Barabara ya Mtaa – Nyamanoro (Mwanza) ni mateso kwetu au viongozi wanasubiri watumie kama ahadi wakati wa Kampeni?

Barabara ya Mtaa – Nyamanoro (Mwanza) ni mateso kwetu au viongozi wanasubiri watumie kama ahadi wakati wa Kampeni?

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
WhatsApp Image 2024-10-30 at 10.10.27_398c6c6b.jpg

WhatsApp Image 2024-10-30 at 10.10.44_e9c652aa.jpg
Mimi ni mmoja kati ya Wananchi wa Mtaa wa Green View uliopo Kata ya Nyamanoro, Manispaa ya Ilemela hapa Mwanza tuna malalamiko yetu kuhusu hali ya ubovu wa barabara zilizopo katika Kata yetu.

Barabara mbovu zimekuwa zikisababisha usumbufu kwa Watumiaji wa barabara hizo kwa muda mrefu sasa bila kufanyiwa matengenezo yoyote.

Tumekuwa tukipewa ahadi na Diwani wetu kuwa barabara hizo zitafanyiwa matengenezo lakini ahadi hizo zimekuwa azitekelezwi.

Sasa tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa Mwakani, sijui ndio atakuja kuanza kuerekebisha au ubovu huu utatumika katika kampeni za chaguzi hizo zinazokuja?
WhatsApp Image 2024-10-30 at 10.10.43_ae72fcee.jpg

WhatsApp Image 2024-10-30 at 10.10.48_4b1cd66f.jpg
 
Watu weusi tuna upumbavu wa milele
 
Back
Top Bottom