Naomba nichukue nafasi hii kumponda rais JK kwa baraza mbovu na ya kiushikaji aliyouweka.
Siwezi amini kwamba wana_JF mnasema tuwape muda? wa nini?
- Ni sura ngapi mpya zilizoongezwa kwenye baraza? 3 au 4
- Wengine waliobaki wote walikuwa kwenye cabinet iliyopita, je walitenda kazi ipasavyo, waliboronga au they just lived through another day? Watendaji wazuri walikuwa 2 au 3 by anyone's estimate kama vile Magufuli. Wengine walilala tu au kusimama kusema ujinga. Kati ya waborongaji wa kubwa waliobaki ni Chiligati (labor market is a chaos!), Wassira (wakulima wa korosho watamlaaani milele) etc
- Sura mpya zinasemaje? Dkt Mwinyi mnayemsifia eti mchapakazi,mmh, na hiyo digrii yake feki hata madaktari enzake Muhimbili hawakumkubali. Nchimbi ndo huniambi kitu! Eti mnataka kuwalinganisha Moringe Sokione and Salim Ahmed Salim na hawa? PLZZZZ
- Kaendeleza ule ushikaji wa kulipa fadhila. Malima? Kalipwa fadhila kwa ajili ya kuwa 'attack dog' against Mengi? Na alidhihirika kusema uwongo bungeni! Integrity : 0!
- Kupunguza cabinet haikuwa mjadala, he just went back to the good old days, alicho'tunga' ukubwa wa cabinet in 2006 kwa ajili ya ushikaji, kairudisha katika hali yake ya Mkapa era. Nothing creative about it. Na elimu kazidi kuboronga eti kaunganisha Elimu ya Juu na Elimu ya msingi+sekondari+ufundi. Alafu kaongeza District Education Officers wawe wawili kila wilaya, sasa hii si kuongeza gharama!? Kapunguza nini?
- Yaani simalizi list yangu
Kusema eti tumpe muda, wa nini? Tunarudi palepale, kwa miaka 2 waandishi na baadhi ya watu pamoja na upinzani wamepiga kelele kwamba nyumba inaungua, tukajibu wapeni muda, sasa after billions of loss and poor infrastrucure and all the crap, tunashangaa how did we get there! Ni hii 'tuwape muda!"
Hii cabinet ni mbovu na ya kushikaji. Na it will not last more than 1 year!
Tuache unfaiki na ushabiki usio wa maana na tufuate aliyosema Anna Kilango, hapa si muhimu chama bali uzalendo!