Baraka Mpenja ana mengi ya kujifunza kutoka kwa Gharib Mzinga

Huyu wa Unguja ananiboa kabisa kabisa na hunifanya nihame chaneli nikimsikia. Kinachonikera ni hicho cha kumuiga Hilary, ajifunze kusimama yeye mwenyewe na si kipitia bahati ya mwengine.
 
Mpenja n kabila yangu kabisa na jiran yangu kutoka santilya mbeya kuna mapungufu anayo akirekebisha atakua bonge la mtangazaj
 
JAMANI NJOENI , MPENJA MWENYEWE UYU HAPA 👆👆😂😂😂😂😂
 
Ni wivu tu.
Kwa hiyo mpenja awe sawa na ngoda, ibwe au hillary?
Lakini nimependa umeshauri nini aache na nini aongeze.
 
wewe ni UTOPOLO bisha??
 
Kweli kila mtu na mtuwe,
Mimi the best of them ni Iddy Kidedea "Ulamaa".
 
Hata mim huyu dogo huwa simkubali ingawaje watu wanampendea hayo hayo maujinga yake

Ukisikiliza anavyotangaza anaongeaga mambo mengi sana
 
Ghalib ndio anajua kutangaza mpira
 
Napenda ma commenter wa ki Spain japo sielewi hua wanaongea nini hasa goal likifungwa
 
Ghalib Mzinga mzee wa takwimu. Huyu ni Yusuph dayo,anachezea clab fulani,msimu huu kacheza mechi kadhaa katia assist kadhaa,na magoli kadhaa. Wakati Berkane wanashinda kombe la shirikisho mwka 2019 ndio mfungaji wa goli pekee.
 
Gharib mzinga ni noma sana kwenye utangazaji anawafaham wachezaji uwezo wao na historia ya mchezaji
Jamaa yupo vizur sana anamzid mbali sana Mpenja..
 
Nimeamini kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.
 
Ghalib Mzinga ni habari nyingine kabisa

Amenikosha sana ktk michuano ya Afcon, anajua kutangaza, anajua historia ya wachezaji, anajua historia ya nchi kuanzia kisoka mpaka ktk siasa za nchi husika, anajua mpk referees wanatokea nchi gani walichezesha mechi zipi na walileta gumzo lipi

Kwa ufupi jamaa anajua mambo mengi sana ktk soka ndani na nje ya uwanja

Kumsikiliza ni burudani sana sana

Kiukweli naomba Azam Media wamuongezee mshahara huyu kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…