Barabara ya Mwendokasi kutoka Gerezani - Mbagala kukamilika Aprili 2023

Barabara ya Mwendokasi kutoka Gerezani - Mbagala kukamilika Aprili 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema awamu ya pili ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka kutoka Gerezani hadi Mbagala Rangi tatu, utakamilika Aprili.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3. Pia ujenzi wa vituo 27 vya mabasi ya mwendo wa haraka, barabara za juu tatu na njia za maji za chini zenye urefu wa kilomita 40.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Febuari 27, 2023 wakati akikagua ujenzi wa awamu ya tatu ya barabara ya kiwango cha zege ya mabasi yaendayo haraka kutoka Posta ya zamani hadi Gongo la Mboto yenye urefu wa kilomita 23.3 utakaogharimu Sh231 bilioni.

“Hivi karibuni tunakwenda kumaliza ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili. Katikati ya Aprili itakamilika kwa asilimia 100 tulipata changamoto ya daraja la juu kwa sababu tulichelewa kuwapa eneo.

“Hii ya awamu ya tatu itakamilika Machi mwakani, niwaambie tu wakazi wa Dar es Salaam, kabla ya uchaguzi mambo yatakuwa mazuri,” amesema Profesa Mbarawa.

Kuhusu ujenzi wa awamu ya tatu, Profesa Mbarawa amesema mkandarasi amejipanga vizuri kutekeleza jukumu hilo na ametembelea ghala lililopo Buza kuoana maandalizi yake.
 
Hizi za mwanzo tu zimeshinda ila wanataka mpaka Mbagala

USSR
 
Naona political target!! Nimepita barabara ya kawawa hadi Chang'ombe sijaona uwezekano WA hii barabara kukamilika by June 2023!! Anyway kila kitu ni siasa hata maprofesor!! By the way nimekutana na mambo ambayo wanatakiwa wayafanyie kazi na Sio kusubiria matatizo ambayo yapo dhahiri, ni hii section ya VETA hadi Chang'ombe Magari ya kawaida yamewekewa barabara nyembamba sana na huna overtaking!!! Hivyo basi tumekutana na Lori bovu tumekaa pale nusu saa!!

Sasa wasisubiri mkandarasi atoke site ndio wajue tatizo hili ni kubwa sana ila ni utashi WA kawaida!! Hawa wenye mradi (Brt) hawana shida na mixed Traffic ila sisi watumiaji tumeshaona tatizo na hatujui pa kesemea!!

Mheshimiwa Makalla RC, Tarura au Tanroads fanyeni hima msijitoe ufahamu!! Ushauri hata kama VETA pamebana kwingineko kuwe 4 Ways!! Hii itakuwa aibu ya Mwaka, Pia nimeambiwa matatizo hayo pia yapo njia ya tabata, njia ya mwai kibaki, Shime Shime wahusika
 
Njia moja kwa barabara ya short cut ya kwenda uwanja wa taifa wameweka njia moja. Hili ni janga
 
Sijui kwa nini wanapenda kutoa matamko na ahadi ambazo hazitekelezeki.
Bado kuna kazi nyingi kwenye barabara hiyo.
 
Tunataka bandari habari za barabara achana nazo kwanza
 
Hivi huyu si Magu alimuondoa? Mama anamtazama tu wakati anauza Bandari yetu, halafu tunaambiwa habari ya barabara kukamilika Aprili wakati hii ni Juni tena kati kati. Hivi hawa wanatuonaje sijui?
 
Back
Top Bottom