Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Is True kwamba Mathayo David ni mtoto wa nje wa Msuya?

Kwamba huyu jamaa PhD yake ni Fake nilisha wahi zipata sehemu lakini sikuwa na uhakika.

Kwa nini watu waliofoji Elimu Vihiyo wakubwa wankubalika serikalini?

Hii kweli ni serikali ya wasanii.

Huyu Mama mke wa mtu na adabu zake zote alikuwa akimvulia kaptula Rais mstaafu Ben Mkapa.

Halafu nikisema umalaya ni hatari kwa maendeleo ya taifa watu mnabisha na kwa uchungu mnataka hata kula nyembe mpya na sime za kimasai.

Umalaya wa viongozi wetu unatugharimu mamilioni.
Viongozi wetu wanatumia kuni zao vibaya matokeo yake wote tunabebeshwa gharama.

MKO WAPI FIELD MARSHALL NA MWAFRIKA WA KIKE? MMEUONA HUO MTUNDIKO HAPO JUU?
 
Ukiacha hiyo data aliyokupa YN, sisi tuna PhD holders wengi kuliko wao, tuna academic journals nyingi kuliko wao, tupo cited zaidi kwenye international journals kuliko wao, our standing in intenational academic fora ipo juu kuliko wao, tuna mitaala bora kuliko wao, you mention every aspect of quality higher education tunawazidi. Unapokuja kwenye academics kupata kazi katika international scientific organisations sisi tupo juu, ndio hao akina Tibaijuka, Mgongo, Lipumba et al wanatuwakilisha. Isipokuwa inapokuja kwenye kazi za kupitia mlango wa nyuma tupo nyuma kwa sababu watanzania sio kasumba yetu kutafuta vitu ambavyo hatuna sifa nazo.

You confirm my suspicions, sir. Inaelekea chuo hicho kiko top-heavy. Sifa zote zinahusu wakufunzi ambayo si lazima i'translate' kwenye elimu bora kwa wanafunzi. Bado nina wasiwasi na elimu inayotolewa na quality ya wanafunzi wanaotoka hapo. Itakuwaje mtu akiri kuwa kiingereza kinapiga chenga halafu akadai kuwa ni wakali katika kupanga mada katika mikutano ya kimataifa! Mafaniko ya hao wakina Tibaijuka n.k. yasitubweteshe maana hata wakenya na waganda wako wengi kwenye sehemu hizo. Si fair kudai kuwa ati wao wanatafuta kazi kwa kupitia mlango wa nyuma (Mbona hata sisi hizi nafasi hazitegemei shule tu bali na siasa). Wao wamezoea ushindani na kujiuza kitu ambacho sisi hatuna.

Tusipende sifa zisizo na maana (mfano ni the Noble prize that never was). Tusijivunie hao walio katika hizo international scientific institutions ambao pengine ni msasa waliopewa huko walikoenda kusomea hizo post-grad. ndiyo zimewapandisha chati bali tuangalie hao wanafunzi wetu tunaowatoa! Kweli tuna haki ya kujivunia kiasi hiki?

Kuna kijana wangu anasoma mlimani na hali anayoisimulia si hii ambayo nyinyi ma profesa mnataka kutuambia. Anazungumzia lack of basic resourses kama vitabu (naam, vitabu bado vinahitajika hata katika karne hii ya Google), madarasa yaliyo jaa kupita kiasi na kibaya zaidi walimu ambao hawana mpango nao maana wako busy na mambo yao! Walimu wanaotaka watambulike kuwa wao ndio waliosoma na hawana msukumo wa kuwaelimisha wanafunzi wao. Hatua tumepiga lakini bado safari ni ndefu. Huu si wakati wakupongezana bali ni wakati wa kukumbushana tunakotakiwa kwenda. Hatuwachukii lakini kuna haja ya kuwa na reality check.

Ni hayo tu, wakuu. Haya na turudi kwenye mada.
 
Fundi:
I am talking from practical experience, having been a receipient of the Univ. of Dar; and having a wide ranging educational exposure, both as student and educator/researcher at various international western institutions; and, having worked/taught people from our region; our Univ. of Dar. ni lulu ya kipekee. Tusijirudishe nyuma mahali ambapo kweli tunang'ara. Tatizo lilikuja tu wakati mahitaji ya vifaa/chemikali za kufundishia mambo ya kisayansi yalipoanza kuwa adimu, hasa huko katika shule za sekondari. Lakini elimu ya chuo kikuu chetu bado ni nzuri kabisa, lack of facilities notwithstanding.
 
Koba, unachobisha ni kipi hasa? Mfano mdogo ameshakupa YN, sasa unataka nini tena? Evidence is always both qualitatively and quantitatively attribiutable! Sisi tuliopo katika career hii ya elimu ya juu tunajua na wenzetu wakenya na waganda wanajua hivyo kwamba sisi kwenye mambo ya academics tupo juu. Na hapa sisi tunaongelea ubora wa elimu, sio wingi. Kwa wingi ni sawa wametuzidi kama vile ambavyo wametuzidi kila kitu katika wingi isipokuwa idadi ya watu. Ukiacha hiyo data aliyokupa YN, sisi tuna PhD holders wengi kuliko wao, tuna academic journals nyingi kuliko wao, tupo cited zaidi kwenye international journals kuliko wao, our standing in intenational academic fora ipo juu kuliko wao, tuna mitaala bora kuliko wao, you mention every aspect of quality higher education tunawazidi. Unapokuja kwenye academics kupata kazi katika international scientific organisations sisi tupo juu, ndio hao akina Tibaijuka, Mgongo, Lipumba et al wanatuwakilisha. Isipokuwa inapokuja kwenye kazi za kupitia mlango wa nyuma tupo nyuma kwa sababu watanzania sio kasumba yetu kutafuta vitu ambavyo hatuna sifa nazo. Sasa wewe umeng'ang'ania idadi ya mavyuo, wenzako wanapopima ubora wa vyuo hawahesabu idadi ya vyuo wanaangalia quality, na quality inapimwa kwa knowledge production and intellectual contribution-na hivi vitu vinaangaliwa kwa vigezo kama vya hapo juu.

Ni kweli watz tu wanyonge katika mambo kibao, lakini sio hili la ubora wa elimu ya juu, hili hapana. Pale tunapofanya vizuri kidogo tusisite kusema na kujipongeza. Waswahili wanasema "You cannot be inferior unless you feel that you are inferior"!

...naona sasa unataka kufanya something simple more complex,unaleta mifano ya ajira za kina Lipumba & Tibaijuka kama quality of our education,na sijui una maana gani na intellectual contribution huku hakuna hata paper/research ya UD imekuwa published in any respected journals i know,za wakenya zimejaa kila kona na ukitaka nitakuonyesha,anyway i dont see this kind of discussion/debate ikitupeleka popote or benefit anybody,i respect your opinions/fact mkuu lakini lets just agree to disagree,na dont get me wrong labda ufikiri i dont respect or appreciate the intergrity of our academic institution...i do!
 
Ifuatayo ndiyo orodha sahihi ya Baraza la Mawaziri na Majina Sahihi ya Wizara zao.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NI:

1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA SOFIA) - Sophia SIMBA

2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA

3. WIZARA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SHUGHULI ZA MUUNGANO) MOHAMED SEIF KHATIB

4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI
5. WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA NA URATIBU WA BUNGE) WAZIRI PHILIP MARMO

6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA WAZIRI STEVEN WASSIRA NAIBU SELINA KOMBANI

7. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAZIRI MUSTAFA MKURO NA

MANAIBU NI JEREMIH SUMARI NA OMARI YUSUF MZEE

8. WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAZIRI PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA

9. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WAZIRI JOHN CHILIGATI

10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WAZIRI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE NAIBU GAUDENSIA KABAKA NA MWANTUMU MAHIZA

11. WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAZIRI SHUKURU KAWAMBWA NAIBU NI DK. MAUA DAFTARI

12. WIZARA YA MIUNDO MBINU WAZIRI ANDREW CHENGE NAIBU DK. MAKONGORO MAHANGA

13. WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO WAZIRI KAPT. GEORGE MKUCHIKA NAIBU JOEL BENDERA

14. WIZARA YA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA WAZIRI PROFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE

15. WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI WAZIRI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU ENG. CHRISTOPHER CHIZA

16. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA, USHIRIKA WAZIRI PROF. PETER MSOLLA, NAIBU DR. MATHAYO DAVID MATHAYO

17. WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO WAZIRI MARGARETH SITTA NAIBU NI DR. LUCY NKYA

18. WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI WAZIRI JOHN POMBE MAGHUFULI NAIBU JAMES WANYANJA

19. MALIASILI NA UTALII WAZIRI NI SHAMSA MWANGUGA NAIBU EZEKIEL MAIGE
20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI DR. LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI

21. WIZARA YA MAMBO YA NJE USHIRKIANO WA KIMATAIFA WAZIRI NI BENARD MEMBE NAIBU SEIF ALI IDDI

22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAZIRI WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA

23. WIZARA YA SHERIA NA KATIBA MH. MATHIAS CHIKAWE

24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NA NAIBU EMMANUEL NCHIMBI

25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. DEODATUS KAMALA

26. WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI

Naomba ufafanuzi kwenye rangi nyekundu
 
Baraza kwa ujumla wake naona bado, matarajio tuliyonayo ni makubwa zaidi, lakini naona hii ni hatua, ni bora kuliko la awali. Kama ni mwanafunzi alikuwa kwenye F sasa kasogea kwenye D (tunataka A au angalao hata B basi).

Lakini sikubaliani na suala la kumhukumu mtu kutokana na umri pekee. Kuna ushahidi gani kuwa mtu akiwa na umri mdogo hawezi kuwa waziri wa ulinzi? Salim Ahmed Salim alipoteuliwa kuwa waziri wa ulinzi mwaka 1985 alikuwa na umri wa miaka 40, je huu ni umri mkubwa? Umri wa Dr Hussein Mwinyi ni miaka 41. Sasa kwa nini wa miaka 41 aonekane "kijana" kwa hiyo ati "hawezi" wakati wa miaka 40 aliweza? Hata marehemu Edward Sokoine aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi miaka mwishoni ya 1970's akiwa kwenye early 30's, na alifanya kazi nzuri sana tu. Kwa nini Nchimbi mwenye late 30's ashindwe? Kumbukeni ninachopinga hapa ni hili wazo la kudai ati "vijana" hawawezi maswala ya majeshi yetu. Kuweza masuala ya majeshi hakutokani na umri, ni mengi zaidi ya hapo, tuyajadili hayo tusianze kubagua kwa msingi wa "ujana".

Mwinyi kapelekwa Ulnzi akapikwe, jiandaeni Mwinyi SMZ 2010 au 2015 Muungano!
 
Wakuu napenda kutoa heshima kwa wale members hapa ambao tumekuwa siku nzima tukihabarishana yanayojiri, na hivyo kuwepo hapa JF hata bila ya kuwepo, maana wneinge tunategmea habari zetu za taifa hapa tu JF, kwa hiyo shukrani na tuendele na hiyo tabia,

Halafu nimpongeze rais Kikwete, kwa uchaguzi wa baraza la mawaziri, ambalo kwanza tunafanana nalo sisi wananchi, na the fact kuwa wengi ambao wamehusishwa na maovu wameachwa, na mawaziri wengi tuliowazoea wameachwa, it a fair deal, ingawa pia kuna some dis-appointments pia, kama kurudi kwa Kapuya ambaye we know as a fact kwamba hali yake ki-afya sio nzuri sana, mama Nagu kuwekwa wizara ya viwanda, Sophia kwenda ofisi ya rais kwa kweli ni un-called for, lakini anyways ninampa rais the benefit of the doubt,

Niwapongeze washikaji Masha na Chikawe, kwa kupanda unga na kuwa mawaziri kamili, Mkuchika, Balozi Idd, Chiligati, Mkulu Hussein, I mean this is good politics, kwamba sasa tumeweza kuwa na wakuu wengi tunaofanana nao, na pia ninampongeza rais kwa kuwatema viongozi ambao hapa JF tumekuwa tukilia nao sana kama Meghji(BOT) & Rostam, Diallo(Aliyetumia Helikopta kwa uchaguzi wa NEC), Mramba (BOT, Radar, Ndege ya Rais), Ngasongwa(Mtandao), Rita Mlaki (Rushwa nzito NEC), Mungai (Air Tanzania Mufilis), Karamagi (Richmond, buzwagi), Msabaha (Richmond), Mwapachu (Mufilis Air Tanzania). Kwa kweli ninampongeza Rais kwa jeuri ya kuweza kuwatoa hawa viongozi incompetent, na ninaaamini kuwa amekuwa akisikia kilio chetu hapa JF.

On the other hand, ninataka kuamini kuwa rais na ccm wana mikakati imara ya kuwa-contain walioachwa, maana sasa kuna Lowassa, Karamagi, Diallo, Msabaha, Rita Mlaki, Rostam(Meghji), this people could be deadly, maana pia ninawaona Sumaye, Londa, Sykes, Mkali, Nyimbo, Kimiti, na Mzindakaya, wakijiunga nao as a political group, now that is wasup! Maana hawa ni rich na pia ni ugly politicians, ninatabiri kivumbi kizito sana in the coming days, maana tutegemee waende kulima? Wafanye biashara? Wakae bench tu? No way hosee, they are coming back tena soon, na nina-predict kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wetu wa sasa watatutumikia wananchi ipasavyo kwa mara ya kwanza toka Mwalimu, aondoke maana it is their only tool kupambana na hawa wakuu, Kikwete ataliweza hili baraza jipya maana hakuna tena wa kumtisha, ingawa bado kuna swali kubwa sana je atawezaje kupata second term bila hao wakuu aliowaacha? Ndio maana ninasema kuwa his best bet ni kututumikia vyema wananchi, and ninaamini wananchi tutapata hiyo this time arround, yaaani uongozi angalau bora,

I understand kuwa kuna some concerns, kutoka kwa baadhi ya members hapa JF, ninasema ni haki yao, lakini some times hapa JF huwa tuna-demand too much kuliko uwezo wetu bongo, kwa sababu kufanya tofauti rais ilikuwa either achukue viongozi toka upinzani, au arudishe wazee kwa sababu kama ni ccm tu, aliowachagua ni almost all we got kwa mtizamo wangu,

Sasa ninawaomba wananchi tuwape nafasi hawa mawaziri wapya watuonyeshe tofauti, kwa wale manorusha maneno mazito ambayo kwa kweli kwenye mjadala mzito wa taifa kama huuu sio mahali pake, ninawaomba mfikirie kuwa kuna wananchi wengi sana wanaokuja hapa kuchota habari za uhakika, na analysis za siasa, na wengine ni vijana wadogo, kina mama, I mean Jf ni jina kubwa sana ndugu zangu, kuliko wengi mnavyofikiri,

Mkuu Invisible na Mods, mngejaribu kupunguza lugha nyinigne ni nzito kidogo kwa wananchi wasioujua siasa, wanaojaribu kuja hapa kujifunza.

Mungu Aibariki Tanzania.
 
they are coming back tena soon, na nina-predict kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wetu wa sasa watatutumikia wananchi ipasavyo kwa mara ya kwanza toka Mwalimu, aondoke maana it is their only tool kupambana na hawa wakuu, Kikwete ataliweza hili baraza jipya maana hakuna tena wa kumtisha, ingawa bado kuna swali kubwa sana je atawezaje kupata second term bila hao wakuu aliowaacha? Ndio maana ninasema kuwa his best bet ni kututumikia vyema wananchi, and ninaamini wananchi tutapata hiyo this time arround, yaaani uongozi angalau bora,

Mkuu FMES
Umeeleweka vizuri sana. Nimekuwa nikipiga mahesbabu ya kisiasa kuangalia jibu litakuwa vipi 2010. Lakini sijaweza kupata jibu, hasa ikizingatiwa kuwa kuna NEC, kuna CC, kuna Bunge na kwenye ngazi mbalimbali za mikoa, wilaya etc. Naona kuna casualities wa CCM mtandao operations the likes of Mangula, Sumaye, na sasa naona casualties wa Richmond report, ambao kuna uwezekano mkubwa wakaenda kuunda timu itakayoanza kupambana na establishment ya sasa. Na hasa ukizingatia kuwa Tanzania kuchaguliwa kuwa rais haitokani na utendaji wako au kuwatumikia wananchi. Ukichaguliwa tu kwenye vikao vya CCM ndio umepita, na unakuwa rais wa Tanzania. This time naona vikao vijavyo vya CCM vitakuwa more interesting kuliko hata bunge, kutakuwa na makundi mawili au matatu makubwa.
Lakini naona pia kuwa unaweza kutumika ujanja wa kutowafikisha hawa jamaa wa hizi kashfa kwenye mkono wa sheria ili kununua ukimya wao. Naona kama kuna ugonjwa utafugwa ili wengine waweze kuendelea bila kusumbuliwa! Nasubiri sana hiyo come back yao, nione impact yake kwa Tanzania!
 
I mean kwa mtizamo wangu, hawa wameumizwa tena sana na washirika wenzao, kama uchaguzi wa rais 2015 ungekuwa unafanyika leo, Membe ni a big winner wa this whole thing,

Lakini nina wasi wasi kuwa as we move forward, kuwa tutajionea mengi sana, maana hawa hawaendi quitely, kuwafikisha mkono wa sheria, labda another administration siyo hii, It won't happen now, kwa sababu kuna washirika wao wengi waliobaki kwenye power,

na walioko kwenye power hawana anything cha kuwa-offer walioachwa kwa mbali ninaiona Muungwana kumuachia Lowassa urais, somehow somwhere ninaiona hiyo as the only remedy kumridhisha Lowassa, ambaye aliacha ambitions zake last elections with understanding kuwa ni zamu ya Muisilam, na ndiye aliyekuwa the creator wa Mtandao, je atashindwa kuanzisha mwingine?

Pia kuna Lukuvi, ambaye naye hajaridhika, kabisa halafu kuna Kitwana Kondo, hapa naye ameumizwa na hii change, tatizo kubwa kuliko ni kwamba hawa wakuu walioachwa ni wabunge, kwa hiyo hawawezi kupewa ubalozi, ambayo ndio ilikuwa the best alternative kwa Muungwana, kuwa-neutralize, ninawaona wakiwaweka vibaraka wao mbele, na baadaye kuibuka wenyewe mbele, kuingia upinzani hawawezi, maana watageuka kama kina Akwilombe na Hiza,

Ninawaona wakileta sokomoko ndani ya ccm, I wish sisi wananchi ndio tungekuwa the beneficiary wa hilo sokomoko!
 
they are coming back tena soon, na nina-predict kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wetu wa sasa watatutumikia wananchi ipasavyo kwa mara ya kwanza toka Mwalimu, aondoke maana it is their only tool kupambana na hawa wakuu, Kikwete ataliweza hili baraza jipya maana hakuna tena wa kumtisha, ingawa bado kuna swali kubwa sana je atawezaje kupata second term bila hao wakuu aliowaacha? Ndio maana ninasema kuwa his best bet ni kututumikia vyema wananchi, and ninaamini wananchi tutapata hiyo this time arround, yaaani uongozi angalau bora,

Mkuu FMES
Umeeleweka vizuri sana. Nimekuwa nikipiga mahesbabu ya kisiasa kuangalia jibu litakuwa vipi 2010. Lakini sijaweza kupata jibu, hasa ikizingatiwa kuwa kuna NEC, kuna CC, kuna Bunge na kwenye ngazi mbalimbali za mikoa, wilaya etc. Naona kuna casualities wa CCM mtandao operations the likes of Mangula, Sumaye, na sasa naona casualties wa Richmond report, ambao kuna uwezekano mkubwa wakaenda kuunda timu itakayoanza kupambana na establishment ya sasa. Na hasa ukizingatia kuwa Tanzania kuchaguliwa kuwa rais haitokani na utendaji wako au kuwatumikia wananchi. Ukichaguliwa tu kwenye vikao vya CCM ndio umepita, na unakuwa rais wa Tanzania. This time naona vikao vijavyo vya CCM vitakuwa more interesting kuliko hata bunge, kutakuwa na makundi mawili au matatu makubwa.
Lakini naona pia kuwa unaweza kutumika ujanja wa kutowafikisha hawa jamaa wa hizi kashfa kwenye mkono wa sheria ili kununua ukimya wao. Naona kama kuna ugonjwa utafugwa ili wengine waweze kuendelea bila kusumbuliwa! Nasubiri sana hiyo come back yao, nione impact yake kwa Tanzania!

BongoLander:

Kuna vitu vya kujifunza katika wiki mbili zilizopita. Kwanza tuachane na siasa za UBUNTU. Siasa za UBUNTU zinasema inachukua kijiji kulea mtoto. Siku zote nilikuwa nasubiri watanzania wengi wapate kuamka hili mabadiliko ya maana yatokee. Kama wabunge wachache wa upinzani wanaweza kusimama bungeni na kuleta mabadiliko kwa kutumia taarifa zinazopatikana JF na vyanzo vingine inaonyesha kabisa hatuitaji kijiji kulea mtoto. Mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko.

Kitu kingine muhimu ni kutosubiri mabadiliko ya kipindi cha uchaguzi. Good Ridance isisisubiri wakati wa vipindi vya uchaguzi. Watu wabakie kwenye mashambuli hata kama viongozi wanafanya vizuri. Tabia za kufanya kazi kwa manufaa ya taifa hazijaingia damuni kwa wengi wetu.
 
On the other hand, ninataka kuamini kuwa rais na ccm wana mikakati imara ya kuwa-contain walioachwa, maana sasa kuna Lowassa, Karamagi, Diallo, Msabaha, Rita Mlaki, Rostam(Meghji), this people could be deadly, maana pia ninawaona Sumaye, Londa, Sykes, Mkali, Nyimbo, Kimiti, na Mzindakaya, wakijiunga nao as a political group, now that is wasup! Maana hawa ni rich na pia ni ugly politicians, ninatabiri kivumbi kizito sana in the coming days, maana tutegemee waende kulima? Wafanye biashara? Wakae bench tu? No way hosee, they are coming back tena soon,

FM...no chance no chance kwa hawa mafisadi and they will never come back labda kama hawajipendi si unajua kesi zao ziko pending na hazijaisha wala kufunguliwa,utasikia tuu wakifungua mdomo watafanywa kama Zuma,lakini wakirudi na wakakubalika na wananchi utabiri wa Nyerere utatimia..wapinzani watatoka CCM ingawaje is a long shot kwa hawa uliowataja,labda utupe scenario ya namna wanavyoweza kurudi!
 
Wakuu napenda kutoa heshima kwa wale members hapa ambao tumekuwa siku nzima tukihabarishana yanayojiri, na hivyo kuwepo hapa JF hata bila ya kuwepo, maana wneinge tunategmea habari zetu za taifa hapa tu JF, kwa hiyo shukrani na tuendele na hiyo tabia,

Halafu nimpongeze rais Kikwete, kwa uchaguzi wa baraza la mawaziri, ambalo kwanza tunafanana nalo sisi wananchi, na the fact kuwa wengi ambao wamehusishwa na maovu wameachwa, na mawaziri wengi tuliowazoea wameachwa, it a fair deal, ingawa pia kuna some dis-appointments pia, kama kurudi kwa Kapuya ambaye we know as a fact kwamba hali yake ki-afya sio nzuri sana, mama Nagu kuwekwa wizara ya viwanda, Sophia kwenda ofisi ya rais kwa kweli ni un-called for, lakini anyways ninampa rais the benefit of the doubt,

Niwapongeze washikaji Masha na Chikawe, kwa kupanda unga na kuwa mawaziri kamili, Mkuchika, Balozi Idd, Chiligati, Mkulu Hussein, I mean this is good politics, kwamba sasa tumeweza kuwa na wakuu wengi tunaofanana nao, na pia ninampongeza rais kwa kuwatema viongozi ambao hapa JF tumekuwa tukilia nao sana kama Meghji(BOT) & Rostam, Diallo(Aliyetumia Helikopta kwa uchaguzi wa NEC), Mramba (BOT, Radar, Ndege ya Rais), Ngasongwa(Mtandao), Rita Mlaki (Rushwa nzito NEC), Mungai (Air Tanzania Mufilis), Karamagi (Richmond, buzwagi), Msabaha (Richmond), Mwapachu (Mufilis Air Tanzania). Kwa kweli ninampongeza Rais kwa jeuri ya kuweza kuwatoa hawa viongozi incompetent, na ninaaamini kuwa amekuwa akisikia kilio chetu hapa JF.

On the other hand, ninataka kuamini kuwa rais na ccm wana mikakati imara ya kuwa-contain walioachwa, maana sasa kuna Lowassa, Karamagi, Diallo, Msabaha, Rita Mlaki, Rostam(Meghji), this people could be deadly, maana pia ninawaona Sumaye, Londa, Sykes, Mkali, Nyimbo, Kimiti, na Mzindakaya, wakijiunga nao as a political group, now that is wasup! Maana hawa ni rich na pia ni ugly politicians, ninatabiri kivumbi kizito sana in the coming days, maana tutegemee waende kulima? Wafanye biashara? Wakae bench tu? No way hosee, they are coming back tena soon, na nina-predict kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wetu wa sasa watatutumikia wananchi ipasavyo kwa mara ya kwanza toka Mwalimu, aondoke maana it is their only tool kupambana na hawa wakuu, Kikwete ataliweza hili baraza jipya maana hakuna tena wa kumtisha, ingawa bado kuna swali kubwa sana je atawezaje kupata second term bila hao wakuu aliowaacha? Ndio maana ninasema kuwa his best bet ni kututumikia vyema wananchi, and ninaamini wananchi tutapata hiyo this time arround, yaaani uongozi angalau bora,

I understand kuwa kuna some concerns, kutoka kwa baadhi ya members hapa JF, ninasema ni haki yao, lakini some times hapa JF huwa tuna-demand too much kuliko uwezo wetu bongo, kwa sababu kufanya tofauti rais ilikuwa either achukue viongozi toka upinzani, au arudishe wazee kwa sababu kama ni ccm tu, aliowachagua ni almost all we got kwa mtizamo wangu,

Sasa ninawaomba wananchi tuwape nafasi hawa mawaziri wapya watuonyeshe tofauti, kwa wale manorusha maneno mazito ambayo kwa kweli kwenye mjadala mzito wa taifa kama huuu sio mahali pake, ninawaomba mfikirie kuwa kuna wananchi wengi sana wanaokuja hapa kuchota habari za uhakika, na analysis za siasa, na wengine ni vijana wadogo, kina mama, I mean Jf ni jina kubwa sana ndugu zangu, kuliko wengi mnavyofikiri,

Mkuu Invisible na Mods, mngejaribu kupunguza lugha nyinigne ni nzito kidogo kwa wananchi wasioujua siasa, wanaojaribu kuja hapa kujifunza.

Mungu Aibariki Tanzania.

Mkuu, wengi wa hao uliowataja ni mafisadi hawana chao tena na hawakubaliki na umma wa walio wengi wa Watanzania. Kama wananchi watawapa tena nafasi ya kurudi kwenye anga za siasa basi hakuna wa kulaumiwa bali ni umma wa Watanzania ambao utakuwa umethibitisha tena kwamba kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.
 
Baraza sio baya kiasi hicho. Wapeni muda, yapa matatizo ya kuwa na Chenge , Kapuya, Simba Sophia kweli zinakera ila jamani ni wachache. Wengi tumefurahia mabadiliko.

Nimefurahi sana kuona vijana wanapanda na wengine wapya kujitokeza!

Al in all HONGERA JK!
 
Sasa wewe umewahi kuona wapi unajilinganisha na wagonjwa wenzako ambao wanaumwa zaidi. Sisi ndio tunaongoza kwa elimu ya juu East Africa halafu unataka kutulinganisha na waganda na wakenya! Haya tuwaambie ile report iliyoletekeza wizara hizi mbili kutenganishwa nini leo kimepungua au kuongeza kiasi kwamba tunarudi miaka 1980? Unaongelea Naibu Waziri, hujui kama mtu kama huyo hata kwenye mikutano ya cabinet haingii? Ninaelewa vizuri sana maana ya elimu na elimu ya juu na ninaongea hili with great intellectual authority wala sihitaji kusubiri maelezo ya ziada ya JK ili kuelewa!

Ukweli ni kwamba science/techology huwezi kuvitenganisha na elimu ya juu sababu shina la sci/tech ni elimu ya juu.

Hapo ni sawa kabisa na kumtenganisha samaki na maji
 
muungwana naye,wakati anaingia kutaja baraza jipya,akamgusa binti mmoja begani..nadhani mliiona hiyo
 
JK hayuko serious jamani hivi huyu Chenge shida zote hizo alizotusababishia bado yumo tuuuuuuu? Tatizo hatuna watu au ana siri kubwa ya JK????!!?-JK ni kituko kwa kweli wala si uongo.Message ninayoipata hapa ni kwamba tusitarajie la maana lolote kutoka kwenye uchunguzi wa BOT (meremeta, tangold, epa n.k) na hakuna la maana pia toka kwenye ile kamati ya kisanii aliyounda ya mikataba ya madini.

Halafu pia hivi wizara nyeti kama nishati na madini unampaje Ngeleja na naibu Malima? Simfahamu sana Ngeleja lakini kwa bahati kidogo namfahamu Malima, huyu jamani pasipo kuunyaunya maneno ni KIAZI CHA KUTOSHA AU KWA MANENO MENGINE NI ZERO KUBWA jamani.
 
Frankly speaking nimekelwa na kubaki kwa Chenge na Kapuya anyway labda watajirudi.May the lord enlighten them so that they may accomplish their tactical and strategic tasks for the interest of the nation and not otherwise.
 
Heshima mbele.....

Kweli naona mjadala umeanza kwa kasi kubwa kweli kweli..... Kama nilivyosema kule mwanzoni, unajua hawa jamaa wengi watakuwa tayari ku-prove a point (wakiwemo kina Masha, Chenge, Mkullo nk) na kuna ambao wote tunajua watakuwa ndani na kujitutumua kuonyesha makucha yao (Malima, Nkya nk)!! Ni kweli kwamba wote wana makosa yao, ule ukweli kwangu ni kwamba kila Mbunge wa CCM aliyepo madarakani leo (MP wote) kwa njia moja au nyingine alitoa rushwa wakati wa kampeni (though I can bet my life in it, I still stand to be corrected - but I will die trying to stand for this). Hivyo mimi kwa sasa since political side of the govt (Ministers and Deputies) wameshawekwa, nangojea Muungwana akituwekea Makatibu wakuu na Wakurugenzi.

Kwangu although Waziri/Deputy anachangia sana katika ufanisi/utendaji wa Wizara, Katibu Mkuu ndiye ambaye amekamata mpini!!! Kwa mawazo yangu (I stand to be corrected on this) ni kwamba kwa kweli kwenye wizara nyingi ambazo zipo goigoi ni maPS ndio wanalete rongorongo..... Mifano ya haraka ni pale Fedha, Viwanda n Biashara, Energy, Afya, Miundombinu zamani, Elimu ya Juu etc..... Kwa muangalio wa haraka haraka nilichogundua ni kwamba most of these posts tumewapa "non-professionals in the field"... Hii imekuwa more political!!

Hili linanirudisha pale kwenye issue ya "Civil Service Reform" by Mama Ghasia (nadhani wengi tunakumbuka......

For argument sake naomba niseme kwamba Baraza tumepata na sio kubwa na pana lakini kuna some signs of light at the end of the tunnel. Kina Chenge msiwe na wasiwasi nao manake kule kuna issues tulisema tutaanza kuzishughulikia baada ya kumaliza Richmon....., EPA; nazo sio nyingine bali ni MIKATABA YA UJENZI WA BARABARA!!!!

Wahenga walisema "You can fool somepeople sometimes but you cant fool all the people all the time"......... Pia tukumbuke hakuna mwezi wala mwaka wa Sundays!! Allow them to work wakichemka tutalia nao!!!

Mungu Ibariki Tanzania!!
 
Habari wana JF!
Hofu ya fulani tukimpa nafasi atatufunika ndo inaharibu maendelao ya Tanzania. Watu wazuri wapo wa kupewa wizara nyeti lakini hawapewi maana wata perform vizuri na kujinyakulia umaarufu ndani ya Chama Chao Maarufu na kwa wananci pia. Hakuna seriousness, kubebana ndo kitu kilicho tufikisha hapa, na bado tunazidi kuimarisha hako ka mfumo hasi. Kama kawaida yetu, tuwape mda. Hiki ni kipimo cha umakinifu wao lakini kipimo pia kwa wapiga kura. Majibu yatapatika soon!

Kaka K
 
Back
Top Bottom