Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuandika juu ya kero ya barabara itokayo Tabora Mjini kuelekea Igalula, Goweko na Makibo kupitia Ndevelwa hatimaye kipande cha Kilometa 30 Igalula-Ndevelwa-Tabora Mjini kimeanza kufanyiwa kazi kwa maboresho.
Kero ya Mdau ~ Barabara ya Tabora Mjini hadi Igalula ni mbovu, inatutesa watumiaji
Ukarabati wa barabara hiyo ambayo ni kiunganishi cha huduma kwa Kata 5 huku Kata 3 zikiwa za Wilaya ya Uyui, Kata moja ya Tabora Manispa na moja ya Wilaya ya Sikonge.
Awali, Wananchi walikuwa wakipata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara hiyo, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za nauli hali inayosababisha bidhaa kupata bei kulingana na gharama za usafirishaji.
Pia katika huduma za afya ilikuwa ni changamoto pindi mgonjwa anapopewa rufaa kutoka katika Kituo cha Afya Igalula kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete) kulingana na ubovu wa barabara uliokuwepo
Barabara hiyo inahudumiwa na Halmashauri 3 kulingana na vipande vya maeneo husika, Tabora Manispaa, Uyui na kibande cha Nsololo-Makibo ambacho Kilometa 10 zipo upande wa Wilaya ya sikonge