Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Jaman mnataka kutumia kodi haramu inayotokana na nyama ya kitmoto.kodi kutoka kwa makafir walio haramu mbele ya mtume mud.hv kweli mbona munachafua ibada kwa kuwaingza makafr kuchangia mahakama ya kadh.bakhresa,manj na rostam aziz x waanzshe kama tatzo pexa.kama mnataka power ya sheria mnatka mgogoro
 
Kwani kuna aya katika dini yeyote ulimwenguni inayofahamisha katika katiba ya nchi kuwe na kipengele cha Sanaa pamoja na uigizaji?? Kwani mulipotunga katiba yenu mulizingatia kila kilichotajwa katika Quran kwa mujibu wa aya zilivyokuja?

Mbona Quran inafafanua haki za kila mwanamme na mwanamke kwa misingi yake maalum nyinyi mukaweka 50-50 kama kweli mulizingatia Quran?

Hapa Waislamu tumedai hii Mahkama ya Kadhi lengo tupate chombo kinachotambulika kikatiba na katika dola ya nchi ili kiweze kuzisimamia hizi haki ambazo tayari zimetajwa na kufafanuliwa katika Quran. Na wasimamizi wa chombo hiki lazima wawe ni waislamu ambao wamebobea katika kuchambua, kusimamia na kutoa haki kwa Waislamu.

Hata kama munakosa elimu ya utambuzi wa haya mambo lakini rudi katika nadharia ya kawaida utaweza kujifunza na kujuwa hasa Waislamu hapa wanachotaka ni kitu gani.

daah upo kidato cha ngap
 
Waislam walikwishatamka kuwa mahakama ya Kadhi kwa waislam ni ibada. Tukikubali tu kuwa ni ibada ni lazima ibada hiyo ifanywe na igharimiwe na waumini wake. Hili jambo lisipofanywa kwa umakini linaweza kuleta mtafaruku usio wa lazima.

Katibu yetu inatamka kuwa serikali yetu haitajihusisha na masuala ya dini, kwaajili ya kujenga utengamano mzuri ni muhimu tukaliishi hili. Serikali ishughulike na mambo ya jumla ambayo ni huduma kwa watu wote. Wenzetu waislam wanaizungumzia sana MoU kama ni uthibitisho wa serikali kujihusisha na masuala ya dini lakini kiuhalisia ni kuwa MoU ya serikali na taasisi za dini ililenga kwenye huduma zinazotolewa kwa watu wote (na siyo kwa kundi fulani la dini, ndiyo maana seminary school hazikujumuishwa, vyuo vya wachungaji au mapadre havikuingizwa. Kilichoangaliwa ilikuwa ni taasisi zinazotoa huduma kwa watanzania wote, wawe waumini au siyo waumini, wawe wakristo au Hindu, n.k.

Kama Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa waislam, tuiheshimu kama tunavyoheshimu mambo mengine yanayofanywa na imani mbalimbali lakini huwezi kumlazimisha mtu wa imani nyingine afanye au agharamie ibada ya imani ya mtu mwingine.

Na pia itambulike kuwa huyu Muislam anayeweza kwenda kwenye mahakama ya kadhi bado ni Mtanzania, akitaka kutumia Mahakama za nchi kwa nini alazimishwe kutumia mahakama ya kadhi? Kama ni masuala ya ndoa, labda itabidi wanandoa waulizwe wakati wa kufunga ndoa, watatumia mahakama ipi endapo kutatokea mgogoro unaohusiana na ndoa? Ukisoma huu waraka, inaonekana hawa Mashekhe wanataka kila muislam apende asipende ni lazima atumie Mahakama ya Kadhi na siyo Mahakama za nchi. Mimi sioni kama ni sahihi.

Inashangaza kuona mada ikiwa jambo la waislam/uislam basi kila mtu atakuwa mchangiaji hata kama uelewa juu ya hilo jambo. Ningeomba ndugu zangu wasio waislam waifaham kwanza mahakama ya kadhi na shughuli, nchi vipi zinafuata huo mfumo na athar zipi wamezipata kwa kuwa na mahakama ya kadhi. Lkn kinachoonekana hapa ni kejeli na matusi bila kufanya mjadala kwa hoja.
 
Na ni wapi katika katiba hiyo pendekezwa imetaja Haki za msingi za WAKRISTO??????! Kwa hiyo Waislam ni bora kuliko Wakristo nchini mwetu??! NDIO maana Tangu mwanzo Serikali ikatenganishwa na DINI... (Haya mwalimu Nyerere aliyajua yangetokea.. DINI Moja kujiona bora ndani ya katiba...Hakuna nchi tena hapo)...Ila Serikali Imara isiyokumbatia DINI na kuziacha DINI zijiendeshe na kujiamlia mambo nje ya mfumo wa serikali ndiyo sahii Kabisa ili kupusha huu Mvurugano).. Watanzania tujitambue..! ili kulinda umoja wetu..!
Ikiwa ndiyo msimamo wa Waislam, basi naam, kura yangu itakuwa ni hapana, siwezi kwenda kinyume na Waislam wenzangu hata siku moja, kinachotuunganisha Waislam ni kamba ya Mwenyeezi Mungu.

Hiyo katiba siioni ina maana gani kama haitambui kuwa kuna Waislam na wana haki zao za msingi.
 
Mbona kodi za waislam zinagharamia uezeshwaji wa MOU.
Mbona kodi ya muislam imeliwa na ASKOFU KILAINI kupitia MKOMBOZI BANK ,banki ya kifisadi inayomilikiwa RC.
Hiyo MOU ipo kwenye katiba.?
Mbona Kikwete kama Rais na kama Mwislamu alisema kama mnaweza na ninyi anzisheni MOU yenu serikali itaangalia namna ya kushirikiana na ninyi.

Ila kwa sababu ya ubinafsi wenu mnakazinia Kadhi tu sijui huduma za kijamii nani atawapigania ndani ya katiba.

Kuhusu Kilaini ni swala la kisheria, sio kikatiba.
Kama serikali inaona mhalifu amekula fedha za uma imshitaki kwa majibu washeria za nchi.
 
Mbona wasio wakristo wanatibiwa katika hospitali zilizojengwa kwa michango ya wakristo? Mbona wasio wakristo wanasoma katika shule na vyuo vilivojengwa kwa michango ya wakristo? Je, huyu Kilaini, Mkombozi bank na MoU vipo ndani ya katiba? Hebu tajeni ni vitu gani vya ibada ya wakristo vipo ndani ya katiba.

Mkombozi bank acted prudently and professionally on Rugemarila money. Askofu Kilaini ana makosa ya kimaadili lakini sina uhakika kama ana makosa ya kijanai. Kwa wale wasiofahamu ni kwamba Kilaini aliondolewa Dar es Salaam kwa makosa ya kulidhalilisha kanisa kwa kutoa kila mara matamko yenye utata. Kule Bukoba alikopelekwa anafanya kazi kama padre wa kawaida huku nafasi ya Msaidizi wa Askofu (Vicar general) ikishikwa na Padre. Title ya Askofu imekuwa ikikuzwa zaidi na wapambe wake ambao ni serikali kuliko ndani ya Kanisa.
Mbona kodi za waislam zinagharamia uezeshwaji wa MOU.
Mbona kodi ya muislam imeliwa na ASKOFU KILAINI kupitia MKOMBOZI BANK ,banki ya kifisadi inayomilikiwa RC.
 
sio kila kitu kuiga ya mwenzio,nchi nyingine kuna ndoa za jinsia moja na ni halali,mbona hatujaiga?we do what is in our best interest,..wakristo na wapagani wengi wanapinga hii mahakama kuingizwa serikalini,tusilazimishe tukaja kuleta vurugu huko mbeleni...mbona kuupinga ushoga tumekubaliana kwa pamoja!kama taifa,hakuna consesus kwenye mahakama ya kadhi kuanzia mitaani hadi bungeni,surprisingly hadi ikulu ilipinga hili swala.

Mimi nadhani siala sio wakati wake nakubaliana na wewe, baada ya kuruhusu hili jambo yatazuka makundi mengine nayo yatadai mahakama zao. Itakuwaje kama wakristo na wapagani nao wakidai? Sio kila ulionalo kwa jirani ni lazima ulipeleke kwako, mengine acha yapite.
 
Rejea ahadi za CCM wakati wa chaguzi, kama jambo haliwezekani kwa nini watoe ahadi wa kuanzisha mahakama? Point ya msngi IPO hapo
Ndugu hivi bado huwa unaamini ahadi za wanasiasa wakati wa kampeni?
 
mahakama hizo za nini!! kwenye katiba hii!! ambayo serikali haina dini ila watu wake!! hii inamaana ni kuvunja katiba ya nchi!!! Tanzania ina dini nyingi zote mnataka ziwe na mahakama?
 
JE? Kodi ya mauzo ya NGURUWE na POMBE biashara kuu ya Wakristo itaswihii kuendesha IBADA ya Kiislamu(Mahakama ya kadhi)????!!
Hivi ni upungufu wa ufahamu wako ama bado tukugeiye muda huenda ikawa khalafu ukajafahamu pole pole kwa kuwa yarukhusika sio....!?

Zile alizo idhinisha yule Mmasai na jopo lake ziende kwenye ati Spitali za Makanisa na Skuli zake (MoU) zile hazina tatizo kwakuwa zachangiwa na "KODI" za Wakristo pekee sio....!?

Hizo dhihaka na kujivika kwenyu upogo kwa upande mmoya wa Watanzania(WAISLAAMU) wenzenyu sasa tamati ndo yakuijieni kwa kwasi.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.
 
Na ni wapi katika katiba hiyo pendekezwa imetaja Haki za msingi za WAKRISTO??????! Kwa hiyo Waislam ni bora kuliko Wakristo nchini mwetu??! NDIO maana Tangu mwanzo Serikali ikatenganishwa na DINI... (Haya mwalimu Nyerere aliyajua yangetokea.. DINI Moja kujiona bora ndani ya katiba...Hakuna nchi tena hapo)...Ila Serikali Imara isiyokumbatia DINI na kuziacha DINI zijiendeshe na kujiamlia mambo nje ya mfumo wa serikali ndiyo sahii Kabisa ili kupusha huu Mvurugano).. Watanzania tujitambue..! ili kulinda umoja wetu..!


Kwani nyinyi mlikatazwa kudai haki zenu za msingi?

Kama mna sheria zenu ambazo mnaona hamtendewi haki na mahakama za Serikali mngekaa kimya mpaka leo?
 
Nani Ana mamlaka kutoa tamko kwa niaba ya ndugu zetu waislamu? Nani asikilizwe? Nani asisikilizwe? Na hapo ndo tatizo Lilipo.

masanja
Kwani nani ana mamlaka ya kutoa tamko la, kwa mfano, Wakristo? Tatizo ni nyinyi mnaotaka kuwapa Waislamu msemaji mmoja.

Nadhani serikali inakataa kwenda na wakati, inawezekana zamani zile BAKWATA moja ilikuwa inatosha kuwawakilisha waislamu wote, tena serikali ilifanya jambo la busara kuitambua BAKWATA kwa uzito wa kipeke. Lakini mambo yamebadilika, wananchi wameelimika, taasisi mbali mbali zenye mirengo mbali mbali ya kidini na mengineyo zinaibuka kila uchwao, serikali haiwezi kuchagua taasisi moja kuwakilisha watu wote.

Waislam wasiofungamana na BAKWATA wakadai mahakamani kuvunjiwa haki zao za equal protection under the law. Serikali inapoilea BAKWATA peke yake inafanya upendeleo unaokatazwa kikatiba. Kwa nini, kwa mfano, BAKWATA ndio iitangazie nchi sikukuu za kitaifa za Kiislamu?
 
Sisi tuna tambua kuwa serikali ya Tanzania si ya wakristo peke yao,ndiyo maana (Roman Catholic) tuna mahakama yetu "Canon law" Na haigharimiwi wala, haihitaji kuingizwa kwenye KATIBA...! Je? Nyinyi wenzetu hamuwezi kufuata mfano wetu??? Au nyinyi mnataka serikali iwe ya kiislam??!
Kwani nyinyi mlikatazwa kudai haki zenu za msingi?

Kama mna sheria zenu ambazo mnaona hamtendewi haki na mahakama za Serikali mngekaa kimya mpaka leo?
 
Tatizo ni kwamba Serikali haipo kusimamia interest za DINI za watu!! Bali DINI zinaweza kusimamia interest za wahumini wake zenyewe!!( Je serikali ina usishwa kuamasisha watu kuswali misikitini au kusali makanisani????! Mambo ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpeni Mungu.. Msichanganye madawa hapa...( Mahakama yenyewe musema ni IBADA ya Kiislam).. Sasa Biashara ya NGURUWE na POMBE ambazo ni biashara Haramu kwa uislamm sijui kama zitaswihii kuendesha hiyo ibada yenu.. Endeleeni kupaaza sauti uenda mkafanikiwa ibada yenu kugharimiwa na KODI za Biashara ya Nguruwe na POMBE)!!!
Kwa kuwa nyinyi hamjaomba na Waislam wawaige nyinyi? Kwendeni zenu huko!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom