Hersi namkubali kwa uongozi thabiti ila huyu jamaa ana katabia flani ka mashindano yasiyo na tija na nadhani ana ule moyo wa kufanya kitu hata kama hakina faida kikubwa kiwe kinamuumiza mpinzani wake. Hivi inawezekanaje kwamba kila anae zinguana na makolo ghafla anakuwa anahitajika na Yanga? Kwani tunashindwa kutafuta watu wetu tukawaajili, si wanayanga wamejaa nchi nzima na nje? Kwamba tulikuwa na sababu gani ya kumrudisha Morrison, kumchukua Manara na leo Barbara? Hersi akue, aache mashindano kama vijana walio kwenye barehe.