KERO Barabara ya Mtengu (kupitia Kilongoni Sheli ya TSN kuelekea Njia Nne kabla ya Daraja la Mtikatika) haijarekebishwa

KERO Barabara ya Mtengu (kupitia Kilongoni Sheli ya TSN kuelekea Njia Nne kabla ya Daraja la Mtikatika) haijarekebishwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hii changamoto tulisha itolea taarifa kwa Viongozi wetu wa Serikali za Mtaa lakini hakuna mabadiliko yoyote, barabara hiyo iliyoharibiwa na mvua kubwa ya mwaka Jana (2024) na vipindi vingine tena vya mvua vinaanza sijui hali itakuwaje!

Tunaomba Serikali itusaidie kutatua changamoto hiyo kuepukana na adha ya usumbufu.

Barabara hiyo inaunganisha Kilongoni yote kwa Juma Uhai, Kwa Buda, Kwa Chaula, na Njia Nne mpaka Vikindu Kituo cha Polisi, hii inasababisha hata maendeleo kurudi nyuma, Wafanyabiashara wa jumla hawawezi kuleta mzigo yao sababu ya miundombinu mibovu.

Serikali ya Kijiji cha Mkokozi na mwema, Mamlaka zinazohusika zirekebishe hii mapema kabla mvua hazijachanganya.

Hali hii imesababisha gharama za maisha kupanda ikiwemo Bodaboda na Bajaji hawataki kutumia njia hiyo, vitu tunapata kwa ghala kubwa sababu ya changamoto ya usafiri.

Tunaathirika Kisaikolojia kipindi hiki cha mvua, suala hili liwafikie viongozi wa Mkuranga - Pwani hasahasa Mkokozi na Mwema Nani.

IMG_20241210_154700_4.jpg
IMG_20241210_154656_8.jpg

IMG_20241210_154555_8.jpg
 
Back
Top Bottom