Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 16,480
- 38,367
Wakuu tuseme tu ukweli hii nchi bado ni ya hovyo sana, hizi barabara kipindi cha mvua ni mtihani sana hasa ukiwa na gari ya chini!
Ukiwa unapita hizi barabara kuu unaweza ukasema mji si ndo huu! Sasa jana nilitoka Kimara nikaenda Tabata, mtaani kwetu kuna madimbwi ila sio ya kutisha kushindwa kupita.
Muda wa kwenda nilipita Ubungo hivyo hakukuwa na changamoto yeyote zaidi ya foleni, sasa wakati narudi mwenyeji akanishauri nipite Kimanga kisha maji chumvi maana ni shortcut, picha linaanza ile nakatisha tu njia ya Kimanga nimekutana na madimbwi ya kutosha(nina miaka kama 10 sijawahi pia huko Kimanga), nikajiuliza huku si kulikuwa na lami kwani imekuwaje? Sijapata majibu bado.
Hicho kipande chenyewe cha kuunganisha Tabata na maji chumvi ni mqjanga maatupu, yaan ile maana ya shortcut inakuwa haipo tena!
NB; Huko mtaani kwako hali ya barabara ikoje, kama Dar tu imetushinda ni lini nchi nzima itakuja kupata barabara nzuri?