haa hi kitu ni balaa, maana kuna siku baada ya kunyolewa nikaambiwa niende kuoshwa kichwa pamoja na uso, huyo dada aliyekuwa anafanya hii kazi haki ya mungu alikuwa keshanitia kishawishini, maana ananiosha uso na sehemu ya masikio alafu akawa anaingiza vidole vyake masikioni kwa makusudi kabisa, kufika kwenye kidevu ndio alikaa kama dakika kazaa akikiosha tu huku ananiangalia kwa macho malegevu kabisa, alikuwa kavaa kasuruali kepesi basi akawa anasogelea goti langu na kuliweka katikati ya miguu yake na huku kama anajisuguasugua,
nilikuwa mpole nasubiri ushahidi tu
wakina mama (mlioolewa) kweli mna kazi (bar maid, house maid, networking friendz, and now berbershop ladies)
Yes, this is a new threat for marriages. kwa kweli kama umeoa na unaipenda ndoa yako jiepushe na hizi barber shop, bora ununue scrubs and massage lotion mkeo awe anakufanyia home if you so like it. Na nyie kina mama/dada, jifunzeni hii service muwe mkiitoa kwa waume zenu huko home, bila hivyo kwa kweli only time can tell.
natafuta investors wa kuja kuanzisha hooters!
Itakuwa the first hooters in africa. Sasa sijui itakuwaje hapo mjini?
Yes, this is a new threat for marriages. kwa kweli kama umeoa na unaipenda ndoa yako jiepushe na hizi barber shop, bora ununue scrubs and massage lotion mkeo awe anakufanyia home if you so like it. Na nyie kina mama/dada, jifunzeni hii service muwe mkiitoa kwa waume zenu huko home, bila hivyo kwa kweli only time can tell.
kama mtu ni mhuni ni mhuni tu na mwungwana ni mwungwana.siku hizi madem wanajirahisisha kwa wanaume sijui maisha magumu au ni laana.mtu mstarabu hata akienda salon si lazima atoke na mhudumu tatizo nadhani ni tabia za mtu tu
Vipi wamasai wanaowasuka wake, dada zetu huku dada wakikaa chini wakati huo mmasai akiwa amesimamia! Uchunguzi unaonyesha wamasai wa kiume wengi huwa hawavai nguo za ndani! Kwa hiyo unakuta mwanamke anapata flava ya kingómbe ngómbe mpaka amalize kusukwa!
sa si ungemaliza tu, mtu anakulegezea kabisa?
Seto huyu Mkuu Kituko alimaliza ila kaamua kuminya details nyingine.
Mkuu BAK,
Nilikemea mkuu, unajua hivi vitu vipo kabisa yaani unakuwa tempted kabisa, kwa sasa nipo mwangalifu sana na hivi vitu, yaani hawa na Bar maid ni kundi moja, mora Bar Maid unaanza kutamanika kwa mbali, lakini hawa wanakugusa kabisa ni balaa kubwa
Vipi kuhusu maradhi hamjafikiria na hizo scrub zenu? maana vitaulo tunachangia na mikono ya wadada pia?
I suggest this should be intervened!
Yes, this is a new threat for marriages. kwa kweli kama umeoa na unaipenda ndoa yako jiepushe na hizi barber shop, bora ununue scrubs and massage lotion mkeo awe anakufanyia home if you so like it. Na nyie kina mama/dada, jifunzeni hii service muwe mkiitoa kwa waume zenu huko home, bila hivyo kwa kweli only time can tell.
Hili suala la sehemu za kujikwatua na kutanashitika zina athari siyo tu kwa ndoa bali hata kiafya.
Kuhusu athari katika ndoa, binafsi nadhani kila mahali kuna athari kama tutaangalia kwa undani.Ni mtu binafsi kujihadhari na mitego.Mara nyingi mchezo mchezo mtu hujikuta kwenye hatari.Kuanzia majumbani kuna wale wadada wasaidizi tumesikia nao huhatarisha ndoa, ukienda maofisini nako usiseme, kwenye sehemu za starehe nako si haba. Hata mitandaoni nako hivyo hivyo .Kwa hiyo hakuna palipo salama.Usalama utapatikana ahera peke yake.
Tukija kwenye suala la usafi, kwanza kitu ambacho nimekiona kwenye hizo barber shops - hao wanaofanya " facial scrub" hawana hata moja walijualo kwenye ufanyaji facial scrub.Ukitaka "facial" yauhakika nenda kwenye saloon zenye specialisation hii na huwa ni ghali siyo bei chee kam humo kwenye barber shops maana hii ni taaluma inayokaribiana na tiba kama siyo tiba.Inatakiwa isomewe ili mtu ajue hasa anafanya nini na kuzingatia taratibu za afya ya ngozi na mambo mengine kama mzio nk.kitu cha kusikitisha sana utaona hata mataulo wanayotumia wanayarudia na hata kufua hayafuliwi. Ukizingatia kuwa wanaume hunyolewa ndevu na wengine wana mapele na huenda mikwaruzo, mtu haoni anajihatarishia afya yake.Yuko radhi aka enjoy hizo huduma za kushikwa masikioni nk.
Kingine ni handling ya products za scrub.Kitaalamu au kiafya, haipaswi kuingiza vidole kuchota ile scrub bali inatakiwa ichotwe ama na spatula au kijiko maana ni kama uji fulani ambao huweza kuzalisha bacteria.Sasa mtu anapoingiza vidole tena ambavyo siyo sterile humo, bacteria wanajizalisha kwa wingi na matokeo yake huweza kuambukiza magonjwa. Yako mengi sana kwenye hii ishu lakini kwa leo naishia hapo.
Tip:
Ushauri kwa wale wasiokuwa na agenda tofauti zaidi ya kutaka usafi wa ngozi ya uso, nenda supermarket au duka la vipodozi, nunua products za ku scrub na ziko za kila aina - bei huanzia 3500/- hadi 30,000/= kutegemeana na unataka nini. Unapooga au kunawa uso, tumia . Au mwambie mkeo/ mpenzi wako akutengenezee home-made - changanya unga wa ulezi au hata oats na maziwa , sugua uso wako na kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.Waweza pia kutumia limao au ndimu kutakatisha uso wako.
Mimi naenda huko kukata nywele tu, hayo mengine siyajui na nikiambiwa kuwa nahitaji huwa nakataa haata wanaponiambia bei haiongezeki. Siku ya kwanza baada ya mwanaume kunikata nywele akaondoka bila kuondoa kile kitambaa wala nywele, kazi hiyo ikafanywa na mdada ambaye baadae aliniambia twende akanioshe kichwa (sasa sijui ni kilichokatwa nywele au kile kingine!) - nilimwambia nitaoshea nyumbani - hii inataka commitment kwenye ndoa yako tu. Mbona salon za wanawake kuna midume na vitanda vya kupumzikia?