Barabara zilizojengwa na China magharibi mwa Kenya zaleta mageuzi kwenye eneo hilo la kilimo

Barabara zilizojengwa na China magharibi mwa Kenya zaleta mageuzi kwenye eneo hilo la kilimo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
4E894B2DFCB07D2FE0C66E99F5F552387C20268F_size3439_w5304_h2984.jpg


Kwa miongo kadhaa, maisha katika Kaunti ya Uasin Gishu, kitovu cha kilimo magharibi mwa Kenya, yalitambuliwa kwa maziwa na mahindi, na wakati mashamba yake yakilisha taifa la Kenya, wakulima wa huko walikabiliwa na changamoto ya kila mara ya kusubiri malipo ya kupakia mahindi, na hii ilitokana na mtandao mbaya wa barabara.

Mandhari hii maarufu sasa inabadilika kwa kasi, kwa mchanganyiko wa barabara kuu mpya, uvumbuzi wa teknolojia za kilimo, na upatikanaji wa soko pana la kimataifa vinabadilisha simulizi ya kiuchumi ya moja ya vitovu vya uzalishaji wa chakula nchini Kenya. Katikati ya mabadiliko haya ni nguvu kubwa ya miundombinu inayoongozwa na kampuni za uhandisi za China chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambapo barabara mpya za pembezoni zilizojengwa zinabadilisha shughuli za kilimo katika kanda hiyo.

Kichocheo kikubwa cha ukuaji huu ni barabara ya kando ya Eldoret yenye urefu wa kilomita 32 iliyojengwa na kampuni ya Wu Yi ya China. Kwa kuchepusha usafirishaji wa mizigo mikubwa mbali na katikati ya mji wa Eldoret wenye msongamano, barabara hiyo imetengeneza njia isiyo na vikwazo ya mizigo inayokwenda Rwanda, Uganda, na Sudan Kusini. Shoroba muhimu za kando kama barabara ya Cheplasgei-Maili Tisa pia zimepunguza muda wa usafirishaji wa bidhaa za kilimo kutoka shambani hadi ghalani kwa nusu.

Kutokana na maboresho haya ya mtandao wa barabara, wakulima wa huko wanafanya mabadiliko kutoka kilimo cha jadi cha mahindi na kuingia kwenye bidhaa zenye thamani katika soko la nje kama vile parachichi, maharagwe, maua mabichi na matunda ya pesheni. Majukwaa ya teknolojia ya kilimo kwa sasa yanawaruhusu wakulima wadogo kukusanya mazao, kufuatilia mnyororo baridi wa ugavi, na kuingia katika masoko ya kimataifa. Kwa kuboreshwa kwa muda wa usafiri, mazao yaliyovunwa alfajiri yanaweza kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Eldoret jioni, na kufika katika rafu za maduka makubwa ya Ulaya na Mashariki ya Kati ndani ya saa 36.

Mfugaji wa huko John Korir anakumbuka taabu alizopata zamani kabla ya miundombinu ya barabara kuboreshwa, akisema kufikisha maziwa mabichi katika viwanda vya kuchakata ilikuwa ni mbio dhidi ya muda mara kwa mara. Kutokana na barabara mbovu, zenye matope wakati wa msimu wa mvua, kuchelewa kwa usafiri mara nyingi vilisababisha maziwa kuharibika kabla ya kuwafikia wanunuzi, na hivyo kuleta hasara kubwa. Lakini hii leo, Korir anasema mtandao bora wa barabara umebadili kabisa utendaji wake, kwani magari ya kukusanya maziwa sasa yanafika mpaka kwenye geti la shamba lake mara mbili kwa siku bila kukosa, na kumwezesha kusambaza mazao mabichi bila ya hofu ya kuharibika, na hivyo kupata kipato cha uhakika, na kuwekeza tena katika kuongeza mifugo yake.

Maofisa wameelezea ujenzi wa miundombinu ya barabara katika kanda hiyo kama mkakati wa makusudi wa muda mrefu, wakisema barabara mpya za pembezoni na shoroba zinazoingiliana katika kaunti zilipangwa maalum kufungua fursa za kiuchumi za eneo hilo. Gavana wa zamani na seneta wa sasa wa Uasin Gishu Jackson Mandago anasema, mtandao wa barabara walioupanga, kuanzia barabara za kando hadi muunganiko katika kaunti, zilijengwa kwa mkakati wa wazi wa kuibadili Eldoret kuwa kusanyiko la asili na kituo cha usafiri kwa Afrika Mashariki, na matunda ya miundombinu hiyo yanaonekana hivi sasa.

Lami inateremka katika Bonde la Ufa, majukwaa ya kidijitali yanawaunganisha wakulima wadogo na wasafirishaji mizigo, na hadhi ya mji mpya wa Eldoret inaweka msingi wake kama kituo cha bara. Simulizi ya Uasin Gishu kwa sasa haijadhibitiwa tu kwenye malori ya maziwa na mahindi, ni simulizi ya ghala ya nafaka inayojijenga yenyewe kama njia ya kupaa kwenda duniani.
 
Back
Top Bottom