KERO Barabara za mitaani za lami Dar zimetoboka sana, TARURA changamkeni

KERO Barabara za mitaani za lami Dar zimetoboka sana, TARURA changamkeni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Barabara nyingi za pembezoni jijini Dar es Salaam zipo katika hali mbaya sana kufikia Juni 2025, zimetoboka kupita kiasi.

Tunatoa wito kwa TARURA kuchukua hatua za haraka kuziba matundu hayo.

Kwa sasa, jiji linakabiliwa na msongamano mkubwa wa magari kutokana na ujenzi wa miundombinu ya mwendokasi unaoendelea, hasa katika maeneo ya katikati ya jiji.

Hali hii imeongeza utegemezi wa barabara za pembezoni, ambazo kwa bahati mbaya nyingi pia zimeharibika vibaya – hususan Tabata, Mbezi Beach, Ununio na maeneo mengine.

TARURA /TANROADS ni muhimu sana kuchukua hatua sasa.

Wananchi wanapoteza muda mwingi barabarani kutokana na uharibifu wa njia mbadala uliosababishwa na mvua ambazo zingesaidia kupunguza foleni. Mfano halisi ni barabara ya chini (ya mkato) kutoka Boko Chama hadi kwa Mwamunyange ambayo imeharibika ikiwa na matundu lukuki, huku Tabata pia barabara kadhaa zikiwa zimetoboka, hali ikiwa mbaya wananchi wakipoteza muda njiani.

TARURA, fanyeni jitihada za haraka kurejesha hali ya barabara hizi – wananchi wanahitaji suluhisho, tunajua bajeti ipo!.
 
Hata TARURA wajenge barabara vip kwa mtindo huu wa BANDARI kavu kujengwa mpaka Vichochoroni na kufanya milori mikuuuuubwa kupita Barabara zisizo na uwezo wa kupitisha Malori hayo ni sawa na kuruhusu Unajisi na Ubakaji.

Barabara mzuuuuri za Mtaani za Lami zimekwisha kwa huu upuuuzi.
Pita barabara ya MCHICHA pale TAZARA kutokea MIKOROSHINI utalia.
 
Back
Top Bottom