Barbara Gonzalez CEO wa Simba SC nakukubali kiutendaji, ila acha kumdharau Senzo Mazingisa kwani hujafikia hata 15% tu ya uwezo wake

Ni nani anamiliki hiki chombo bwana popoma?

Utani.

Sema huyu dada ana uswahili sana ndani yake..
Huyo Senzo mwenyewe naye ni Mswahili Swahili tu kama akina Masau Bwire na wengineo. Juzi hapa alikuwa amepost kwenye twitter 'vijimaneno' vya Kiswahili swahili, Oooh sijui vuvuzela imekuwaje. Hivi CEO anayejielewa anaweza kuandika Utopolo wa aina ile kweli?
 
Huyo mwanamke kaajiliwa lini na Fifa,au yeye kawa lini kiongozi wa events za kimataifa.
 
Tunaomba kuijua elimu ya bwana Senzo
Ya Gonzalez si umeiona hapo?
Hivi mfano Tanzania ikiandaa kombe la dunia, Unadhani kina mwakalebela watakosekana kwenye kamati ya maandalizi?
Nyie Simba mlimuajili kwa cv zipi
 
ACHA WIVU.
bakhresa alikuwa fundi viatu
Dunia inakwenda kwa kasi sana, Babra kutoka kusimamia upishi wa mikate na Juice za MO mbaka kuwa mtendaji mkuu wa Mbumbumbu fc.
 
Kipindi Simba anafika robo finalise Champions 🏆, CEO alikuwa nani unataka mafanikio yapi zaidi ya hayo.? Mkuu.
 
Barbra yupo sahihi, huwezi fananishwa na mtu ambaye hampo level moja, ebu anayefaham cheo cha Senzo pale Yanga aniambia ana cheo gan na ofc yake ipo wap?

Barbra anafahamika ni CEO pale Simba, Senzo ni nani pale Yanga?
 
Mimi ni mwanayanga. Ila nachoona hapa ni chuki binafsi na mfumo dume. Barbara kufika alipofika ni uwezo.tuacheni udaku kwa wanaume si jambo zuri. Ana mahusiano yapi na Mo? Huu uandishi wa insta na fb mnapoleta JF kuja dhalilisha jinsia sijambo jema. Kuna siku mama yako atachaguliwa nafasi flani kwa uwezo wake. Then feel watu wakijasema amechaguliwa sababu ana mahusiano ya kimapenzi na aliyemchagua. Sidhani kam ni sahihi ikiwa hamna uthibitisho. Achen utoto kwenye mambo ya msingi.
 
Yule aliyekuwa CEO wa Simba bwana Magori leo amesema kwamba Simba kocha hana nafasi ya kusajili wachezaji.

Unategemea mtu Professional atakaa kwenye genge la wahuni kama hao?
 
Huyu dada ananyambulika vizuri zaidi ya senzo
1.Anajua mahusiano ya kitaifa na kimataifa

2.Anaongea vizuri kireno, kiingereza, kifarasa na kiswahili
 
Yule aliyekuwa CEO wa Simba bwana Magori leo amesema kwamba Simba kocha hana nafasi ya kusajili wachezaji.

Unategemea mtu Professional atakaa kwenye genge la wahuni kama hao?
Professional nani?
Huyu aliyekimbia baada ya kushindwa kukamilisha yaliyomleta?
 
Ameteuliwa kuwa CEO kupitia mchakato gani?

Au simba ni mali ya Mwamedi?
 
Ameteuliwa kuwa CEO kupitia mchakato gani?

Au simba ni mali ya Mwamedi?
Hata ikiwa mali yake nadhani si jambo baya. We unamiliki nini? Senzo tunaye yanga ana nafasi gani? Ilitumika njia gani kumpa nafasi hiyo? Mi nadhani Yanga tuachane na wivu wa kike. Ni aibu kwa wanaume kukaa na wivu,husda na kijiba. Huyu dada kwa kweli ame ibrand sana Simba. Sana. Kwetu senzo apewe cha kufanya.

Simba chini ya Mo imenawiri na ndo kinachotuumiza sisi Yanga. Tunabaki hangaika. Tumesahau miaka ya Manji alikuwa ameifanya team yake akihudumia kila kitu.
 
Usimba na Uyanga usikutoe kwenye uwezo wako wakawaida wa kufikiri. Yaani serious Gonzalez kamzidi Senzo kimafanikio hapo Simba?
 
Mudy anafaidi jamani hata kama mimi ningekuwa mkude nisingevumilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…