Baraza Madaktari Tanzania (MCT) lamgomea Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu Madaktari Watarajali

Baraza Madaktari Tanzania (MCT) lamgomea Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu Madaktari Watarajali

Wewe ndo una hoja za kijinga...

TCU iko chini ya wizara ya elimu..

Mabaraza yote ya taaluma yako chini ya wizara husika....

Mfano Baraza la madaktari (MCT),baraza la wauguzi (TNMC), baraza la wafamasia, baraza la wataalamu wa maabara yote yako chini ya wizara ya afya. Na yote utaratibu ni uleule wa kufanya mitihani kabla ya kupata leseni. Ni kiwango cha kufaulu ni kinafanana fanana ivoivo..

Hata Law School iko chini ya wizara ya sheria, haiko wizaranya elimu.

Sasa jiulize hao madaktari wanacholalamika ni nini? Qewe kwa akili zako MCT wanaweza kufanya jambo ambalo waziri hana taarifa nalo?

Mitaala ya Wizara ya Elimu (TCU) kuna mahali inapwaya. Sasa vijana wakija site wanakutana na mambo yasiyo na konakona ndiyo maana wanafeli..

Jiongeze acha uzwazwa..
Hivi una akili sawa sawa? Wauguzi na taaluma ziingine wana pre and post Internships? Msome vizuri mtoa post acha ufa.la
 
Ifike mahali mnzava atumbuliwe tu hiyo kazi anaifanya kimaslahi binafsi sana kama sio upigaji ni nini sasa hii tutamlaumu sana mama lakini wanaoharibia ni vikundi tu vya watu wachache kama hao MCT,waziri tumbumbua hicho kikundi maana hakijui kazi yao ni nini na nini wanatakiwa kufanya,hao hawana tofauti na wezi
MCT, TNMC, HLPC, PCT endeleeni kukaza ivoivo, hatutaki mazumbukuku maeneo ya kazi...

Wapikeni vijana vile inavyotakiwa, hizi kelele za mitaani zisiwasumbue...

Kule law school waliunda mpaka tume mwaka juzi. Nenda kafuatilie majibu yalikuwaje ndiyo utajua hawa intern doctors wanatakiwa wakae kwa kutulia..
 
Ninyi wana jf, msichojua ni kwamba hao MCT wasipokaza ili vijana waive, basi tegemeeni kutibiwa hovyohovyo siku za mbeleni, na msije mkamlalamika huku mitandaoni...

Shida kubwa inaanzia kwenye ufundishaji huko vyuoni, elimu ya huko imechekechwa kiasi kwamba vijana wakipewa mitihani ya critical thinking wanaangukia pua.

Hebu tuacheni kuleta siasa kwenye mambo serious.

Kinachotokea kwa madaktari, kinatokea pia kwa nurses,pharmacysts plus wale wazee wa law school... Wote hao kabla ya kusajiliwa lazima wafanye mitihani na wengi wao huwa wanafeli..
Tayari watu Kila siku wanaleta malalamiko Ila wahusika wanapochukia hatua tunaanzia Tena kuwalalamikia, niliwahi kupeleka mgonjwa Temeke Dr akakimbia akabaki kuhudumiwa na nesi Hadi akafariki.
 
Hivi una akili sawa sawa? Wauguzi na taaluma ziingine wana pre and post Internships? Msome vizuri mtoa post acha ufa.la
Wako njiani kuwa na pre na post...

Hata zamani hii ya kufanya mitihani ndiyo uwe licensed zamani haikuwepo. Ilikuwa ukimaliza intern unakuwa licensed directly...

Walioanza kuwa na post intern exams ni nursing, mwanzo walilalamika weeeh lkn mwisho wa siku wakaeleweshwa na kuelewa...

Ndiyo zikafuata hizo kada zingine kuwa na mitihani na wao...

Na kila baraza lina kanuni zake kulingana na sheria mama ya mabaraza yao... Kwenye kanuni za MCT wana pre and post exams..

NA KANUNI ANATUNGA WAZIRI.

Hivyo acha ufala mwenyewe mkuu, nenda kasome hizo sheria za mabaraza na kanuni zake... Ukikosa njoo hapa nikupe uzisome.

Acheni kuharibu mifumo thabiti ya kuzalisha competent products iliyojengwa kwa jasho na damu.
 
Tayari watu Kila siku wanaleta malalamiko Ila wahusika wanapochukia hatua tunaanzia Tena kuwalalamikia, niliwahi kupeleka mgonjwa Temeke Dr akakimbia akabaki kuhudumiwa na nesi Hadi akafariki.
Ni wapumbavu tu ndiyo watapinga hiyo mitihani...

Ila siku wakikutana na madaktari low score huku wakiwa na wagonjwa wao walio critical ndiyo watajua uchungu wa kufiwa na ndugu zao huku wanawaona bila msaada wa maana..
 
MCT, TNMC, HLPC, PCT endeleeni kukaza ivoivo, hatutaki mazumbukuku maeneo ya kazi...

Wapikeni vijana vile inavyotakiwa, hizi kelele za mitaani zisiwasumbue...

Kule law school waliunda mpaka tume mwaka juzi. Nenda kafuatilie majibu yalikuwaje ndiyo utajua hawa intern doctors wanatakiwa wakae kwa kutulia..
Hao hao ndo wanaowatibu kwenye hospital za rufaa na hata za mitaani kwenye, polyclinic n.k, hongera kwa kutibiwa na mazumbukuku!!
 
Ninyi wana jf, msichojua ni kwamba hao MCT wasipokaza ili vijana waive, basi tegemeeni kutibiwa hovyohovyo siku za mbeleni, na msije mkamlalamika huku mitandaoni...

Shida kubwa inaanzia kwenye ufundishaji huko vyuoni, elimu ya huko imechekechwa kiasi kwamba vijana wakipewa mitihani ya critical thinking wanaangukia pua.

Hebu tuacheni kuleta siasa kwenye mambo serious.

Kinachotokea kwa madaktari, kinatokea pia kwa nurses,pharmacysts plus wale wazee wa law school... Wote hao kabla ya kusajiliwa lazima wafanye mitihani na wengi wao huwa wanafeli..
Hujaelewa Uzi, kinacholalamikiwa ni mtihani wa pre enternship sio ule wa post internship. Ukumbuke internship ni sehemu ya training kumuivisha huyu mtaalamu wa afya kivitendo, hivyo kumpima kwa mtihani Baada ya hiyo 1 year training ni justified. Lakini lengo pre internship ninini??
 
Kanuni ndivyo zilivyo....

Na kanuni anatunga waziri...

Msajili wa MCT anateuliwa na waziri..

Unategemea kama waziri hajampa waraka wowote msajili ataacha kufuata almanac ilivyo?

Kwani mtihani wa pre intern una shida gani?
 
BARAZA MADAKTARI TANZANIA(MCT) LAMGOMEA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Baraza la Madaktari Tanzania(MCT) ambalo kimsingi ndilo lenye mamlaka ya kisheria katika kusimamia taaluma ya Utabibu nchini linalalamikiwa na Wanataaluma wa tiba hasa madaktari tarajali kwa kukiuka makubaliono yaliyotokana na majadiliano ya kikao kati ya wataalam hao tarajali pamoja na Naibu waziri wa Afya Dr Godwin Moleli akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu aliyefunga mjadala kwa kuunda tume ya kiuchunguzi juu ya malalamiko yao.

Wanauliza ni kwanini MCT wametangaza tarehe ya kufanya mtihani wa Pre-Internships mwaka huu wakati kamati ya Mhe Waziri bado haijatoa ripoti yake? Mwenye uhakika na usalama wa huo mtihani ni nani haliyakua watuhumiwa wanachunguzwa? Siyo ukaidi ni nini?

Ni takribani zaidi ya Mwezi mmoja kupita baada ya Mhe Waziri kutoa taarifa kuundwa kwa tume ya kitaalam itakayochunguza ni kwanini Wataalam hao wamekua wakifeli mitihani zaidi ya nusu ya watahiniwa wote? Hata kabla Kamati au Tume ya Mhe Waziri haijatoa Ripoti yake imekuaje MCT wanatangaza mtihani? Yaani wanachunguzwa halafu wanaendelea kufanya kile kile nicholalamikiwa, hii ni sawa?

OMBI/USHAURI KWA MHE WAZIRI.
MCT wasitishe kwanza kusajili watahiniwa kwa ajili ya mtihani ambao watungaji wake wametiliwa mashaka.
Kitu kiingine ni kwamba. Hakuna mantiki au hoja yenye mashiko kwenye kufanya mtihani wa Preinternship wakati kuna mtihani wa Postinternship, kwenye preinternship wanapima kitu gani hasa wakati wanafunzi hawa wamekaa darasani miaka 5 na wakafaulu katika vyuo walikotoka? Kama vyuo vingekuwa na walakini TCU wana kazi gani?

Mhe Waziri ulisema kwamba watakaofanya mitihani ya Preintetnships wataendelea na kazi mahospitalini haijalishi wamefeli au wamefaulu, hii maana yake nini? Nini mantiki,tija na umuhimu wa Preinternship zaidi ya siasa na kikundi cha watu wachache kujitengenezea posho kutoka pesa za umma ambazo zingefanya mambo mengine?

Hivyo basi, Mhe Waziri kwa niaba ya Watoa elimu ya utabibu nchini nikiwa kama mwalimu wa vijana hawa, sioni kama Baraza likiwatendea haki, tutapoteza wataalam wengi bila sababu za msingi. Tuige mifano toka kwenye mataifa ya wenzetu.

MCT wasitishe mara moja usajili wa watahiniwa wa mtihani wa preinternship mpaka tume yako itakapokuja na majibu Mhe Waziri.

KAZI IENDELEE!
Barua ya MH. Waziri ilielekeza kwamba wakati Tume inaendelea na kazi,MCT waendelee na program zao kama kawaida,kwahyo MCT wako sahihi.
 
Barua ya MH. Waziri ilielekeza kwamba wakati Tume inaendelea na kazi,MCT waendelee na program zao kama kawaida,kwahyo MCT wako sahihi.
Kwahiyo wangeendelea hata kuwafelisha vijana hata kama wanachunguzwa. Basi waziri hakua serious. Umewahi kuona mbakaji anayetuhumiwa akaendelea kubaka wakati anachunguzwa?

Nadhani hili Suala Ummy Mwalimu ameshindwa kazi Vijana Warudi kumpigia Rais magoti. Ummy analeta siasa na kwanza siyo mtaaluma.
 
Kanuni ndivyo zilivyo....

Na kanuni anatunga waziri...

Msajili wa MCT anateuliwa na waziri..

Unategemea kama waziri hajampa waraka wowote msajili ataacha kufuata almanac ilivyo?

Kwani mtihani wa pre intern una shida gani?
Nimekuambia acha ujinga, kwakua wewe na roho yako ya kutu unakula unajishibia na kujijambia hujui watoto wa maskini wako mtaani hawana leseni na hawajui ni kwanini wslisoma hiyo kozi.
 
Hao vijana enzi za Ulimboka walikuwa chekechea au shule ya msingi?

Fani ambayo WSatanzania hatutaki kabisa kusikia inafanyiwa ubishi na malumbano ni hii ya afya. Hatutaki "tarajali au darajali watuletee ujinga kabisa. Wakacheze na vingine wasicheze na afya zetu kabisa.
 
Back
Top Bottom