye nchi hizo.
Ongezeko la idadi ya Watu ni ndogo Sana, nchi nyingi sana za Ulaya zina Aging Population.

Ujerumani ndio nchi yenye Uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, hii ni kutokana na Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin Kitendo ambacho kilisababisha nchi Mbili za Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mashariki kuungana tena pamoja na kuzaliwa kwa nchi moja ya Ujerumani, ambayo ina Ardhi kubwa ya kutosha na yenye idadi kubwa ya Watu
 
Kila kitu kinahitaji data.

Hata hilo la India inakaribia kuipita Uingerwza kiuchumi liweke hapa kwa data.

Tuangalie unaposema India inakaribia kuipita Uingerwza kiuchumi una maana gani?

Weka GDP per capita ya India na Uingereza tuangalie hapa.
As of 2024, the Gross Domestic Product (GDP) of India and the United Kingdom (UK) are as follows:

India:

Nominal GDP: Approximately $3.89 trillion in 2024.

Real GDP Growth: Projected growth between 6.5% and 6.8% for the fiscal year 2024-2025, driven by strong domestic demand and increased government spending.


United Kingdom:

Nominal GDP: Approximately £2.56 trillion in 2024.

Real GDP Growth: Estimated at 1.5% for 2024.


In January 2025, the UK economy experienced a slight contraction of 0.1%, attributed to declines in the manufacturing and construction sectors.

These figures indicate that while India's economy continues to grow at a robust pace, the UK is facing challenges in maintaining consistent economic growth.

Data hizo hapo
 
Unalinganishaje GDP ya nchi yenye watu 1.44 billion (India) na GDP ya nchi yenye watu milioni 68 (India) ?

Unajua tofauti ya GDP na GDP per capita?

Unajua kwa nini nimeuliza GDP per capita na si GDP?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…