Responded Barabara ya Mazimbo–Manyuki (Moro) yarekebishwa kwa Greda baada ya malalamiko

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Nimepita kwenye barabara ya Mazimbo–Manyuki, ambayo niliilalamikiwa hapa JamiiForums, na nikaona ni vyema nilete mrejesho kuwa kwa sasa imekwanguliwa kwa kutumia greda ili kupunguza mashimo yaliyokuwa yakisababisha usumbufu mkubwa, hasa kwa watumiaji wa vyombo vya moto.

Pia soma: Je, TARURA Morogoro wapo likizo au hakuna bajeti ya ujenzi wa barabara? Wakazi wa Manyuki tunapata shida

Kwa sasa, angalau inapitika kwa urahisi zaidi, tofauti na awali ambapo haikuwa rafiki kwa watumiaji. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba baadhi ya madereva wa daladala na bajaji walikuwa wakiona ugumu kuendesha shughuli zao kwenye njia hiyo.

Natoa rai yangu kwa mamlaka husika, hasa TARURA Morogoro, kuangalia uwezekano wa kufanyia maboresho ya muda mrefu njia hiyo hususani kuiwekea lami, ikizingatiwa umuhimu wa barabara hiyo katika shughuli za kila siku.
 
Kwa Sasa wako buzy na barabara ya tungi tubuyu kwakwel imeanza kupendeza
 
Back
Top Bottom