Kuna mtu mmoja alipoteza maisha kati ya 10 ambao walikuwa vibarua waliokuwa wamebebwa ndani ya Fuso hilo, wengine wakipata majeraha mbalimbali.
Dereva naye ni mmoja alibanwa miguu ilibidi jitahada za ziada zifanyike kutolewa kwani alikuwa amebanwa kwenye Skani.
Nimeanza na mfano huo kwa kuwa hiyo ni mara ya pili gari kama hilo la kupata ajali ndani ya mwezi mmoja.
Pamoja na vyanzo kudaiwa kuwa ni kupasuka kwa mipira lakini kuna haja ya Serikali kuboresha barabara za Pemba kwa kuzitanua.
Hatari zaidi ni magari makubwa, yakiendeshwa ovyo inakuwa hatari zaidi kwa kuwa shida ni wembamba wa Barabara
Ukiachana na vyombo vya moto, pia kuna Wanyama na Watu wanaopita kando ya Barabara, hali hiyo inafanya mazingira kuwa magumu zaidi.