Tetesi: Baraza la Maaskofu (TEC)kukutana hivi karibuni

Tetesi: Baraza la Maaskofu (TEC)kukutana hivi karibuni

Mnada wa Mhunze

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
168
Reaction score
819
Vyanzo ndani ya Kanisa Katoliki vinatabanaisha kutakuwa na kikao rasmi cha Baraza la Maaskofu huku pamoja na mengine litajadili SINTOFAHAMU kubwa inayolikumba Taifa kwa sasa kuhusu suala la BANDARI.

"...baba Maaskofu watapewa mwaliko wa kutaniko ndani ya wiki hii na tayari Mhashamu Rais wa TEC alishatoa maelekezo kwa Katibu ili aandae ratiba ya kutaniko lile."

"....yaah, kama unavyoona jambo hilo limezua SINTOFAHAMU kubwa hadi ndani ya Waamini wetu sasa wao kama Wachungaji ni muhimu walijadiri ili pamoja na mambo mengine wawe na namna bora hata ya kulisemea kwa Jumuiya ya Waamini wao."

"...ni imani yangu utatolewa ( WARAKA ) na kutumwa kwenye Jumuiya za Wakatekumeni baada ya kutaniko lile."

Chanzo.
 
Sijui wanachelewa nini kutoa msimamo wao, hapa ndipo utakapowaona mawakala wa shetani wanavyoanza kumwaga povu.

Tanganyika yetu imetekwa, lazima sote kwa pamoja tusimame kuikomboa kutoka mikononi mwa mwarabu, na serikali ya mkoloni wa Tanganyika.
 
Mbona uwekezaji wa gas ya Lindi waliyopewa wazungu hauzui sintofahamu!?..nyakati zimebadilika,siyo 70,80,90s hii,wao wakae,wanywe divai,wapige goti mbele ya sanamu,dp watapewa bandari
Bado mawakala wenzako wa shetani nao waje..

Tuwekee huo mkataba wa wazungu wa gas hapa tuuone, kama nao ukiwa wa hovyo kama wa bandari kelele lazima zipigwe.

Usijidangaye kukwepesha hoja kivivu hivyo, mkataba usio na ukomo karne hii ni matusi sio kwa kizazi chetu, bali hata vizazi vijavyo.

Tanganyika lazima ikombolewe kutoka mikononi mwa mwarabu, na serikali ya mkoloni wa Tanganyika.
 
Duru ndani ya Kanisa Katoliki zinatabanaisha kutakuwa na kikao rasmi cha Baraza la Maaskofu huku pamoja na mengine litajadili SINTOFAHAMU kubwa inayolikumba Taifa kwa sasa kuhusu suala la BANDARI.

"...baba Maaskofu watapewa mwaliko wa kutaniko ndani ya wiki hii na tayari mhashamu Rais wa TEC alishatoa maelekezo kwa Katibu ili aandae ratiba ya kutaniko lile."

"....yaah, kama unavyoona jambo hilo limezua SINTOFAHAMU kubwa hadi ndani ya waamini wetu sasa wao kama Wachungaji ni muhimu walijadiri ili pamoja na yote wawe na namna bora hata ya kulisemea kwa jumuiya ya waamini wetu."

"...waraka ni imani yangu utatolewa na kutumwa kwenye jumuiya za wakatekumeni baada ya kutaniko lile."

Chanzo.
Nawaaminia,mapdre ni wasomi wa elimu Dunia Hadi Canon law,najua myakachojadili kitakuwa kina maslahi kwa watanzania
 
Hapo makachero wa kanisa,ukute wameshasafiri hadi Dubai na wameshaleta ripoti.Hao nina uhakika watajadili kwa kina,kuliko bunge,na inaweza ikawa na impact.Hilo kanisa,siyo mchezo,lina watu wake toka Ikulu hadi kwenye kitongoji na bila kusahau kwenye taasisi yoyote ile unayoijua,wewe msomaji,iwe kwenye dini,siasa au taaluma yoyote ile.Never underrate them.
 
Back
Top Bottom