Baraza la Mawaziri 2020 Halina Ukanda, Udini wala Ukabila!

Baraza la Mawaziri 2020 Halina Ukanda, Udini wala Ukabila!

Quote aliyesema kimei kanyimwa uwaziri.

Afterall kimei sjui nini kimemuingiza ktk siasa, unapewa uwaziri unatukanwa mkeo na watoto wanakuonaje, watakuona poyoyo tu
umeona eeh, tukubali tu JPM kaleta baraza lenye sura ya kitaifa, wasio tutakia mema ndio wanasemaet , lina waislamu asilimia 3, mara mchagga mmoja, mara kimei kanyimwa uwaziri wa fedha, yani porojo zisizoisha.
 
Kwani hao kanda ya ziwa sio Watanzania?

Kipindi kile Kigoma ilikuwa na Mawaziri 3 hakuna aliyehoji.
1. MPANGO
2. NDITIYE
3. NDALICHAKO.

Na sasa hivi Kigoma ina mawaziri 2 hakuna anayehoji.

Halafu uwaziri siku hizi unagawiwa kwa ukanda au udini? Kwani mawaziri wanaenda kutekeleza sera za kanda au dini.

Kwenye suala la Ukanda ingekuwa Chadema kweli ningekubali kuwa kulitakiwa kuwe na mawawzir 50 kuwe na uwakilishi wa kila kanda.

Pumbavuu kabisa, sasa hivi mmeanza kuhubiri ukanda na udini utafikiri hii ni serikali ya kidini
Kwandikwa -shinyanga
Katambi -shinyanga
Biteko- shinyanga
Mashimba- simiyu
Kalemani -Geita
Mabula-Mwanza
Bashungwa- kagera
Waitara-Mara
 
Wengi wao hao mawaziri ni wahivyo kabisa afadhali kidogo Ndugulile,Abdullah na aweso
 
Wizara 23 tuu siko kila mtanzania anaweza kuwa waziri.
Kuna mambo mengine mengi tunaweza kufanya na yakaletea nchi maendeleo na heshma kubwa sana

Mungu ibariki Tanzania
Mikoa ipo 30, sasa sijui hawa watu walitaka kila mkoa atoke waziri hata kama hana sifa anazozitaka mwenye kuteua. Tulizoea kupeana tu vyeo hata kama mtu hana sifa ilimradi ionekana kuna kubalance maeneo. Hapo sasa ndipo tulikuwa tunajaza wale jamaa waliokuwa wakieleza makongamano ya kimataifa " Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zimbabwe uliofanyika mwaka one thousand nineteen sixty four.

Ni kweli kabisa tunahitaji wachapakazi hata ikiwa wote watatoka Kigoma sawa tu. Nani atapinga kazi ya Mpango na Ndalichako au Kabudi?
 
Kweli kabisa Bill
Tunahitaji watendaji wazuri bila kujali dini, kabila wala jinsia
 
Kwandikwa -shinyanga
Katambi -shinyanga
Biteko- shinyanga
Mashimba- simiyu
Kalemani -Geita
Mabula-Mwanza
Bashungwa- kagera
Waitara-Mara

1. Kwandikwa - Shinyanga
2. Katambi - Shinyanga
3. Biteko - Geita
4. Mashimba- Simiyu
5. Kalemani - Geita
6. Mabula - Mwanza
7. Bashungwa- Kagera
8. Waitara - Mara
9. Masanja - Mwanza
10. Mpango - Kigoma
11. Ndalichako - Kigoma
12. Ummy - Tanga
13. Awesu - Tanga
14. Kitila - Dar
15. Ndugulile - Dar

Yaani hawa watu wanaoleta hii hoja ni wabaguzi na ni bora walikosa uongozi wa nchi. Hiyo sera yao ya ubaguzi wa majimbo hapa ndio inajidhihirisha wazi
 
Kwani hao kanda ya ziwa sio Watanzania?

Kipindi kile Kigoma ilikuwa na Mawaziri 3 hakuna aliyehoji.
1. MPANGO
2. NDITIYE
3. NDALICHAKO...
Katiba inaelekeza kuzingatia usawa sasa haiwezi kutamka wazi usawa wa kidini au kikabila/kikanda.
 
Mawaziri mnashangalia alafu huyo rais ndio anaanza tena kuzunguka kutatua kero za wananchi hao mawazir sijui kazi yao nn
 
Kuna tathmini ya kawaida sana katika Baraza jipya!!

Wanawake 4
Wanaume 19....
Tunashindwa kutofautisha kuteuliwa na kuendelea kutumikia nafasi zao.

Hapa ndipo wengi tumejikuta tunajadili ukanda, udini, ukabila na jinsia, pasipo kujua hatujaelewa wapi.

Mtazamo wangu ni kuwa wengi wa Mawaziri ni wale wa Zamani, wangelikuwa wote wapya ndiyo walau tungeli thubutu kusema haya ya Udini, ukabila, Ukanda na jinsia.
 
Quote aliyesema kimei kanyimwa uwaziri.
Afterall kimei sjui nini kimemuingiza ktk siasa, unapewa uwaziri unatukanwa mkeo na watoto wanakuonaje, watakuona poyoyo tu
ali-tumbuliwa u-kurugenzi CRDB akawekwa abdul Majid, sasa Kimei badala ya kukaa nyumbani na kucheza na wajukuu zake kaenda kudanganya wamarangu eti katumwa na Magufuli agombee ubunge alafu atakuwa waziri wa fedha, hivi hizo nafasi lini vijana watashika kama mtu ana kitukuu kimoja na hataki kuachia nafasi?
 
Back
Top Bottom