Barabara nne Dar kufungwa kuimarisha Usalama mkutano wa SADC na EAC kujadili mzozo wa DRC na M23

Barabara nne Dar kufungwa kuimarisha Usalama mkutano wa SADC na EAC kujadili mzozo wa DRC na M23

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Mkutano huo utakuwa chini ya uenyeji wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia ugeni huo hali ya usalama imeimarishwa maradufu Februari 07, hadi 08, 2025 ambapo Jeshi la Polisi limetangaza baadhi ya barabara zitakuwa zinafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kupisha misafara ya viongozi wa Mkutano huo.

Barabara ambazo zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kadri itakavyoruhusu
ni ;

1. Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji.
2. Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.
3. Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena.
4. Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun.

photo-output.jpeg
photo-output.jpeg

Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limetangaza kuzifunga kwa muda barabara nne zinzoingia katikati ya jiji, ili kutoa nafasi kwa ugeni wa wakuu wa nchi wnaotarajiwa kukutana kesho, jumamosi Februari 8,2025

Barabara zitakazofungwa ni nyerere kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyere kwenda katikati ya Jiji.

Barabara nyingine ni ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi ikulu.

Pia, barabara ya ohio kutokea kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun.

Aidha Bodaboda na bajaji zimezuiliwa kuingia kwenye maeneo katikati ya jiji hasa barabara zilizotajwa kwa muda kwa sababu za kiusalama wakati wa ugeni.

Soma, Pia: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo
 
Mikutano mingine wangeileta huku Sukamahela wafunge barabara tusiende kazini
 
Mikoani wanaleta lini mikutano hii mikubwa? Hii mikutano inapanua sana fursa
 
Back
Top Bottom