Barabara nne Dar kufungwa kuimarisha Usalama mkutano wa SADC na EAC kujadili mzozo wa DRC na M23

Barabara nne Dar kufungwa kuimarisha Usalama mkutano wa SADC na EAC kujadili mzozo wa DRC na M23

Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Mkutano huo utakuwa chini ya uenyeji wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia ugeni huo hali ya usalama imeimarishwa maradufu Februari 07, hadi 08, 2025 ambapo Jeshi la Polisi limetangaza baadhi ya barabara zitakuwa zinafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kupisha misafara ya viongozi wa Mkutano huo.

Barabara ambazo zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kadri itakavyoruhusu
ni ;

1. Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji.
2. Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.
3. Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena.
4. Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun.View attachment 3227940View attachment 3227942
View attachment 3227937
Tena!
 
I wish all universities wahamishie vyuo Dodoma,singida na tabora mpaka shinyanga yaani dar Iko crowded mno , pia baadhi ya viwanda viletwe hata singida na Dodoma Kuna mapori mno Mana hapo ni rahisi mno kusafirisha kwenda pengine within a country
Idea yako ni nzuri kabisaaa,hujazongatia malighafi,masoko ...Dar ipo karibu na Bandari,Anga na Bahari yaani ni multipurpose tofauti na Singida
 
Kwa wanaojua ratiba ya kufika Kagame, tafadhali. Tunataka tumuandalie hafla ya kumzomea
Acha ujinga wako mumzomee kwa sababu gani? Hujui historia ya mgogoro Ndio maana unazungumza ujinga huu!
Leo hii Mkiamua kuwapa kipigo wamasai wa Tanzania unadhani wamasai wa Kenya wataacha kuja kuwasaidia ndugu zao? Ndio Kagame anachofanya DRC.
 
Back
Top Bottom