Baraza la Madaktari Tanzania(MCT) limchunguze Dr Omary wa Hospitali ya Selian Arusha ALMC

Mbona hatukuelewi, mbona Kama una chuki na uongozi? Kichwa Cha Habari hakiendani na mada uliyoleta? Ukweli hospital ya ALMC imebadilika sana, na kutoa huduma Bora zaidi Toka uongozi Mpya ulivyo ingia. Nyie Ni wale waharibifu ambao hamkujua uongozi huu Mpya unaweza kufanikiwa. Ebu Tulia usitupigie makelele kwa mada za kujitungia na zilizo jaa chuki.
Unamaanisha Nini ukisema ukabila?
 

Kwahiyo anataka tumsaidie arudishwe kazini! Anaonesha ni mkorofi.
Mkorofi na mvivu.
 

Mitanzania mingi mijinga mijinga mkuu.
Mtu akileta humu jambo la maslahi ya nchi utaskia fitna hizo mara majungu wakati humu ndio sehemu sahihi ili watu waone jambo lifanyiwe kazi
 
KKKT ni kanisa linalojiendesha kama taasisi ya mtu binafsi.
Kila Askofu ni mmiliki wa Makanisa kwenye Dayasisi yake kama alivyo mwingira.

Askofu mkuu wa KKKT Hana nguvu yoyote mana kila Dayosisi Ina Katiba yake.
Ni kanisa lililogawanyika kuanzia kwenye mitaa chini mpaka juu.

Wajirekebishe wawe na kanisa Moja Tanzania nzima lenye katiba Moja na mfumo mmoja wa kujiendesha na ajira.
Ndio maana wanaingiliwa sana na wanasiasa kulingana na maeneo badala ya mwongozo. Maaskofu Wanachaguliwa lakini hawana muda Maalumu wa ukomo matokeo yake ni urasimu na kugeuka kuwa wamiliki wa Dayosisi na uadilifu kushuka kwenye miradi ya kanisa.
KKKT haiandai watumishi wake kuanzia Nursary school . Watu wanaibukia TU vyuoni na sekondari wakati wa kutafuta ajira.
Usishangae kuona daktari asiye mwadilifu au asiye na sifa. Nilishangaa kuona kule Konde viongozi wanapinga maamuzi ya Askofu mkuu hadharani kwenye vyombo vya habari . Siasa za kipuuzi kabisa kwenye kanisa na mambo ya kiroho. Walipaswa kumwandikia Askofu mkuu barua na kutoa malalamiko yao. Yote ni Kwa sababu wanajua hakuna la kuwafanya mana Dayosisi ni Mali yao na Askofu wao . Ndio maana hata ajira zao ni za kupeana bila sifa wakati mwingine.
 
Sio kila chuo lazima ufanye MMed Surgery ndo ufanye Superspeciliazition. Hata hapo Kenya kuna chuo kinatoa MMed Neurosurgery.

Kikubwa ujikite alisoma miaka mingapi?! What if amefanya Mmed Neuro for good six years?!

Na hata hapo MUHAS muda sio mrefu wanaweza kurevise mtaala ili kuruhusu uwepo wa MMed Neuro.

Tatizo ni ukiritimba tu kwa watu waliopewa mamlaka. Wanaamini wao tu ndo wanastahili kuwa Neuro.

Imebainika nchi inapoteza wataalamu wengi wa kufanya Neuro kwasababu ya hilo daraja la MMed Surgery.
 
Mitanzania mingi mijinga mijinga mkuu.
Mtu akileta humu jambo la maslahi ya nchi utaskia fitna hizo mara majungu wakati humu ndio sehemu sahihi ili watu waone jambo lifanyiwe kazi
Kanisa limewachangisha waumini wake wewe unatuletea sisi malalamiko ili iweje!
 
Hatari sana endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Umeongea point mkuu, mfano mdogo tuu kipindi sisi tunapata kipaimara ilikuwa mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa biblia anapewa zawadi siku ya kipaimara.

Lakini tukashangaa wamebadili gia wakaanza kutoa zawadi kwa atayetoa sadaka nyingi.
 
Mimi nachojua hiyo Hosptali ina matibabu ghari sana kama unatibiwa Nje ya Nchi...
 
Nafikiri ungejikita kutueleza ukabila umeingiaje hapo kwanza na kwa nini unafikiri ni huyo Dr. Kisanga tu ndie mwenye hati miliki ya kuwa CEO na siyo vinginevyo! Usije ukawa ww ndio upo ki ukabila zaidi ndg! Pia kunywa maji kwanza uvute hewa safi nje ndani x 100, calm down ndio uanze kutililika kwa mpangilio, siyo hivi ulivyokuja maana hasira zako zimesambaa kila kona na hivyo kupoteza mantiki ya unachotuhumu...kinachoonekana hapa ni 'personal verndetta'! Hivi aliyekukaririsha kuwa ni lazima ufanye general surgery kwanza kabla ya kuwa specialist au superspecialist ni nani vile? Au aliyekuambia anayeamua 'standards' za udaktari ni muhi2 ni nani vile!?😳
 
Selian hosp ndio hosp ya hovyo pamoja na gharama kubwa vifo vya kizembe ni vingi sana,wanalazmisha kukaa na mgonjwa ili kupata pesa wakti hawana uwezo wa kumtibu
 
Mkuu umemaliza atakae bisha akapimwe akili
 
Hijasema success rate yake ikoje,
Anzia hapo kabla hujaenda kwenye failure rate
 
Watu humu JF ni matahila Sana, yaani mtu akileta Jambo fulani ambalo kwa maslai ya Taifa, mnamuita mfitini,
Mkuu hutakiwi kulaumu kwenye hili, Hili linasababishwa na Mitazamo tofauti ya watu hakuna Jambo Dunia binadamu wote watakuwa upande mmoja? Dini, Siasa, Makabila, Utafutaji wa pesa na mambo mengi huwa ina pande mbili, hata Mahakamani sometimes mtu amefanya kabisa kosa ila kwa taratibu za kimahakama anaonekana hajatenda kosa.

Hivyo ni utaratibu wa Kimtazamo miongoni mwa watu, usitegemee kuungwa mkono na kila mtu duniani utateseka sana
 
Selian haifai?? Wakati ndio kimbilio la wengi kwa Arusha au unataka watu waende wakafe pale Mount Meru hospital kwa huduma mbovu?
Nagikiri mleta uzi na hoja.
Selian ina mazingira bora sana na vifaa lakini kuna malalamiko mengi mno mkuu.
Miaka ya nyuma mimi mwenyewe niliwahi kuuguza pale kuna siku niliuwasha moto kwa madaktari.
Kuna uzembe mkubwa msipuuzie
 
Umeongea point mkuu, mfano mdogo tuu kipindi sisi tunapata kipaimara ilikuwa mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa biblia anapewa zawadi siku ya kipaimara.

Lakini tukashangaa wamebadili gia wakaanza kutoa zawadi kwa atayetoa sadaka nyingi.
Wanakosea sana.
Kanisa kubwa sana na Lina waumini watoaji sana lakini halina Shule zenye sifa za kuwafanya waumini wao Wapeleke watoto wao na kujenga falisafa za Kiluteri na kuandaa Vijana Kwa ajili ya kanisa la kesho na Taifa Kwa ujumla. Shule zimekua kama Mali binafsi ya Askofu na familia yake matokeo yake ni ajira za Upendeleo na wanafunzi wengi ni watoto watukutu wasio na sifa na kufanya shule kushika Mikia mana hawachujwi Kwa sababu wengi wao wameingia Kwa kigezo Cha watoto wa Fulani.

Kanisa la KKKT ni kanisa ambalo watumishi wake wanauza mpaka viwanja na Mali za kanisa bila hofu mana hakuna wa kuuliza mana Askofu asipohiji basi kila mtu anaufyata. Hakuna Cha askofu mkuu Wala nani kila mmoja na Dayosisi yake.Ndio maana migogoro haiiishi mana hakuna mwenye mamlaka na katiba ya pamoja.
Na hali hii ya utengano inajenga ukabila kwenye nafasi za utumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…