Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Jamani eeeeee sie tusubiri tu tusimlaumu sana jk.mi nadhani huyu chenge anayo ya kujibu mengi sana baada ya akina zitto nao kuwasilisha ripoti ya madini sie tusubiri..atajiuzulu mwenyewe kama akina karamagi.Yeye si ndio alikuwa mwanasheria mkuu kabla ya mwanyika ?
 
Well lets see how bad this one can be, however kuna nafuu fulani ndogo hivi!!
 
Mkullo kuwa Waziri wa Fedha imeni dissapoint kweli?
 


Kwa mtaji huu. Itabidi watu msiache kupiga kelele hata kama rais anafanya vizuri.
 
Kwa mtaji huu. Itabidi watu msiache kupiga kelele hata kama rais anafanya vizuri.

Bahati mbaya kwako wewe uliyekata tamaa. Wengine wetu tunataka kukata hii circle ya kushindwa na kuanza the whole new dimension ya kufikiri na kuamua.

Usikate tamaa mkuu. Futures zinaweza kubadilishwa tu na vizazi vilivyopo na vinavyokuja na sio vilivyopita.
 
Ndoto yangu ilikuwa wizara 15; na manaibu 10. Jumla ya baraza lote 25. Niliandika hili mahali fulani. Niliandika pia kwamba hali halisi itakuwa mawaziri 40+. Ndivyo ilivyotokea.

Mwanakijiji bila shaka hutakosa cha kuandika mwaka huu pia.

Swali la kipuuzi: Hivi uchawi na wachawi wana nafasi gani katika serikali ya JK?
 
Eti Mkullo Waziri wa Fedha?

Huyu Mzee ni mmoja wa vihiyo waliochukua shahada za kununua, alikuwa anakimbizana nasisi kugombea vikina Olivia vya JKT Mgulani, vitoto sawa au vidogo zaidi kuliko wanawe.Mzee kamputa mchizi wangu demu hivi hivi, integrity less than zero, yaani mara mia ya Meghji kulko Mkullo.

Huyu si ndiye aliyepitisha mikopo isiyo collateral ya Sumaye? Au siye huyu? Sasa tunaenda kumpa access zaidi afanye madudu zaidi? Kikwete is not serious at all.

Ulishamsikia Mkullo alivyokuwa anajigamba kwa u-consultant wake wa "dollar 2,000 kwa mwezi"

Watu wengi walikuwa na expectations kubwa sana walipoona Kikwete anachukua muda zaidi kupanga timu, kuja kuona matokeo anaendelea kuboronga tu kama kawaida yake.

Repulsive,
 

Huh????? Tunaongoza kweli? Tupe statistics mkuu!!!
Na hiyo sentensi yako ya mwisho, Mkuu! GREAT INTELLECTUAL AUTHORITY!!!!Ndiyo maana napenda watanzania
!
 

Andrew Chenge na Mustafa Mkullo ni lazima waende na maji.
Hatutaki majangiri katika Baraza la mawaziri.

JM Kikwete umechemsha kwelikweli.

Ujue kwamba, muda wa Chenge na Mkullo kuvuliwa nguo ukifika MH Kikwete utabeba lawama zao kwa 100%, kama una masikio yakusikia na kichwa cha kufikiri waondoe sas kungali mapema.
 
Huh????? Tunaongoza kweli? Tupe statistics mkuu!!!
Na hiyo sentensi yako ya mwisho, Mkuu! GREAT INTELLECTUAL AUTHORITY!!!!Ndiyo maana napenda watanzania
!

Katika Afrika and EA UD is the only University among 20 best in ranking! Vyuo vya Uganda na Kenya wako nyuma sana kwa hili!

Sijui na mimi ni kigezo gani kingine Kitila anatumia kulinganisha Kenya na Uganda!
 

Hapa mkuu tuko pamoja ila nina haya machache ya kuongeza:

-Kuwaweka watu kama Nchimbi na Husein Mwinyi kwenye wizara muhimu ya Jeshi letu la Ulinzi na kujenga Taifa ni kulidharau jeshi hilo ambalo ni chombo muhimu sana kwa Taifa letu hasa katika kipindi hiki ambacho karibu majirani zetu wote wapo kwenye vita au machafuko ya kisiasa.
-Inaelekea JK bado hajaona umuhimu wa kupunguza timu yake pamoja na ushauri wote aliopewa.Nchi kama Tanzania kweli haipaswi kuwa na wizara zaidi ya 15!!kuwa na wizara zaidi ya 25 ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

-Naona mawaziri wengi wamewekwa si kutokana na uchapakazi au ufanisi au uwajibikaji au usafi bali ni sera zilezile za ushikaji,urafiki,kusoma pamoja,kuoneana haya na bila kuzingatia zile sera za ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya!.Hebu tuchukulie mfano wa Prof.Kapuya kweli huyu mtu anatufaa?? je kweli uchapakazi wake unaridhisha? mtu huyu kila kukicha anawaza kununua vipanya ili apeleke kule ISAKA-Shinyanga mpaka sasa ni mtu mwenye vipanya vingi kule ISAKA sasa swali linakuja kavipatapataje?????

-Kumpeleka Prof.Mwandosya wizara ya maji badala ya wizara ya Sayansi na Technologia ambako ndiyo mtaalam huko ni kukoroga mambo tu! Sijui ni kigezo gani kimetumika hapo..hebu nielimisheni.

-Kumuondoa pombe magufuli wizara ya ardhi ambapo alionekana kupamudu kabisa na kuweka mtu mwingine nikukaribisha lile wimbi la wageni kujitwalia tena ardhi yetu huku watanzania tukiendelea kunyanyasika.

Wembe Mkali
 


Mzee elimu ya juu tumeachwa sana hata kwa standard ya Afrika.
 

huyu ni MKULLO AMBAYE HATA kampuni yake ya DRY CLEANERS yenye makao yake makuu pale JENGO LA MWANAMBOKA kinodoni[former shoprite]..aliyoifungua baada ya kustaafu.....ilimshinda kuiendesha .....akawa anajiendesha kwa hasara ..hadi anapagawa...pamoja na kuwa na vifaa first class....

mpaka anaenda kugombea ubunge mwaka juzi ...2005 alikuwa taabani kipesa....sijui kiinua mgongo chake na biashara vilimshindaje...
pamoja na kuwa PERFOMANCE YAKE NSSF ILIKUWA NZURI....siwezi kujua utendaji wake kama waziri utakuwaje..baada ya kumshauri mama meghji kwa miaka miwili pale!!
 
Ngoja tuangalie kama kuna chochote cha maana hao walioteuliwa wataleta katika maendeleo ya nchi,lakini i doubt sana maana wengi ni wale wale tuu waliotufikisha hapa na sijui kama wana new idea...well,lets wait & see,ningeomba sana aniondolee Hosea na Mwanyika na apanngue ile TRA na Bandari maana kule kuna rushwa sana na watu hawafanyi kazi inavyotakiwa,lazimaTRA iende high tech maana tunapoteza pesa nyingi sana kutokana na wazembe wala rushwa.
 
Wote mmesema vyema . Hapa ni JF ni mahali ambapo JK anajua kuna wajuvi .Weka data hapa kwa uwazi na sisi tutashika bango .Weka dara wacha uoga .
 
yupo wapi LUDOVICK MWAMANZILLA ..aliyekosoa SERA YA KIKWETE YA SHULE ZA SEKONDARI KATA ..kisema haukupangiliwa vema..ulipangwa kwa kukurupuka na kusababisha majengo yawe lakini walimu hakuna....inabidi asugue benchi...nahisi kwa maana hiyo utendaji wake na uke wa magreth sita haujafanikiwa!
 

Mzalendohalisi,

Wizara ya Chenge imemegwa katikati na sehemu imepeleka wizara ya science and Technology.

Yeye amebaki na barabara.
 

Sijui kama Mheshimiwa anahusika lakini yeyote mwenye kidole kwenye dili hii ya waHadzabe anastahili laana zote za mwenyezi mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…