KERO Barabara ya Singida-Babati-Arusha ni mbaya ina mashimo ya kutosha, wahusika hili mnaliona tunaomba mlishughulikie hali ni mbaya

KERO Barabara ya Singida-Babati-Arusha ni mbaya ina mashimo ya kutosha, wahusika hili mnaliona tunaomba mlishughulikie hali ni mbaya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Singida–Babati–Arusha ina mashimo mengi na hali yake ni mbaya. Wahusika, je, mnaliona hili? Tunaomba mlifanyie kazi kwani hali ni mbaya.

IMG_20250413_093124_835@1613294015.jpg
IMG_20250413_093301_007@1613294019.jpg

~ TANROADS: Tunaendelea na matengenezo barabara ya Singida–Gehandu pamoja na Singida - Manyara
 
Ni eneo la Endasak Wilaya ya Hanang, ni kweli barabara Ile Ina mashimo Sana kipande kile

Ubovu wa Barabara unaanzia Kata ya Masakta Hadi Endasak. Ukipita Dareda mbele. Changamoto hiyo ni ya Muda mrefu na hiyo ni barabara kuu
 
Strategic solution ni maximizing utilization of rail. Mtu ataniuliza reli na huko Hanang wapi na wapi? Jibu linapatikana kwa kuweka incentive kwenye rail na kuongeza carbon taxation. Mzigo ukitoka Tanga lazima utawekwa kwenye MGR kwenda Ruvu then SGR to Western maana huko Hanang ni transit tu. Swali la msingi treni ya mzigo ya SGR imeanza kazi? Jibu analo Kadogosa.
 
mnatakiwa hata mshukuru kwasababu licha ya mashimo vado kuna lami ...nendeni njombe huko ludewa muone jinsi barabara zilivyo
 
Kipande cha Singida-Kona kipo safi kabisa. Pia Kipande cha DAREDA-Babati kipo safi, mkeka safi kabisa, mtelezo. Kipande cha Babati-Magugu napo ni mkeka safi kabisa, mtelezo. Mkeka mwingine safi kabisa, ni kuanzia Minjingu hadi Arusha.

Vipande vyenye shida kubwa sana katika barabara ya Singida - Arusha ni Kona ya Singida-Katesh, Katesh-Dareda, Maguugu-Mbuyu wa Mjerumani-Minjingu
 
Back
Top Bottom