Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
 
Ndiyo yatakuwa yaleyale ya DART...

Yani hiyo barabara mpaka waje wairudishe ni mpaka pale hiyo barabara ichakae kwanza.

Hawataikabidhi kwa muda kwa visingizio vya hapa na pale hasa "Bado Hatujarudisha Chetu"..

Na hapo tenda ndiyo utakuta kuna mkono wa mkubwa mmoja.

Yani inshort ni kwamba hapa tayari kuna mkubwa kashaichukua hii tenda.

RIP JPM, ULISEMA TUTAKUKUMBUKA KWA MAZURI NA KWELI YANATIMIA.
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
 
Aliyejenga njia 8 Ubungo - Kibaha yeye hakuona umuhimu wa tozo au nyie ndio mnaijua sana hela?
Itakua Matumizi Mengineyo yamedizi tax collection, now hawana pesa za miradi to the point wamesahau kua teyari tunalipia toll kwenye mafuta(road fund).
sasa sijui wanataka tulipie kitu kile kile mara 2 au ndo kutaftiana madili with the so called wawekezaji?
 
Mambo ya kufikirika
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba [emoji23] mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Jule mwamba alikua mtu na nusu...alianzisha road fund ili tuweze kujenga barabara zetu wenyewe...naona walioachiwa wameshindwa kua na maono...
 
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
Hizi ni Zama za King Charles III
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Wanawarahisishia sana kazi upinzani. Wao wakisema tu kuwa watapunguza au kuondoa kabisa hizi tozo watanganyika wengi watawapa kura zao.

Amandla...
 
Hizi tozo zisipoangaliwa kwa umakini, ndio zinakwenda kuwa mfumo kamili wa maisha ya mtanzania, tutakatwa tozo kwenye kila kitu na kodi sijui matumizi yake yataishia wapi.

Huku tunalia tozo zipunguzwe, kule wengine wanawaza kututengenezea tozo mpya, ajabu.
 
Huu utaratibu wa PPP kwenye ujenzi wa barabara ni utaratibu sahihi na wenye ufanisi hasa ukizingatia hali ya uchumi wa nchi na mazingira ya miundombinu.

Utaratibu huu unatumika sana kwenye advanced economies, na umeleta transformation kubwa.
 
Ndiyo yatakuwa yaleyale ya DART...

Yani hiyo barabara mpaka waje wairudishe ni mpaka pale hiyo barabara ichakae kwanza.

Hawataikabidhi kwa muda kwa visingizio vya hapa na pale hasa "Bado Hatujarudisha Chetu"..

Na hapo tenda ndiyo utakuta kuna mkono wa mkubwa mmoja.

Yani inshort ni kwamba hapa tayari kuna mkubwa kashaichukua hii tenda.

RIP JPM, ULISEMA TUTAKUKUMBUKA KWA MAZURI NA KWELI YANATIMIA.
Je, Serikali itumie mikopo ya gharama kubwa kujenga au imtafute Sierra one mwenye mtaji na utayari wa kuwekeza kujenga kipande fulani cha barabara kwa makubaliano fulani ya kurudisha pesa yake na faida kupitia tozo bila kuiongezea mzigo serikali na wakati huo kuongeza accessibility?

Binafsi sera nyingi za hii serikali sikubaliani nazo, lakini kwenye hili naona a good step in the right direction.

Changamoto kubwa ninayoiona ni ulafi, wizi, na ubinafsi. KIJANI ni mafisi, na huwa hawana jema.
 
Back
Top Bottom