Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bagamoyo lashiriki One Stop Centre

Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bagamoyo lashiriki One Stop Centre

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
6d8cd0c3-c0c2-49e0-ac0a-95722fa76e98.jpeg


Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bagamoyo limeshiriki katika zoezi la One Stop Centre linalofanyika katika Kata ya Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo, kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Zoezi hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Mji Bagamoyo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, likihusisha taasisi na sekta mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi katika eneo moja.

One Stop Centre hiyo inafanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mtambani, Kata ya Mapinga, kuanzia tarehe 22 hadi 26 Septemba 2026, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Kupitia ushiriki wake, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bagamoyo linatoa huduma na ufafanuzi kwa wananchi kuhusu masuala yanayohusu migogoro ya ardhi, taratibu za kufikisha mashauri Barazani pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na Baraza.

Zoezi hilo linawapa wananchi fursa ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa wataalamu wa Serikali na kupata ufafanuzi na huduma kulingana na mamlaka za taasisi husika.
 
Back
Top Bottom