kuhusu wapinzani kuwekwa katika Barza jipya la Mawaziri,Basi utabiri utakuwa umetimia,JK to be one term president.Kwanza itakuwa aibu kwa chama.ina maana chama kimekosa watu mpya achague watu wa upinzani??kama kashauriwa hivyo atakuwa anajimaliza mwenyewe katika CCM.
Upande wa Wapinzani kukubali kuingia madarakani ni kukubali kutekeleza seara ya chama cha Mapinduzi ambayo inapingana na sera zao,na ninavyofahamu kiapo cha pili anachoaapa waziri au Naibu waziri kinamfunga kufanya mambo kwa matakwa yake binafsi.(kumbuka Mrema).hapo hapo hata serikali ikishindwa kutekeleza Matakwa yao ina maana na wapinzani watakuwa wameungana nao katika hilo.
Huu utakuwa Mtaji Mkubwa wa kisisasa kwa wanasiasa kama Mtikila na Vyama Vyao ambao hawatakuwamo katika baraza la Mawaziri,Mtaungana nao katika uchafu wote wa EPA,Suala la Madini na mambo yote machafu ambayo CCM ya wafanyabiashara wanayasimamia. sababu mtakuwa ndani ya kiapo!labda mje mseme nje ya kiapo kwamba mlitolewa 'Bangusilo'.
Kimsingi kama Jk akiwap wapinzani na wakakubali,Basi sitakipa chama cha Upinzani Kura yangu,au ndio mambo ya kina Mzee Mwanakijiji,Kama ukiona mtu anakushinda unaungana naye?au ndio walichukuwa wanakitaka(rejea Hotuba ya Waziri Mkuu wakati akitangaza adhma yake kujizuru).
Kama Zitto,Mdee na Hamad Rashid Mko Tayari,Kila la kheri. Na huu ndio utakuwa Mwisho wenu kisiasa.Ndio mtakuwa mnawapa Ushindi CCM,
Naamini JF huru ndio itakuwa Chama Cha Upinzani.tusikate Tamaa Bali tuweke Msimamo thabiti sababu Subira huvuta Heri