Kwa kweli hicho kipande huwa ni shida sana especially jioni, hata kama hakuna breakdown hali huwa ni tete. Yaani kuanzia mlandizi, misugusugu,Kongowe, kwa mfipa, kwa Mathius, picha ya ndege mpk Kibaha stand ya zamani ni msongamano tu wa magari unaweza kutembea hata masaa 2 usipocheza cheza rough. Cha kushangaza ukishafika kwenye njia sita pale Kibaha gari zinaanza kutembea, unakuta askari na mitochi yao hapo karibu na St. Joseph University, sasa kwa njia zile wanataka watu watembee kama wanasindikiza harusi tena, nchi ya ajabu sana hii.