Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Baraza la Chuo Kikuu Huria, limekaa kikao cha dharura na kuagiza Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Elifas Tozo Bisanda aombe radhi kwa Wizara ya Elimu, Chuo Kikuu Huria na Umma kwa waraka wa tahadhari ya #CORONAVIRUS alioutoa Februari 8, 2021.
Prof. Bisanda alitoa waraka kuwatahadharisha wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho kuhusu ugonjwa wa Corona. Baraza limebaini kuwa yalikuwa maoni binafsi na alikosea kutumia nembo za Serikali.
Aidha imedaiwa taarifa ya Prof. Bisanda imeonekana kukinzana na Sera ya Serikali juu ya tahadhari dhidi ya #COVID19 pia haikuwa na takwimu za kuthibitisha uhalali wa baadhi ya taarifa hizo.
Baraza limeagiza wanafunzi na wafanyakazi wa chuo waendelee na kazi na masomo kama kawaida. Pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Pia soma
- Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21
- Corona: Wizara ya Elimu yaukana waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT)