Barabara ya njia nane- Dar - Kibaha yakwama. Serikali yakanusha

Barabara ya njia nane- Dar - Kibaha yakwama. Serikali yakanusha

Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba habari kama hii kipindi cha Mwendazake ingeandikwa? Huyo Mkurugenzi angeongea kama alivyoongea?? Angepewa majina yafuatayo; Mpinga maendeleo, anatumiwa na mabeberu, siyo mzalendo, kama ana PhD angeambiwa ana PhD fake, Polepole angeitisha press na kumtishia vibaya mnoo, then Magufuli angemwita majina yote machafu kwenye hotuba zake!! Baada ya hapo Uhamiaji na TRA wangemwandama, may be na watu wasiojulikana wangemtembelea pia, then wangemfuta kazi!! Baada ya miezi 6 tungesikia anapanda kizimbani kwa kesi ya uhujumu uchumi!! Miaka 5 ya jamaa yako tulikosa habari za namna hii za kuikosoa serikali, ni jambo jema sababu unaweza kuta kuna lijinga tu huko serikalini limekalia hela hata uongozi wa juu wa nchi haujui!! Tunategemea immediate measures from uongozi wa juu, ikiwezekana walitolee ufafanuzi pia. Heko waandishi...
 
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
Alikuwa anaiweza bila pesa?wakati ndio wizara iliyokuwa inapewa pesa zote nizazopitishwa na bunge?kwenye wizara ya ardhi , na uvuvi alifanya nini kikubwa sana, kwani kule pesa hakuwa anapewa kama wizara ya ujenzi!!unafikiria kama angepewa wizara ya elimu kuna kitu angefanya?tatizo wizara inapewa 30℅ya fedha iliyoomba hapo utegemee miujiza ipi?ilikuwa wizara ya kimkakati pesa yote alikuwa anapewa.
 
Hela si ulikuwa wewe na mwenda zake? Mmeiacha nchi mfilisi na mikopo kibao mcliochukua huku nusu yake ikiishia mifukoni mwenu
Mwanamume siku zote ndio mwenye nguvu ya kutafuta kwa jasho na damu, kwa ngumi na teke
 
Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba habari kama hii kipindi cha Mwendazake ingeandikwa? Huyo Mkurugenzi angeongea kama alivyoongea?? Angepewa majina yafuatayo; Mpinga maendeleo, anatumiwa na mabeberu, siyo mzalendo, kama ana PhD angeambiwa ana PhD fake, Polepole angeitisha press na kumtishia vibaya mnoo, then Magufuli angemwita majina yote machafu kwenye hotuba zake!! Baada ya hapo Uhamiaji na TRA wangemwandama, may be na watu wasiojulikana wangemtembelea pia, then wangemfuta kazi!! Baada ya miezi 6 tungesikia anapanda kizimbani kwa kesi ya uhujumu uchumi!! Miaka 5 ya jamaa yako tulikosa habari za namna hii za kuikosoa serikali, ni jambo jema sababu unaweza kuta kuna lijinga tu huko serikalini limekalia hela hata uongozi wa juu wa nchi haujui!! Tunategemea immediate measures from uongozi wa juu, ikiwezekana walitolee ufafanuzi pia. Heko waandishi...
Gaidi na Lisu wameongea sana licha ya kwamba hakuna mradi ulioshindwa enzi hizo
 
Rais Samia amesema hataki ujambazi wa kuwanyang'anya pesa watu kama alivyokuwa anafanya marehemu.
Ndipo umeulizwa pesa zimekwenda wapi, mbona unang'atang'ata maneno?.
 
Alikuwa anaiweza bila pesa?wakati ndio wizara iliyokuwa inapewa pesa zote nizazopitishwa na bunge?kwenye wizara ya ardhi , na uvuvi alifanya nini kikubwa sana, kwani kule pesa hakuwa anapewa kama wizara ya ujenzi!!unafikiria kama angepewa wizara ya elimu kuna kitu angefanya?tatizo wizara inapewa 30℅ya fedha iliyoomba hapo utegemee miujiza ipi?ilikuwa wizara ya kimkakati pesa yote alikuwa anapewa.
Utanyooka tu na roho yako ya korosho
 
Rais Samia amesema hataki ujambazi wa kuwanyang'anya pesa watu kama alivyokuwa anafanya marehemu.
Huwezi kuendelea bila mapambano ya jasho na damu
Ulaya wameendelea kwa kuwakamua waafrika
Waafrika tukamuane wenyewe, hata Samia alisema hivyohivyo

My take: Ukamuaji ni kwa matajiri sio wanyonge!
 
Tatizo la mwenda zake hakuwa na vipaumbele

Anarukia rukia tu mambo

Mara SGR,Mara ndege,Mara Barabara,Mara bwawa

Kote huko kuna cost hela ndefu sana

Alikuwa anatafuta misifa tu.

Kwanza hio Barbara ya morogoro road kawavunjia masikini wengine Sana nyumba zao bila fidia maana Barbara imewakuta hapo.

Kafa hajaona hata mmoja ukikamilika

Hela zenyewe za dhuruma na kupora watu

Roho mbaya haijengi
Bara bara imeshaamalizika mbona yaan magu alifikisha 96% hiyo asilimia 4 anashindwa kumalizia mamaa Aache uvivu
 
Hivi palikuwa na ulazima gani wa kuifungua na kuanza kuitumia hiyo stendi kabla haijakamiliaka?
 
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
Mkuu, kwako wewe Magufuli alikuwa na uwezo wa kipekee? Ulimfahamu lakini? Au kwa kumsikiliza tu?
 
Tatizo la mwenda zake hakuwa na vipaumbele

Anarukia rukia tu mambo

Mara SGR,Mara ndege,Mara Barabara,Mara bwawa

Kote huko kuna cost hela ndefu sana

Alikuwa anatafuta misifa tu.

Kwanza hio Barbara ya morogoro road kawavunjia masikini wengine Sana nyumba zao bila fidia maana Barbara imewakuta hapo.

Kafa hajaona hata mmoja ukikamilika

Hela zenyewe za dhuruma na kupora watu

Roho mbaya haijengi
Na wewe ni wale wakudandia magari kwa nyuma achana na siasa focus on your life.
Narudia si kila unachosikia ni kweli
 
Barabara iliyokuwa inajengwa kwa kasi ya njia nane kutoka Dar hadi Kibaha imekwama kumalizika ujenzi wake kutokana na ukosefu wa fedha,Tanroads wamebainisha.

Waziri wa ujenzi prof Mbarawa alipotafutwa kutolea ufafanuzi madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa.

My take.
Chadema meno yote nje kwa furaha kwa sababu hii ndiyo njia pekee ya Lisu kumkomoa hayati Magufuli. Yani miradi ya watanzania ishindwe kukamilika ili wawe na maisha magumu.

========

barabarapic.jpg

Dar es Salaam. Licha ya umuhimu wake kwa uchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mikoa jirani na Taifa kwa ujumla, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara (Tanroads), Rogatus Mativila amesema wanashindwa kumalizia kujenga kipande cha kutoka Kimara hadi Kibaha na barabara za kuiunganisha barabara hiyo ya Morogoro na Kituo cha Mabasi cha Magufuli kutokana na ukosefu wa fedha.
“Kimsingi bado ujenzi unaendelea na hatuwezi kutoa mapipa yaliyopo kwenye Barabara ya Morogoro haraka, kwani itapunguza usalama hivyo kuongezeka ajali,” alisema Mativila.

Alisema wameomba fedha ili kukamilisha sehemu hizo na kuondoa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Katika barabara hiyo inayoendelea kujengwa ikiwa na njia nne za kwenda na nne za kurudi, Tanroads wameweka zaidi ya mapipa 4,280 na kingo 274 za zege kutenganisha mpaka na sehemu ya katikati ambayo ni kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).

“Tumeomba fedha za nyongeza serikalini ili kutengeneza kwa lami kipande cha barabara kutoka stendi na barabara kuu ili kuondoa changamoto ya matope pindi mvua inaponyesha,” alisema Mativila.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa fedha nyingine zitatumika kujenga mawe ya pembeni mwa Barabara ya Morogoro ili kutengeneza mipaka ya barabara hiyo na eneo linaloachwa kwa matumizi mengine.

“Kwa sasa gapestone (kingo) tulizoweka katikati hatuwezi kutoa, kwani tukifanya hivyo tunaweza kusababisha ajali nyingi, kwani madereva wengi wataendesha magari kwa kasi kutokana na uwazi kuwa mkubwa,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kujua kiasi cha fedha zilizoombwa na Tanroads, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, alijibu: “Mimi ndiyo ninafanya mambo mengi. Tutaiweka kwenye utaratibu ili iende vizuri”.

Stendi ya Magufuli

Kwa upande mwingine, uongozi wa Manispaa ya Ubungo umetoa ufafanuzi kuwa changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa ujenzi wa baadhi ya maeneo ya Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Luis ni kutotolewa kwa fedha zinazohitajika kwa wakati.

Ujenzi wa stendi hiyo kwa ajili ya mabasi yaendayo mikoani ulioanza Februari 2019 bado haujakamilika kwa asilimia 100, jambo linalosababisha usumbufu kwa magari yanayosimama wakati wa kupakia na kushusha hasa usiku na asubuhi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mhandisi wa Manispaa ya Ubungo, Masodoya John ambaye ni msimamizi wa mradi wa ujenzi wa stendi hiyo inayojengwa na kampuni ya Hainan ya China, alisema wanategemea mapato ya ndani kuendeleza ujenzi huo.

“Nikiri malipo huwa yanachelewa lakini sio kwa muda mrefu sana kiasi cha kuathiri utendajikazi kwa sababu ndani ya siku 18 mkandarasi anatakiwa awe ameshalipwa. Kukiwa na mapungufu kwenye kuwasilisha nyaraka ikaonekana kuna sehemu inatakiwa ufafanuzi kwa mwajiri ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa manispaa, fedha zinachelewa kutoka,” alisema.

Mtaalamu huyo wa ujenzi alifafanua: “Unaweza kukuta hazijaja tarehe 10 kwa sababu ya mapungufu katika kuandaa nyaraka za malipo.” John alibainisha changamoto nyingine zinazochelewesha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kuwa ni kufanya usanifu wa mara kwa mara.

“Kitendo cha magari kulala eneo lile kunaweka ugumu. Kuna wakati tunalazimika kuruhusu magari kutoka na kuingia na changamoto hiyo inamlazimu mkandarasi kusimamisha ujenzi wakati mwingine. Hili linasababishwa na kulitumia eneo kabla ya ujenzi haujaisha,” alisema John.

Mhandisi huyo alisema mkandarasi wa mradi huo anajitahidi kutekeleza kila hatua kulingana na mkataba unavyotaka ambao unadumu hadi Desemba mwaka huu atakapomaliza ujenzi na kukabidhi mradi.

“Mategemeo yetu Desemba tunakabidhiwa mradi wetu ukiwa tayari ili tuanze kulitumia eneo kulingana na malengo yaliyokusudiwa,” alisema John, anayeamini baada ya kukamilika kwa ujenzi huo changamoto hizo zitaisha kwa asilimia kubwa, kwa sasa sehemu iliyokamilika yanasimama mabasi 104. Stendi hiyo ina sehemu ya kuegesha mabasi 204 kwa wakati mmoja, hivyo kukamilika kwake kutawanufaisha wananchi wanaoelekea maeneo tofauti kupitia Barabara ya Morogoro.

John alisema ujenzi wa stendi hiyo yenye thamani ya Sh50.9 bilioni bado unaendelea na kwa sasa mkandarasi anajenga daraja sehemu ambako mabasi yanaingilia.

Chanzo: Mwananchi

Kwani Lissu hana uhuru wa kujisemea mwenyewe
 
Tatizo la mwenda zake hakuwa na vipaumbele

Anarukia rukia tu mambo

Mara SGR,Mara ndege,Mara Barabara,Mara bwawa

Kote huko kuna cost hela ndefu sana

Alikuwa anatafuta misifa tu.

Kwanza hio Barbara ya morogoro road kawavunjia masikini wengine Sana nyumba zao bila fidia maana Barbara imewakuta hapo.

Kafa hajaona hata mmoja ukikamilika

Hela zenyewe za dhuruma na kupora watu

Roho mbaya haijengi
Kwa hoyo yeye hela alikuwa anatoa wapi?
 
Gaidi na Lisu wameongea sana licha ya kwamba hakuna mradi ulioshindwa enzi hizo
Acha ujinga wewe jamaa, SGR to Morogoro si ilikuwa ikamilike 2019? Hadi leo nini kimekwamisha? Hiyo barabara nayo ilikuwa ikamilike mwaka huu mwanzoni lakini hamna kitu!! Airport Msalato jamaa yako alikuwa anapiga sound tu, kila siku anasema tumeshatangaza tenda, mother kaingia ameshatoa hela mradi unaanza!! Mwendokasi phase 2 na 3 hadi leo haieleweki, juzi tu wafanyakazi wamegoma hawajalipwa since 2020!! Mabus ya mwendokasi yenyewe alishindwa kununua, mother kaingia tu kaingiza mabus 70 barabarani!! Propaganda zenu za kijinga zimeshashtukiwa!! Lissu na mbowe kama registered opposition lazima waongee, ndiyo ajira yao hiyo, walishajichagulia siasa ndiyo njia yao ya kuishi, hivyo wataongea tu, tena sanaaa, na hamna wa kuwazuia...
 
Chadema meno yote nje kwa furaha kwa sababu hii ndiyo njia pekee ya Lisu kumkomoa hayati Magufuli. Yani miradi ya watanzania ishindwe kukamilika ili wawe na maisha magumu.
Uandishi wa kishabiki mno hata mahali pasipokuwa na lazima ya kuweka ushabiki!
 
Back
Top Bottom