Barack Obama: Donald Trump amechangia kuongezeka kwa Gharama za maisha Duniani

Barack Obama: Donald Trump amechangia kuongezeka kwa Gharama za maisha Duniani

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amemshambulia vikali Rais wa sasa Donald Trump wakati wa mikutano ya kampeni katika majimbo ya Ohio na Michigan akiwahamasisha wapiga kura kuwaunga mkono wagombea wa Chama cha Democratic kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula.

Obama alisema utawala wa Trump umechangia kuongezeka kwa gharama za maisha, akidai baadhi ya maamuzi ya rais huyo, ikiwemo kuanzishwa kwa vita dhidi ya Iran, yameathiri uchumi na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta.

Obama aliwataka wananchi kupigia kura mabadiliko huku akiwaunga mkono wagombea wa Democratic kama Sherrod Brown na Abdul El-Sayed. Kwa upande wake, Trump alimjibu kupitia mtandao wa Truth Social, akimkosoa Obama na kutetea sera zake dhidi ya Iran.

Mjadala huo unaonyesha mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya Democratic na Republican huku pande zote zikisaka kura muhimu za kuwania udhibiti wa Bunge la Marekani

Chanzo : Dw swahili
 
Hili hata mtoto mdogo anajua yule Trump ni kavu sana anaanzisha vita ili mafuta wapate USA peke yao tena kwa bila kutoa hela harafu Nchi zingine wanapata kwa gharama kubwa kavu sana yule mzala sasa hivi kakimbilia Russia na katoa baadhi ya vikwazo ili apate mafuta ya bure..
 
Bora hata Trump amemtandika Iran huyo Obama ndio alikuwa anawagawia mabilioni Kila mwezi, ndio wameenda kutengeneza mitambo ya nuclear. Akae kimya huyo tapeli.
 
Hiyo ndiyo faida na uzuri wa demokrasia ingekuwa Tanzania ndio unamkosoa rais hivyo ungepotezwa na wasiojulikana mara moja au kufunguliwa kesi feki ya uhaini.
 
Wastàafu wanawashwawashwa😂 ule uhuni alioufanya palle libya nani aliyemnyooshea kidole?
 
Obama yeye mwenyewe ni wa ovyo tu yeye si ndo aloanza kampeni za ugasho na kusababisha jamii kuharibika mpaka leo
Huo Ushoga ulikuwepo kabla ya Obama, acha kuongea uongo.
Yeye kaamua kuweka ukweli na kuukana unafiki.
 
Hiyo ndiyo faida na uzuri wa demokrasia ingekuwa Tanzania ndio unamkosoa rais hivyo ungepotezwa na wasiojulikana mara moja au kufunguliwa kesi feki ya uhaini.
Hivyo vyama ni sawa na kimoja 😃😃undanganywa USA ina mfumo mmoja ,hivyo vyama viwili ili vyote vinamsujudia mtu mmoja ..Hakuna chama kinashirikiana na watu wa nje kama communist..Huyo Obama ,ndiye alimuua Gaddafi..

Hao wote wanafiki ,USA ina chama kimoja haina ukosoaji ,hapo hakuna ukosoaji ila wanawapumbaza wajinga..USA ukienda kinyume hata kama ni Rais unauliwa ,ilikuwa kwa Kennedy .

Jiulize ,walisema Trump alianzisha vita bila ya congress's approval, mbona hakuna hatua hata haipiti mieizu atashambulia tena 😃😃na baada ya kuhojiwa alishambulia ,tena na tena mbona hakuna hatua?

Mnadanganywa nyie wanuka midomo ,USA hakuna demokrasia ,Wana mfumo wa sera Moja na chama kimoja chenye matawi ..Wote wanamsujudia kiumbe kimoja.
 
trump ni jau yule mzee, putin na nyau wana mafaili yake ya epstein ndio maana anawatii sana
 
Huo Ushoga ulikuwepo kabla ya Obama, acha kuongea uongo.
Yeye kaamua kuweka ukweli na kuukana unafiki.
Yani wewe tena usitetee ugasho

Yani hpo unajihisi roho baridiii kweli kweli
 
Back
Top Bottom