GE2025 Baraza la Maskofu Tanzania (TEC) lakanusha waraka uliosamba kwenye mitandao ya kijamii

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii mijamaa Ina chuki sana sana, nilikuwa sijaijua vizuri ila safari hii ndo nimeijua aisee.
 
Hii mijamaa Ina chuki sana sana, nilikuwa sijaijua vizuri ila safari hii ndo nimeijua aisee.
Mkuu, unawaonea Bure! Wao ni nani wakataze waumini wao kushiriki au kutoshiriki uchaguzi. Vitabu vyao vinaakisi, ya kaizari (serikali) yaachie kaisari na ya Mungu (kanisa) mwachie Mungu.

Msimamo wao walitoa kipalapala walipokataza watawa na si waumini wao kushiriki siasa ili wawe neutral maana wafuasi wao wana utashi wao. Kama ambavyo serikali inakataza kundi Fulani la waajiriwa wake kushiriki siasa ili wawe neutral mfano askari etc.

Wakatoliki walitoa rai kwa waumini wao kabla ya kuamua kupiga kura au kutopiga kura kujitafakari na kumuomba mungu amuongoze katika maamuzi. Akiamua kwenda kupiga kura napo ajitafakari nani wa kumpigia kura.

Kosa la kanisa lipo wapi? Naamini huu ndiyo msimamo maridhawa badala ya kanisa kuchagulia waumini wake. Hii ndiyo neutrality inayotakiwa kwa taasisi ambazo si za kisiasa.
 
Mwana Chadema yupo kazini nyuma ya pazia ya udini. Nadhani sasa ni wazi udini hata kama hatuwapendi CCM lakini waislamu tutapiga kura tu na mambo yataenda.
 
Hii hoja yako haina logic. Kanusho ni la muhimu. Tena kwa wakati bila kupoteza muda.
 
Mh, sawa mkuu lakini mioyo yetu (ukiwemo na wako) inajua ukweli kuhusu hili. Hizi harakati zao zinajulikana zinaelekea na kuegemea wapi
 
Hii hoja yako haina logic. Kanusho ni la muhimu. Tena kwa wakati bila kupoteza muda.
Pale inapobidi. Sio muda wote na jambo lolote mnapaswa kuwa mnatoa makanusho.

Kukanusha ni kuunga mkono jambo. Wahuni wanawabagaza, muamue kukanusha kitu kinachowapa wao uhalali wa ajenda yao.

Kuna muda mnaacha tu hasa mkijua ni wahuni wanafanya hizo mambo. Serikali inamkono mrefu kwa nini inashindwa kuwakamata hao wahuni wanaoibagaza na kutaka kugombanisha taasisi na waamini wake dhidi ya serikali.
 
Duniani Hakuna taasisi imara itaacha taswira yake igalagazwe mavumbini kwa habari zisizo za kweli na ikaacha kujibu. Labda wewe unipe mfano wa taasisi ipi ililishwa maneno ya uongo na ikakaa kimya tuwe na case study
 
Duniani Hakuna taasisi imara itaacha taswira yake igalagazwe mavumbini kwa habari zisizo za kweli na ikaacha kujibu. Labda wewe unipe mfano wa taasisi ipi ililishwa maneno ya uongo na ikakaa kimya tuwe na case study
CCM, serikali, polisi.. tume huru ya uchaguzi. Msajilinwa vyama vya siasa. Mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…