What about MEMBE?
Wanyancha hatimaye kapata Unaibu ili kumzima na kelele zake za kule Mbugani Mugumu amabako wanataka kujenga Uwanja wa ndege na JK na kundi lake wamegawana vitalu na anaanza kujenga hotel na kuwapa nafasi wawekezaji .
Wait and see what is happening .
Sasa hii ni mbaya sana!!!
Mi naona kuna watu wamewekwa ili waweze kuilinda serikali, sio wananchi kama inavyotakiwa.....
Ila nasikia hiyo move ya kujenga mbugani imepigwa stop....Is it kweli??
As for losing a job he has held for 18 years, he said, "The integrity of my eternal soul is infinitely more valuable than a pathetic political career."
Mkullo!!!!! Naikumbuka siku nilipojikuta nae meza moja kwenye function iliyoshirikisha wizara ya utalii wakiwa chini Mama yao Megji wakati ule, yeye (mkullo)na rafiki yake aliyepewa ukatibu mkuu kwa kipindi kifupi na kisha kutupwa mkoani walikuwa wanapeana namba za Vishoka ili wa - by pass umeme majumbani kwao!!! Leo ni Waziri tena wa Fedha! Pathetic!!! Kilichotushangaza mimi na wenzangu tuliokaa nao ni kwamba hata hawakuwa wanatufahamu wakadhubutu kuongelea haya mbele yetu. Tumekwisha!
Kwa vile Kiswahili changu ni cha zamani kidogo, naomba tafsiri ya hayo niliyoyapaka rangi! Uniwie radhi lakini. Utu uzima tu.
Sijui kama hapa ni mahali pake lakini nimeisoma leo. Ni quotation kutoka kwa Republican Rep. Wayne Gilchrest kutoka Maryland aliyeshindwa kwenye primaries huko marekani. Hivi wanasiasa wetu wanaweza kusema hivi? Ku'walk' away from a political career kutokana na principles zake na kukataa kucompromise integrity yake? Tumegeukaje a nation of sycophants?
Quote:- Concord
Wana JF,
Forum hii imeweza kuchambua kwa kina sana Cabinet Mpya ya Mheshimiwa Rais..Nnawaomba tuchukue hatuwa kubwa kama wa penda maendeleo kwa kufanya mambo kimaendeleo.
Nawaomba tu set standards na Goals ambazo ni Specific, Measurable, Attainable(Achievable), Realistic(Results-oriented), Tangible(Timely)
S.M.A.R.T Analysis itakuwa ni kioo kizuri kwa waheshimiwa na hata sisi Wadau wa JF...Ila Tukianza kusema huyu kafanya nini bila kuwa na specific standards mijadala yetu haitakuwa na mafanikio.
Maneno mazito Concord haya......!
Hiyo inafanana na hadithi ya tumbili alipozikosa zabibu, akasema aah zabibu zenyewe kwanza ni mbichi.
Vishoka= Hawa ni watu ama walikuwa wakifanya kazi TANESCO zamani, ama wana ujuzi na mambo ya umeme, hupita majumbani kwa makubaliano ya malipo ya kifisadi, hupindisha njia ya umeme, ili isipitie kwenye mita yako, kiasi kwamba unalipa kidogo sana kulingana na matumizi yako!
Kwa lugha nyingine, hawa ni wataalamu wa umeme ambao hushirikiana na wateja kuihujumu TANESCO !!
Vipi makatibu wakuu?
Imedhihirika kuwa chenge si tu ni mbia katika serikali hiyo, lakini ana stake kubwa kuliko hata JK mwenyewe, chenge ni majority share holder katika serikali kwa sababu deal karibu zote za ulaji alizichonga na kuzifanikisha yeye, anajua siri nyingi sana kiasi kwamba anaweza kumwangusha yeyote katika serikali