Baraka Mpenja ana mengi ya kujifunza kutoka kwa Gharib Mzinga

Baraka Mpenja ana mengi ya kujifunza kutoka kwa Gharib Mzinga

chamakh

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
1,075
Reaction score
1,343
Ukiangalia namna wanavyopangwa Watangazaji wa Azam TV utaona kuwa Baraka Mpenja ndiyo Mtangazaji namba 1 hivyo hupewa mechi nyingi kubwa au zile zenye mvuto. Utaratibu huu pia upo kwenye Channel kubwa za Kimataifa kama Sky Sports, BT Sports pamoja na ITV ( Uingereza) ndiyo maana Peter Drury hupewa mechi nyingi kubwa kule BT Sports.

Baraka Mpenja sio Mtangazaji mbaya ila anapenda sana kuongea mambo yasiyohusiana na Soka wakati anatangaza. Baadhi ya mapungufu yake ni kama ifuatavyo.

1. Kupenda kutaja baba yake anamsikiliza. Hii sio pointi. Ingekuwa kila Mtangazaji katika kila kipindi anamtaja Baba yake au Mama yake kwenye kila mechi/kila kipindi ingekuwa too boring. Aache hayo na kupenda kutaja kina Lawina Nsonda au wanamlipa nyuma ya pazia?

2. Akiona Mashabiki wanawake utamsikia Mashallah maua maua, huku akicheka cheka hovyo. Hii ni tabia mbaya. Inamuonesha sio mtu mwenye maadili lakini ni very unprofessional. Wengine ni wake za watu wapo uwanjani , hayo maneno anayotamka hayana connotation nzuri hata kidogo. Aache awe focused na kilichompeleka kutangaza.

3. Kutumia lugha/ maneno yasiyo na kichwa wala miguu. Utasikia nanunua pasi moja milioni moja, pasi milioni mbili, milioni kumi. Hayo maneno hayana mantiki. Ajikite kutaja idadi ya pasi na ubora wa timu sio kutaja figures zisizo make sense.

4. Aache kutaja masuala ya Siasa na Vyama akitangaza mpira. Kwenye mechi na Viwanja hata kama kuna CCM aachane na hayo maneno, hajui Wangapi hawana affiliation na hicho chama na wasingependa kukisikia.

Nasema ajifunze kwa Gharib Mzinga huyu ni very composed commentator. Tunaona kule Bundesliga, alivyotangaza AFCON 2021 na hata anavyotangaza mechi za CAF unaona alivyotulia.

Anajua kueleza matukio yaliyopo uwanjani, hatoki nje ya matangazo na hana lugha zisizofaa. Bahati mbaya naona Gharib hatangazi mechi za Ligi ya NBC but he is one of the best pale Azam TV. Mpenja ajitahidi kumuiga huyu mwenziwe.
 
No.1 uko sahihi nadhani amechukua ushauri.

No.2&3 hazina madhara ni kunogesha soka maana soka haiendi peke yake bila vionjo. Ndo maana wengine hujichora rangi mbalimbali, wengine hubeba na kupuliza Vuvuzela ambalo halihusiani na soka.

NO.4 AACHE UTOTO. Tukio alilolifanya ya Mechi ya Yanga na Mbeya City ni UPULUZI.
 
GHARIB MZINGA ni promising talent nyingine pale Azam TV binafsi napenda style ya utangazaji wake,

Baraka Mpenja sauti ya radi kama anavyopenda kujiita inabidi ajirekebishe kwa mapungufu aliyonayo, umaarufu alioupata asianze kuvimba kichwa

Naamini JF ni mtandao mkubwa hizi habari zimfikie, ni kwa nia nzuri

Tupo wengi tunaokukubali, keep it up
 
Gharib mzinga, Pascal kabombe na alwatan ngoda ndio watangazaji wanaonivutia kwangu Mimi,na kuna yule jamaa anasauti kama ya Charles Hilary kule Zanzibar jina limenikimbia kidogo.

Ila ukitaka kupata ladha ya utangazaji halisi wa mpira msikilize Enock Bwigane na Jesse John.

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
Hiyo staili yake nadhani ndiyo imemfiksha hapo akiondoa hayo manjonjo atakuwa siyo Mpenja tena
 
Binadam tupo tofauti kabisa mpaka kafika pale ujue watu wengi wanapenda vile watu wangekuwa hawapendi nadhani asingefika pale alipo.
 
Gharib mzinga alikuwa vizuri tangu tupo shule pale mahiwa high school Lindi, aliupenda Mpira kuliko chochote..Ilikuwa kabla hatujaingia class asubuhi tunakaa nje huku tunaota jua la asubuhi tunabishana maswala ya Mpira na yeye alikuwa anajua kuuchambua na ana kipaji cha kuhadithia matukio hata ya miaka ya 90

Kupitia yeye nimeamini ukipenda kitu na kuamua kukipambania lazima ufanikiwe.Kila mechi anayotangaza namcheki na kumtia moyo apambane zaidi,ili awe mbali zaidi..napenda mafanikio yake
 
Back
Top Bottom