Ni kweli haujasainiwa.
Lakini mtu anapokuletea mkataba huku akiwa hajaweka wazi baadhi ya mambo ya mkataba. Mfano: Time frame, fedha iliyowekezwa, serikali italipwa shilingi ngapi?, nk. Unamwona ana nia njema huyu?( Halafu, anakuambia wewe pitisha tu, usiwe na wasiwasi. Na wewe unakubali kupitisha)- Ukifanya hivyo tayari UMETAPELIWA. ( Kwanini?), Kwasababu ukishajifunga kwenye mkataba kinachofuata ni UTEKELEZAJI wa mkataba. ( Lakini, kwanini ukubaliane na masuala yenye sura ya uficho?).
Mkataba ukiwa wazi unakuwezesha wewe kupima FAIDA na HASARA na hivyo kufanya maamuzi yenye tija kwa nchi( siyo unabaki, kubuni faida usizoambiwa). Je, matarajio ya faida yakibuma?, Tunaambiwa hatutakiwi kufanya chochote dhidi ya DP WORLD ( milele). Huu ni mkataba mbaya kuliko wa Sultan Mangungo na Carl peters.