Barabara ya njia nane- Dar - Kibaha yakwama. Serikali yakanusha

Hii nchi ina mipango mingi ya Abunuasi, na inatakiwa iwepo sheria sasa ya kuwashughulia wahusika wa mipango ya kiabunuasi. Hivi ni kwa uchumi upi tulio nao wa kujenga barabara 8? Nani hasa alileta hili wazo? Kwa nini tusingejenga barabara 4 tuu (mbili za kwenda na mbili za kurudi? Au hata barabara yenye njia tatu ambayo ingeweza kufika hata mpaka Dodoma?? Tuache hizi ngonjera za kuiga kunya kwa Tembo jamani tutapasuka msamba bureee...
 
Walipwe fidia kwanza waliobomolewa nyumba zao kwa roho mbaya ya visasi aliyokuwa nayo mwendazake
 
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
Tulikuwa na Raisi wa ujenzi ndo mana aliiweza
 
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
Narudia tena na tena, tuwe na taasisi imara jamani, hivi JPM angeishi miaka 200 nyie?? Hii nchi ina watanzania milioni 60 hakuna kweli wenye uwezo wa kujenga taasisi imara isipokuwa mtu mmoja ambaye Mola amempenda zaidi?? Mfano wewe hapo hakuna chochote unachoweza kusaidia hii nchi yako? Huna hata kimoja unachoweza???
 
Ukweli usemwe chini ya huyu Mama hakuna miradi mikubwa itakayo kamilika... hii barabara ilishafika asilimia 98 kweli unashindwa kumalizia kipande kidogo kama hicho cha asilimia mbili? barabara nzuri kama ile aisee
 
Sawasawa hata hivyo si Hatuhitaji maendeleo ya vitu kama ilivokuwa inasema kauli maarufu ya wanaharakati na wanasiasa kipindi kile miradi ya ujenzi imekolea.
 
Tatizo la mwenda zake hakuwa na vipaumbele

Anarukia rukia tu mambo

Mara SGR,Mara ndege,Mara Barabara,Mara bwawa

Kote huko kuna cost hela ndefu sana

Alikuwa anatafuta misifa tu.

Kwanza hio Barbara ya morogoro road kawavunjia masikini wengine Sana nyumba zao bila fidia maana Barbara imewakuta hapo.

Kafa hajaona hata mmoja ukikamilika

Hela zenyewe za dhuruma na kupora watu

Roho mbaya haijengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…