Baraza la Wawakilishi Zanzibar latoa fedha zote zilizobakia kabla halijavunjwa kutengeneza Barakoa na kuwagawia wananchi

Baraza la Wawakilishi Zanzibar latoa fedha zote zilizobakia kabla halijavunjwa kutengeneza Barakoa na kuwagawia wananchi

Baraza la wawakilishi Zanzibar ambalo liko kwenye mkutano wao wa mwisho kabla halijavunjwa rasmi limeamua fedha zote zilizobaki kwenye akaunti zitumike kutengeneza Barakoa ambazo zitagawiwa bure kwa wananchi.

Fedha hizo atakabidhiwa makamu wa Rais balozi Seif ili azikabidhi kwa vikosi vya ulinzi watakaotengeneza barakoa hizo.

Naye balozi Seif amewashukuru wawakilishi hao kwa kutopuuzia madhara ya janga hili hatari la Corona.

Chanzo: ITV habari!
Safi sana Baraza la wawakilishi ZNZ!!! Huku kwetu wao wanawaza Posho tu kuzifakamia.
 
Zanzibar ni koloni la Tanzania [Tanganyika].


Bila shaka , hivi haya majeshi yao huku wameyasahau ?? hawatoi hata shilingi kusaidia koloni lake katika kupiga vita corona ??

Hivi wanataka hao majeshi , polisi na watu wasiojulikana wao waliozagaa kila kipembe huku Zanzibar , wakianza kupuputika kama inzi tukawatose baharini ?? maana ardhi ya kuwazika haipo huku au wanataka tuwapelekee Mabaniani wakawachome ??
 
Bwashee una uhakika?!

Nimecheka na hilo jina la "Bwashee", tulilitumia sana utotoni. Anyway, Bwashee shida kubwa ni kuwa hatuwezi fanya tafiti huru (si unajua tulivyofungwa vichwa na mikono). Lakini kama una muda tafuta thesis ya Mwakyembe ya 1995 (nenda repository ya udsm), isome ina mawili machache ya kuanza nayo kuhusu maswali ya Muungano
 
Back
Top Bottom