Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

What about MEMBE?

GT inaonesha Muungwana siku hizi hasomi JF. Au kama anasoma anaendelea kujifanya shingo ngumu.....na kuna uwezekano kwamba mkuu anajua kuna dili la kuchezwa, ndio maana karudishwa the same wizara......
Yaani ni kama zamani, kumtoa Karamagi Viwanda na Biashara to Madini na Nishati, after miezi kadhaa ikapigwa kazi ya Buzwagi...n wakuu wote wakawa London on the same day
 
Wanyancha hatimaye kapata Unaibu ili kumzima na kelele zake za kule Mbugani Mugumu amabako wanataka kujenga Uwanja wa ndege na JK na kundi lake wamegawana vitalu na anaanza kujenga hotel na kuwapa nafasi wawekezaji .

Wait and see what is happening .

Sasa hii ni mbaya sana!!!

Mi naona kuna watu wamewekwa ili waweze kuilinda serikali, sio wananchi kama inavyotakiwa.....

Ila nasikia hiyo move ya kujenga mbugani imepigwa stop....Is it kweli??
 
Sasa hii ni mbaya sana!!!

Mi naona kuna watu wamewekwa ili waweze kuilinda serikali, sio wananchi kama inavyotakiwa.....

Ila nasikia hiyo move ya kujenga mbugani imepigwa stop....Is it kweli??

People do change, (either negatively or positively)... 1995 we had Mr. Clean...

In 2005 Mr. Clean was not the same as Mr. Clean of 1995.

So vice versa is also true... depending on Environment Both internal and external.
 
Wana JF,

Forum hii imeweza kuchambua kwa kina sana Cabinet Mpya ya Mheshimiwa Rais..Nnawaomba tuchukue hatuwa kubwa kama wa penda maendeleo kwa kufanya mambo kimaendeleo.

Nawaomba tu set standards na Goals ambazo ni Specific, Measurable, Attainable(Achievable), Realistic(Results-oriented), Tangible(Timely)

S.M.A.R.T Analysis itakuwa ni kioo kizuri kwa waheshimiwa na hata sisi Wadau wa JF...Ila Tukianza kusema huyu kafanya nini bila kuwa na specific standards mijadala yetu haitakuwa na mafanikio.
 
As for losing a job he has held for 18 years, he said, "The integrity of my eternal soul is infinitely more valuable than a pathetic political career."

Sijui kama hapa ni mahali pake lakini nimeisoma leo. Ni quotation kutoka kwa Republican Rep. Wayne Gilchrest kutoka Maryland aliyeshindwa kwenye primaries huko marekani. Hivi wanasiasa wetu wanaweza kusema hivi? Ku'walk' away from a political career kutokana na principles zake na kukataa kucompromise integrity yake? Tumegeukaje a nation of sycophants?
 
Mkullo!!!!! Naikumbuka siku nilipojikuta nae meza moja kwenye function iliyoshirikisha wizara ya utalii wakiwa chini Mama yao Megji wakati ule, yeye (mkullo)na rafiki yake aliyepewa ukatibu mkuu kwa kipindi kifupi na kisha kutupwa mkoani walikuwa wanapeana namba za Vishoka ili wa - by pass umeme majumbani kwao!!! Leo ni Waziri tena wa Fedha! Pathetic!!! Kilichotushangaza mimi na wenzangu tuliokaa nao ni kwamba hata hawakuwa wanatufahamu wakadhubutu kuongelea haya mbele yetu. Tumekwisha!

Kwa vile Kiswahili changu ni cha zamani kidogo, naomba tafsiri ya hayo niliyoyapaka rangi! Uniwie radhi lakini. Utu uzima tu.
 
Kwa vile Kiswahili changu ni cha zamani kidogo, naomba tafsiri ya hayo niliyoyapaka rangi! Uniwie radhi lakini. Utu uzima tu.

Vishoka= Hawa ni watu ama walikuwa wakifanya kazi TANESCO zamani, ama wana ujuzi na mambo ya umeme, hupita majumbani kwa makubaliano ya malipo ya kifisadi, hupindisha njia ya umeme, ili isipitie kwenye mita yako, kiasi kwamba unalipa kidogo sana kulingana na matumizi yako!

Kwa lugha nyingine, hawa ni wataalamu wa umeme ambao hushirikiana na wateja kuihujumu TANESCO !!
 
Sijui kama hapa ni mahali pake lakini nimeisoma leo. Ni quotation kutoka kwa Republican Rep. Wayne Gilchrest kutoka Maryland aliyeshindwa kwenye primaries huko marekani. Hivi wanasiasa wetu wanaweza kusema hivi? Ku'walk' away from a political career kutokana na principles zake na kukataa kucompromise integrity yake? Tumegeukaje a nation of sycophants?

Hiyo inafanana na hadithi ya tumbili alipozikosa zabibu, akasema aah zabibu zenyewe kwanza ni mbichi.
 
Quote:- Concord

Wana JF,

Forum hii imeweza kuchambua kwa kina sana Cabinet Mpya ya Mheshimiwa Rais..Nnawaomba tuchukue hatuwa kubwa kama wa penda maendeleo kwa kufanya mambo kimaendeleo.

Nawaomba tu set standards na Goals ambazo ni Specific, Measurable, Attainable(Achievable), Realistic(Results-oriented), Tangible(Timely)

S.M.A.R.T Analysis itakuwa ni kioo kizuri kwa waheshimiwa na hata sisi Wadau wa JF...Ila Tukianza kusema huyu kafanya nini bila kuwa na specific standards mijadala yetu haitakuwa na mafanikio.

Maneno mazito Concord haya......!
 
Maneno mazito Concord haya......!

Thanks Field Marshall

Ili kuwa na hoja yenye nguvu inabidi tuwe na viwango vinavyoeleweka.kulalamika tu hata kama ni ya kweli watu wanaweza kuona ni majungu.

Pia tuwe fair kwa hawa viongozi na watakapofanya kazi nzuri tuwasifu pia na kwa standards tulizoweka wakikosea itakuwa rahisi kuwakosoa otherwise tutaonekana tunpiga majungu tu.

Wapo watakaosema tuwasifu kwa nini wakati hii ni kai zao.Mimi nnaamini hio ni njia nzuri ya motivation.

Let us have STANDARDS & GOALS
 
Hiyo inafanana na hadithi ya tumbili alipozikosa zabibu, akasema aah zabibu zenyewe kwanza ni mbichi.

Hivi tumekuwa cynical kiasi hicho! Hatuamini kabisa kuwa kuna mtu anaweza akakataa ku'compromise' kutokana na principles zake? Kasome kwanza habari za huyu jamaa ndio u'comment'.
 
Vishoka= Hawa ni watu ama walikuwa wakifanya kazi TANESCO zamani, ama wana ujuzi na mambo ya umeme, hupita majumbani kwa makubaliano ya malipo ya kifisadi, hupindisha njia ya umeme, ili isipitie kwenye mita yako, kiasi kwamba unalipa kidogo sana kulingana na matumizi yako!

Kwa lugha nyingine, hawa ni wataalamu wa umeme ambao hushirikiana na wateja kuihujumu TANESCO !!

Twafa basi kama ni kweli aliyosema Mkuu Liz Senior!
 
UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI

Hoja walizotoa Lunyungu, Katibutarafa, Jokakuu, Chuma na Kamanda haziwezi kupita bila kutolewa maoni.

Kama tungewataka Watanzania watoe mapendekezo juu ya baraza la Mawaziri linalotakiwa, yangetolewa mapendekezo mengi yanayotofautiana kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa Rais ndiye mwenye jukumu la kuliteua baraza hilo, tukubaliane na baraza aliloliteua, huku tukiangalia mwenendo wake kiutendaji ndipo tutoe maoni yetu.

Kulihukumu baraza hilo kuwa halifai kabla hata halijaanza kazi ni kutomtendea haki Rais mwenyewe na Baraza aliloliteua. Rais alieleza wazi baada ya kuliapisha, kwamba linatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na bidii ya hali ya juu, vinginevyo hatasita kulivunja tena. Ni vizuri basi tulipe muda Baraza hili jipya ili kupima utendaji wake kabla hatujalihukumu.

Rais amepewa dhamana ya kuteua Baraza la Mawaziri kwa niaba yetu na amejiridhisha kwamba kikosi cha mawaziri hawa kitampa msaada. Basi ni vyema tukamwamini kuwa ana nia njema na nchi yetu.
 
Baraza la Mawaziri lina miezi miwili tu, mwingine kishaibuliwa kwa ufisadi katika deal ya rada. Muungwana itabidi apangue tena timu! Sijui mpaka 2010 atapanga baraza la mawaziri mara ngapi! maana wengi anaowateua ni mafisadi.
 
Bubu, inaitwa "trial and error" ndugu yangu..... Lakini uzuri Muungwana alishatuambia kwamba tusishangae akibadili tena na tena na tena ili kufanikisha/kuongeza ufanisi!?!#*&^@#

Kaaz kweli kweli............
 
Jamani Chenge hawezi kutolewa baraza la mawaziri, JK alitudanganya aliposema hana ubia na mtu yeyote, lakini sasa inaonekana wazi ana ubia na Andrew Chenge, watu walipiga kelele kwa sababu walimjua sana kabla ya deal la rada kufumka JK kanyamaza kimya sasa hivi najua kabisa hawezi kufanya chochote na jamaa ataendelea kula pesa ya barabara bila tatizo lolote.
 
Imedhihirika kuwa chenge si tu ni mbia katika serikali hiyo, lakini ana stake kubwa kuliko hata JK mwenyewe, chenge ni majority share holder katika serikali kwa sababu deal karibu zote za ulaji alizichonga na kuzifanikisha yeye, anajua siri nyingi sana kiasi kwamba anaweza kumwangusha yeyote katika serikali
 
MN, nimeiona point yako lakini sitashangaa kama "Tembo akauwawa kwa ubua (tena mkavu)".......

Hiki kitendawili hiki nadhani sasa kimeshapata jibu na Muungwana analijua lakini tatizo ni namna ya kuanza.... Tunaendelea kungoja kama ilivyosema ile Tume ya Mwakyembe kwenye Rich...... "Mkuu ataamua mwenye cha kufanya baada ya kuangalia uzito wa jambo lenyewe,.........."
 
Back
Top Bottom