Mtu wa Kwao
JF-Expert Member
- Jan 15, 2008
- 258
- 21
Jamani eeeeee sie tusubiri tu tusimlaumu sana jk.mi nadhani huyu chenge anayo ya kujibu mengi sana baada ya akina zitto nao kuwasilisha ripoti ya madini sie tusubiri..atajiuzulu mwenyewe kama akina karamagi.Yeye si ndio alikuwa mwanasheria mkuu kabla ya mwanyika ?
Aaaahhh aaaahhaa aaaahhhaa. Sometime Mh. Kikwete anatakiwa awe serious. Sasa kumrudisha mtu kama Chenge kwenye baraza hilo ina maana hakukuwa na watu wengine ambao wana-fit hiyo nafasi? Si huyu ametajwa kwenye baadhi ya scandal tena anarudi. Aliwahi kumtishia Mh. Slaa kuwa angekwenda mahakamani kwa kumzulia ufisadi na hadi mwaka kesho hataenda kufungua hayo mashitaka. Hapa kuna kitu JK anajaribu kufunika au..........??? Au ndiyo fadhila yenyewe ya SISIEM.
U know what, ngoma mdundo..... Tutaendelea kuwaumbua tu na ufisadi wao. Naamini kama JK hataki kumuweka kando huyo Chenge basi JF kwa kushirikiana na wenye uchungu na nchi watamuondoa kama walivyoondoka wenzake. Eti Nchimbi naibu wa Wizara ya Ulinzi, mmmh ndo fadhila hizo JK hakuna anayeshangaa lakini angalia sana Mheshimiwa sana maana mabomu yatazidi kuja. Ukiendekeza ushikaji mwaka 2010 utauona mgumu sana. Mmmh labda kutakuwa na mabadiliko mengine hivi karibuni, WHO KNOWS!!