Tunaomba Serikali itusaidie Barabara ya Madale Mwisho kwenda Mbopo kupitia Mikoroshini, Barabara ni mbovu sana na usafiri wa huko ni Bodaboda tu, wanapandisha bei mara iwe shilingi 2,000 mara shilingi 1,500.
Jamani, ki ukweli kabisa barabara za mbopo zina hali mbayaa... Zote mbili, ya kuanzia madale mwisho na ya kutokea mikoroshini. Bahati Mbaya m-bunge tumemtafuta lakini hakuna msaada tunaopata! Labda Jamiiforums mkitusaidia kupaza sauti tutasaidika! Magari yanaharibika, bajaji zimepandish bei.